Tumekosa ustaarabu katika kusitiri miili ya wenzetu

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,968
Ndugu wanaJF,

Katika ajali iliyotokea juzi Arusha,kila mtu atakubaliana nami kwamba utaratibu mzima uliotumika katika kuwasitiri wenzetu haukuwa mzuri na sahihi.Jana katika kipindi maalumu cha Clouds TV,mmoja wa wazazi pia alilalamikia hili.Maiti za watoto zilizivyotolewa kwenye korongo,wengine wana kiatu kimoja,wengine wana soksi moja mguuni na wengine nguo zao zimevuka kabisa.

Mbaya zaidi hata uondoshaji maiti eneo la tukio mpaka mortuary,kwa kutumia pick up na miili ya watoto imepandana hapakuwa na ustaarabu hata kidogo.Niombe tu mamlaka husika ijue kwamba,machungu ya mzazi yanaongezeka sana hasa baada ya kuona mwili wa mwanae ukiwa katika state ya namna hiii.

Mtoto wa mwenzio ni mwanao.
 
Hata ktk mitandao ya jamii watu kutuma pics hizo kila mara sidhani km ni ustaarabu mzuri, na kuwatendea haki hawa malaika pamoja na wazazi, ndg na jamaa !!
 
Nakubaliana na wewe asilimia zote.. Watanzania wengi wana moyo wa kusaidia wakati wa ajali. Lakini wengi hawajui nini cha kufanya wakati huo.

ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU ELIMU

Umma upewe elimu inayohusiana na ajali na uokozi..
Picha nyingi zinapigwa na kusambazwa bila hata tahadhari wala kusitiri sehemu zisizostahili kuonekana.. Wengine wamefunikwa majani daah!

TCRA... Mamlaka husika where are you?? Ondosheni hizo picha kwenye mitandao ya kijamii
 
Ni kweli Mkuu.
 
Nilzani ni mimi tu nililogundua hili. Kweli watu wanamoyo wa kusaidia lakini nadhani mbinu walizotumia si za kistaarabu we mwili unafunikwa kwa majani, hii ya wapi. Kwenye gari watoto wamepangwa kama mihogo utaratibu wa wapi huu.
Tujifunzeni jinsi ya kuhandle vitu bila kuhathiri utu wake, na tusivo endelea kua na staha tunaendelea tu kusambaza hizo picha.
 
Aseee mkuu nilidhani ni Mimi tu nilikerwa na jinsi miili ya watoto ilivyotupwa kwenye karandinga ikiwa imepandana yaaan haipendezi kabisaaaa machoni mwa mfiwa, majambazi ndo wanastahili hilo
 
Jaman Tujitahidi kuficha aibu za maiti ni kuwadharirisha marehemu na kuwapa uchungu zaidi wafiwa. Mungu azihifadhi roho za malaika hawa wasiokuwa na hatia na azidi kuzipa nguvu na subra na uvumilivu familia za wafiwa katika kipindi hiki kigumu.
 
Niliona miili ya watoto wale imefunikwa na majani imenihudhunisha sana
Mi niliona miili imefunikwa na shuka la MSD. Nadhani tuwapongeze walioacha shughuli zao na safari zao wakaenda eneo la tukio na kutoa msaada. Unaposema mtoto ana kiatu kimoja una maana gani jamani kwenye eneo la tukio ulitaka iweje? tuelewe kuwa wale waliotoa msaada ni wasamaria wema tu si wataalamu kama wa Redcross kwa mfano ambao hupewa mafunzo maalumu. Pale ilikuwa ni porini naamini kina mama waliokuwepo walitoa khanga zao kuwasitiri watoto kikubwa tuungane na familia na kuwaombea watoto, walimu na Dereva pumziko la amani. Maana kuna imani manung'uniko yakizidi yanawasumbua marehemu. Kwa sasa ni kuombeleza angalau basi tuache wazikwe salama. Hatuewezi jadiliana baada ya Kuagwa angalau?!?!?
 
Mkuu lilikuwa angalizo tu ili next time ustaarabu utawale.
 
Halafu yale magari ya polisi huwaga sio ya kubebea maiti mtu analazwa mle utafikiri mzigo.yaani kungekuwa na magari maalamu ingekuwa vizuri mijambazi wakiiua wanaiweka mle mtu akipata ajali anatupiwa mle
 
Hakuna atakayekuelewa mkuu,mfano mzuri saiv uwanjani wafiwa wanachukuliwa video na picha kiovyo kabisa basi tu nguvu ya kukataa hawana
kumbe na wewe umeona eeh, yani nimeshangaa kweli yani wakiona mfiwa analia sana ndo wanambandika kamera usoni ili tuone vzr sasa sielewi maana yake ni nini
 
Wanakwenda mbali zaidi wanamuhoji mzazi/mlezi aliefiwa arghhhhh naweza kukukata kibao unanihoji nikujibu nn,si upite tu useme pole
 
Back
Top Bottom