Tumejiandaaje kwa majanga tunayoyatengeneza wenyewe?

Mafie PM

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
1,317
207
[h=5]Swali la Muhimu kwetu. Miaka zaidi ya 50 ya Uhuru..

Tanzania kama kuzima moto kwenye ghorofa moja tu ya PPF tower imetushinda kuifanya kwa wakati muafaka? je? Tunawezapambanaje yakitokea matatizo makubwa kama Tsunami, Katrina, Au iwapo watu wa Mtwara wataamua kulilipua bomba la gesi tunalolazimisha kuja Dar? Simaanishi kwamba watalilipua bomba ila ni tahadhari tu! ila kwa kuwa linalazimishwa na wenyewe wamesema haitoki! Hatuoni kuwa huu ni ugomvi wenye madhara? Tusiongelee sana mgogoro wa gesi ila tuongelee kuwa tumejiandaaje kukabiliana na Maendeleo yanayoweza kusababisha majanga tunayoyaandaa kwa sasa?
Kama Serikali haikuwa makini hadi wakazi wa Nyamongo wanakunywa maji yenye kemikali zisababishwazo na uchimbaji wa madini! Je kwa hili lenye mgogoro tumejiandaje?

Ni mawazo yangu tu sijaongea kisiasa.
[/h]
 
Back
Top Bottom