Tumejaza wapiga Kelele hatuna wanasiasa!!

Tumejaza wapiga Kelele hatuna wanasiasa!!

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,238
Kwa takribani miaka thelathini sasa nchi yetu imekuwa katika upungufu mkubwa sana wa wanasiasa, Nchi yetu imeichukulia siasa kama sehemu ya mtu yeyote aliyepoteza mwelekeo kuwa au chimbo la kujipatia utajiri wa haraka haraka. Hali ilianza kuwa na wanasiasa uchwara mpaka sasa tulipo kuna wasiasa watapia Hatima walio kwenye siasa kwa ajili ya kuchaguliwa tu badala ya kutekeleza vile wanavyoahidi.

Tanzania tuna Dira ya Taifa (Vission 2025) kama kiongozi cha kufanya mambo yetu kuelekea kwenye mafanikio. Lakini ni nadra sana kwa "wanasiasa" wetu kuwakuta kwenye mabishano yao wakibishania kilichomo kwenye dira hiyo. Hadi wakati mwingine unajiuliza nchi yetu inaendeshwaje??
 
Kigarama,viongozi wetu wamelewa madaraka.Sasa ni wakati muafaka wa kuwaamsha kwa kuwamwagia maji baridi ambayo ni kura ya hapana kwa wale wanaofikiria wanahaki ya kuiongoza Tanzania yetu na kujilimbikizia mali.
 
ni kweli kabisa hapa kwetu hakuna siasa ila wapiga kelele,angalia majirani zetu,japokuwa siasa zao zina ukabila,lakini wanajitahidi kuungana,kwaajili ya mstakabali wa nchi yao,ila sisi huku tunaendekeza siasa zenye chuki na kelele nyingi na ubabe.
Na kama watanzania wakiendelea na mtindo huu,tutapa wakati mgumu sana na tujiandae kwa matokeo mabuvu zaidi katika nyanja zote,ikiwemo elimu.
 
Back
Top Bottom