Elections 2010 Tumejifunza nini juu ya uchaguzi huu 2010?

Wakuletwa

Senior Member
Oct 31, 2010
134
9
Ndugu wana JF hatimae ule mchakato kama sio mchakachuo wa uchaguzi umeshapita na wote tumeuona kwa macho yetu. Je tumejifunza nini? Kumekuwa na malalamiko mengi sana juu ya uchaguzi huu ulivyoendeshwa. Kampeni hazikuwa na tatizo kubwa sana kwa kiasi kikubwa zilikwenda salama, tatizo lilianza kwenye mchakato wa kupiga kura.
Kwanza tume kama sio tumwa ya uchaguzi ilichelewa kwa kiasi fulani kubandika majina ya wapiga kura lakini pamoja na hivyo watu wengi hawakwenda kuhakiki majina yao mpaka siku ya uchaguzi wanyewe hili limechangia baadhi yetu kushindwa kupiga kura.
Pili
idadi ndogo ya wapiga kura hasa kwa hapa Dar: Kweli mimi mwenyewe nilishangazwa sana na idadi ndogo ya watu waliojitokeza katika kupiga kura kwa kweli mpaka sasa sijui ni kwa nini watu walikuwa wachache sana. Hii nayo imeturudisha nyuma sana katika kuleta mabadiliko.
Tatu
ni mawakala, jamani wana JF kama kuna wanaotuhujumu basi hawa nao ni miongoni mwao, mfano kituo nilichopigia mimi kura sijui kama walikuwepo maana mle ndani nimekuta watu kama watano hivi. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa limechangiwa na ukosefu wa pesa za kutosha kwa ajili ya mawakala haswa wa upinzani. Hivyo ni bora sasa kuanza maandalizi ya kuhakikisha kuwa tume au serikali inawajibika katika kuhakikisha kuwa chaguzi zijazo wakala wanalipwa pesa na tume au serikali kwa ujumla.
Nne ni mfumo wa upatikanaji wa tume ya uchaguzi kwa utaratibu huu wa sasa uliopo wa tume kuteuliwa na raisitakuwa ngumu kupata tume huru na ya haki, vile vile lililo baya zaidi ni kutumia wakurugenzi wa wilaya kuwa wakuu wa kusimamia na kutangaza matokeo katika majimbo hapo ndio hapafai kabisa kama ni uchakachuaji hapo ndio kwao. Haiwezekani kesi ya mbuzi ukampa chui aiamue labda chui huyao awe wa kichina!!
Mwisho nawaomba ndugu zangu tuhakikishe tunarekebisha hali hii sasa na sio kusubiri uchaguzi mwingine uje vinginevyo tutaishia kulalama bila suluhisho.Unafikiri nani atakubali kuacha hekalu lake kule Obey na masaki alilopewa na Serikali kirahisi rahisi hata kama ungekuwa wewe?

:peep:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom