Tumejipangaje kukorofishana na makampuni makubwa?

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,602
Habari wana JF,

Sio mwandishi sana wa mada jukwaa hili ila nimoeona ni jambo la msingi sana na linahitaji mjadala mpana wa kitaifa. Ni matarajio yangu post hii ifungue mijadala Bungeni na Serikalini na matokeo yake mtaani. Mada yenyewe ni kama ilivyoandikwa, tumejipanga vipi kukorofishana na makampuni makubwa? Na hapa nitatoa mifano ya upande wa Tehama, lakini mada hii inaweza kumaanisha yoyote kati ya makampuni ambayo sisi tunayategemea kuendelea na maisha yetu ya kila siku.

Watu au serikali hutofautiana mitazamo na makampuni, na ni kawaida. Mwanzilishi au waajiriwa wa kampuni hutengeneza utamaduni wa kampuni. Mtu yeyote anayekwenda kinyume na utamaduni huu au mrengo wa kampuni huwa haangaliwi vizuri. Zamani hii haikuwa shida kwa kuwa makampuni yalijitahidi sana kujitenga na mambo ya kisiasa au mapingamano ya mitazamo. Lakini ukweli ni kwamba zama zimebadilika. Nitatoa mifano michache ya kuonesha hili.

Baada ya uchaguzi wa Marekani kwisha, rais wa nchi hiyo Donald Trump aliondoshwa kwenye akaunti zake za Twita, Kitabusura, Discord, Insta, Pinterest, Reddit, Shopify, na mingine mingi. Tafadhali pitia hapa kupata kwa undani. Lakini pia alizuiwa kutumia mifumo ya malipo kama Stripe. Wengi watatofautiana misimamo na Trump na hilo ni sawa na wala sio msingi wa andiko langu. Kwamba unakubaliana kuwa Trump alishinikiza watu wafanye fujo ama la, ni wewe mwenyewe kuangalia ushahidi uliopo na kuamua mwenyewe. Kwa wale ambao wangependa kuangalia Tweet za mwishoni zilizosababisha ban zipo hapa na habari juu ya lile tukio yenye hotuba yake ya Jan 6 ipo hapa baada ya Jan 6 Ipo hapa.

Point yangu ya msingi hapa ni kuwa hawa jamaa walifanya haya ndani ya muda mfupi sana jambo ambalo linaonesha walikuwa na mpango kabambe wa kufanya hivyo kwa lengo maalum. Hapa Trump aligusa maslahi yao ya kimtazamo na utamaduni wao na aliipata freshi! Kitendo cha kumfungia Rais wa nchi kutumia mpaka vitu kama Shopify ambavyo kimsing havihusiani na mitandao ya kijamii bali manunuzi na mauzo kinaonesha wazi hatari iliyopo hawa jamaa wakikuamulia. Kwa hakika kama Rai Trump alikuwa na makosa, ilikuwa ni kazi ya Bunge lao kumuadhibu na kama kulikuwa na jinai kuna vyombo ambavyo ndio vyenye mamlaka ya kushughulikia hayo. Hii mitandao sio kazi yao kuwa mshtaki, hakimu na mnyongaji.

Hili halikuishia hapa, Serikali ya Australia, kwa kulinda maslahi yake kama nchi huru na vyombo vyake, iliona kuna haja ya kutunga sheria inayohakikisha vyombo vyao vya habari vinanufaika na habari zao zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii. Kilichofuata ni vitisho toka kwa jamaa wa Kitabu sura kuwa watazifungia habari za Australia. Yaani kampuni inaipiga mkwara nchi yenye nguvu kama Australia. Waziri mkuu wao naye aliwachimba mkwara kuwa hawatishiki. Serikali ya Australia ilipoendelea na miswada yake Kitabusura wakawafungia kweli, na kuonyesha ukorofi wakafungia mpaka kurasa za Wizara za afya za Majimbo yao.

Ni Juzi (26/4) Kitabusura wamemfungia mbunge wa Australia kwa kusema mambo ambayo hawajayapenda kuhusu Covid-19

Kwa Wavivu wa Kusoma anzia hapa
============================

Ni nini ninachojaribu kusema hapa? Ninachosema hapa ni kuwa, si raia wala serikali ambazo ziko salama na uwepo wa mitandao ambayo uamuzi unatolewa na mtu mmoja San Fransisco na madhara yanaikumba nchi nzima. Wana uhuru wa kufanya hivyo maana ni kampuni binafsi na ndio sababu ya andiko langu hili. Kwamba serikali na wadau waone kuwa tunapaswa kuwa na kampuni za ndani ambazo zitaweza kushindana angalau kwa mbali na makampuni makubwa ya nje. Mahali ambapo wataamua kutufungia kama nchi basi tutakuwa na sehemu ya kwenda.

Kukupa picha, kuna Watanzania wengi sana wanategemea Insta kwa biashara zao na matangazo yao. Lakini wanawalenga Watanzania na sio nchi za nje. Kwa kuwa hatuna mbadala wa ndani, basi tunalazimika kutumia Insta. Lakini je siku serikali yetu ikitofautiana na wazee wa kitabuSura na wakatufungia Insta, umeshawahi kuwaza hali itakuwaje? Au wakaamua kutufungia WhatsApp, IMO, Telegram, Uber, Bolt, n.k. kwenye co-ordinated assault tutafanya nini? Tuna alternative zaidi ya kupiga magoti?

Wengi hawajui kwa nini Google na Facebook walikubali kwenda mezani na vyombo vya habari ili kukidhi matakwa ya sheria ya Australia. Sababu ilikuwa ya kibiashara zaidi. Kuna kampuni ya ndani ya Australia ilichukulia ie kama fursa na ilikua kwa kasi sana ndani ya kipindi cha Mgogoro. Jamaa waliona wanalipoteza soko la kule na mwishowe wakaona kukubali ni bora kuliko kukataa. Wao ndio watakaoumia.

Ushauri wangu ni wa aina mbili. Moja tunahitaji kujenga Miundombinu ya kiteknolojia inayounganisha na wengine lakini ambayo inaweza kusimama peke yake. Kwa sababu dunia inapendeza ikiwa imeunganishwa. lakini ukweli ni kwamba kuna wakati unaweza kulazimika kusimama peke yako kama ilivyokuwa kwa Australia.

Tuangalie uwezekano wa kuweka mazingira ya kuwa na Data Centers kwa gharama nafuu. Soko lipo kama bei itakuwa ni nafuu. Makampuni zaidi yatawekeza na kufanya utegemezi wetu nje ya nchi unakuwa wa hiyari kuliko sasa ambapo hakuna namna nyingine. Hizi data centers ziwe interconnected ndani. Yaani hata bila internet niweze kuzipata data zote za ndani. Hapa ndio umuhimu wa mkongo wa taifa kufika kila wilaya unakuwa na umuhimu. Hii ni muhimu sana!

Pili serikali inapaswa kuangalia namna inayoweza kulea biashara zake za ndani ili kuhakikisha kwa kila biashara za nje kuna angalau teknolojia moja ama zaidi ya humu ndani. Hapa simaanishi serikali iingie kufanya haya mambo, bali iweke mazingira mazuri kwa biashara za ndani za ubunifu na teknolojia (na zingine ambazo tuko tegemezi kwazo) zinaweza kukua na hata kufikia mahali pa kushindana nazo. Zipo njia nyingi ila kwa sababu sio lengo la uzi huu, nitazitunza kwa uzi mwingine.

Tukiweza kufanya haya tutasogea sana na tutaongeza nguvu ya serikali, si tu kukusanya kodi nyngi kuliko sasa, au kuwa na nguvu ya kukaa chini na kuongea na haya makampuni badala ya kutishiwa na kunywea, lakini pia makampuni haya yatakua na kwenda kushindana nje ya nchi na kuleta kodi zaidi na kuajiri watu zaidi.

Niishie hapa.
Wasaalam!
 
Duh...
Angalia walivyokuja kuuwa ile kampuni ya kina Eric Mwenda ya WiA Group kwa kuwakaba na makodi ya kukuharibia maisha, Aiseee....uhasidi tu kwa kwnda mbele...

Siku tuna conflict kama ya Ukraine na Russia halafu tukafanyiwa kama alivyofanyiwa Urusi tutakuwa na ubavu wa kukoroma au ndi tutakubali yaishe?

The entire nation state of Russia is getting the "Gab treatment" by Big Tech and the globalist regime.
By that I mean they are being systematically purged from the internet all within the span of about a week.
Soma full story: https://news.gab.com/2022/03/04/the-deplatforming-of-a-nation-state/

Lakini Warusi kwa sababu ya kuwa na teknolojia za ndani walikuwa na uwezo wa kutunisha misuli na kuwalamba ban wakubwa kwenye teknolojia:

Russia appears to have retaliated by announcing it would restrict the social media platform. The Russian state-owned news agency RIA Novosti said on Friday the Roskomnadzor, the government department that regulates telecommunications and the internet in the country, issued an order against Facebook.
......
The Roskomnadzor and the Prosecutor General’s Office said on February 25 that they have, “in agreement with the Foreign Ministry, decided to recognize the social network Facebook as involved in the violation of fundamental human rights and freedoms, as well as the rights and freedoms of Russian citizens.”

The announcement was vague in terms of what or how the platforms would be restricted but early reports suggest that Facebook Messenger is the most affected as users are having difficulty connecting.

It now appears to have also done the same with Twitter.

The Kremlin has increased restrictions on both platforms, mere hours after Twitter banned Russians from advertising on its platform.

Soma fully story: Russia censors Facebook and Twitter after Facebook and Twitter pulled support for some Russian media

Jamaa wakiamua kutunyuka tuna cha kujitetea kiteknlojia?

Hatuna mbadala wa Instagram
Hatuna mbadala wa Twitter
Hatuna mbadala wa Facebook
Hatuna mbadala wa WhatsApp
Hatuna Mbadala wa Google search
Hatuna mbadala wa....

Hatuna Data Center ya kuaminika na locals
Hatuna...Hatuna...Hatuna!

Je tunasubiri yatufike kwanza? Au tumeshajikatia tamaa kuwa sisi ni no body?
What if wakati wa vita wakaamua kutumia Social Media kinyume na sisi? Tuna ubavu wa kuwazuia?

Jioni njema!
 
Siku tuna conflict kama ya Ukraine na Russia halafu tukafanyiwa kama alivyofanyiwa Urusi tutakuwa na ubavu wa kukoroma au ndi tutakubali yaishe?

The entire nation state of Russia is getting the "Gab treatment" by Big Tech and the globalist regime.
By that I mean they are being systematically purged from the internet all within the span of about a week.
Soma full story: The Deplatforming of A Nation State

Lakini Warusi kwa sababu ya kuwa na teknolojia za ndani walikuwa na uwezo wa kutunisha misuli na kuwalamba ban wakubwa kwenye teknolojia:

Russia appears to have retaliated by announcing it would restrict the social media platform. The Russian state-owned news agency RIA Novosti said on Friday the Roskomnadzor, the government department that regulates telecommunications and the internet in the country, issued an order against Facebook.
......
The Roskomnadzor and the Prosecutor General’s Office said on February 25 that they have, “in agreement with the Foreign Ministry, decided to recognize the social network Facebook as involved in the violation of fundamental human rights and freedoms, as well as the rights and freedoms of Russian citizens.”

The announcement was vague in terms of what or how the platforms would be restricted but early reports suggest that Facebook Messenger is the most affected as users are having difficulty connecting.

It now appears to have also done the same with Twitter.

The Kremlin has increased restrictions on both platforms, mere hours after Twitter banned Russians from advertising on its platform.

Soma fully story: Russia censors Facebook and Twitter after Facebook and Twitter pulled support for some Russian media

Jamaa wakiamua kutunyuka tuna cha kujitetea kiteknlojia?

Hatuna mbadala wa Instagram
Hatuna mbadala wa Twitter
Hatuna mbadala wa Facebook
Hatuna mbadala wa WhatsApp
Hatuna Mbadala wa Google search
Hatuna mbadala wa....

Hatuna Data Center ya kuaminika na locals
Hatuna...Hatuna...Hatuna!

Je tunasubiri yatufike kwanza? Au tumeshajikatia tamaa kuwa sisi ni no body?
What if wakati wa vita wakaamua kutumia Social Media kinyume na sisi? Tuna ubavu wa kuwazuia?

Jioni njema!
Mzee,wanasiasa katika maslahi yao hawajali chochote, watokee nchi maskini au tajiri,utakayeumia ni wewe na mimi pangu pakavu..
Bob alishupaza shingo mpaka anatoka madarakani..
Tukirudi Taleban ndio kabisa..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom