Tumekosa maadili. Tujisahihishe

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
723
241
Ukiangalia kwa juu juu unaweza ukadhani kama taifa tuko sawa. Wengine wanaona ndiyo uhuru na demokrasia. Mimi naona tunaelekea kubaya kama hatujafika pabaya!

Taratibu tunaanza kuwa taifa la watu wanaoshabikia vurugu. Watu wanajichukulia sheria mkononi. Wanafunga barabara na kuharibu mali za umma kama kuchoma moto barabara au kuchoma vituo vya polisi. Wafugaji wanaharibu mashamba ya wakulima na wakulima wanaua mifugo ya wafugaji. Labda utasema hao ni watu wasio na elimu na huenda wamekata tamaa.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana tulishuhudia vurugu katika maeneo mengi. Ama kati ya wapenzi na washabiki wa vyama vya siasa na wanasiasa binafsi, au kati ya vyombo vya usalama na raia.

Vurugu zimeendelea kushamiri bungeni. Baadhi ya Wabunge wanatumia lugha ya kuudhi. Wengine wanazomea. Wengine wako tayari kupigana bungeni, jengo ambalo twaaminishwa ni tukufu. Wananchi wengine wanafurahia kuangalia vurugu za bunge kwenye televisheni. Wengi wao wanasema hiyo ndiyo demokrasia. Kidogo kidogo tumekuwa taifa la watu wanaoshadidia vurugu. Tofauti za mitazamo ya kisiasa zimeleta chuki katika jamii.

Sasa tunashuhudia wanasiasa wabunge wakilumbana na hata kutaka kupigana na wanasiasa walio nje ya bunge. Mifano ya karibuni ni vurugu zilizowahusisha DC Makonda na Mbunge Kubenea; hivi sasa wawili hao wana kesi mahakamani. Hivi majuzi tumeshuhudia DC Kasesera akikabiliana na Mbunge Msigwa. Ilikuwa nusura watwangane masumbwi. Nasikia wote wamepitia mafunzo ya mapigano na kujihami. Sijui nani angeibuka kidedea.

Kwa nini tumefika hapa? Kwa maoni yangu, taifa limekosa maadili.

Nini kifanyike? Serikali na vyama vya siasa viandae viongozi. Vijana wapatiwe mafunzo ya siasa na maadili. Wakumbuka enzi za Chuo cha Chama Kivukoni? Nafahamu chuo kimeanzisha programu ya mafunzo ya maadili kwa wanasiasa na watu wenye dhamana ya uongozi. Hatujachelewa, tujisahihishe.
 
Kuna vituko sana nchi hii

1. Leo Jecha anatoka na vifungu vya sheria, hakuwahi kueleza vifungu vilivyompa haki yeye binafsi au tume ya uchaguzi kufuata uchaguzi

2. Jecha hajatoa kifungu cha katiba kinachoonyesha utaratibu wa uchaguzi wa marudio. Nimeipitia katiba ya ZNZ ya 1984 na marekebisho yote sikuona kitu kinaitwa uchaguzi wa marudio wa nchi nzima isipokuwa wa eneo lenye utata

3. Jecha hajatoa kfungu anachosimama nacho kufuta matokeo.
Alikuja na malalamiko 10 ambayo leo hayaongelei amebaki na la kujitangaza

4. Jecha hajaonyesha kifungu cha kujitangaza kinatoa hukumu gani kwa aliyefanya

5. Jecha anasema majina yatakuwa yale yale bila kutueleza sheria za tume yake na katiba zinasemaje

6. Jecha huyo huyo anayesema wagombea ni wale wale anatoa ulinzi kwa waliokubali kushiriki. Hawa waliokubali kushiriki ni wapi ikiwa majina ni yale yale kama alivyosema hapo juu?

7, Jecha anasema tume itatoa ulinzi. Ulinzi na usalama wa wagombea hautolewi na tume kwasababu si mamlaka yake. Tume inaomba ulinzi kutoka vyombo husika!

8. Jecha aliwahi kukaririwa na gazeti moja akisema amethibitisha vyama kutoshiriki.
Leo hajarudi kufuta kauli ile anapandikiza nyingine. Jecha anajua anachosema?
 
Vyama vingi vinachangia katika kukuza hulka za kambale, kila mtu anazo ndevu kuanzia mtoto mpaka babu. Kila mtu anazijua haki zake, ni vurugu mechi, hakuna tena heshima wala staha. Ikiwa wabunge wanapelekewa polisi ili watulizwe munkari unategemea nini kwa taasisi nyinginezo nje ya bunge?.
 
Back
Top Bottom