Tumeendelea kucheka na nyani mabua tutaraji mabua

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
Nimeshtushwa na taaarifa niliyoiona ikihusiana na afisa mmoja wa soka nchini Ujerumani aliyehukumiwa kwenda jela miezi 42 kwa kosa la kukwepa kodi.

Ikumbukwe kuwa haya ndio mataifa yenye nguvu kabisa duniani kiuchumi, kwa namna ya kushangaza sana hapa kwetu Rais aliwasamehe wakwepa kodi na kuwapa siku saba.

Zaidi ya hayo hatuna sheria kali za kuwadhibiti wakwepa kodi, hapa kwetu watu huiba kodi wakiwa comfortable kabisa wakati kodi ndio pesa ya kuendeshea serikali.

Wajerumani ni miongoni mwa wafadhili wetu wakubwa wako serious na kodi Yao kiasi hicho sisi tunategemea uchawi gani kutuletea meandered?
 
Mkuu, unazungumzia kodi!!??
-Watu wanailiingizia taifa hasara kwa mikataba mibovu na bado wanadunda uraiani!
-Mtu kapokea nchi ikiwa na deni la Trilion 9 yeye kaacha nchi ikidaiwa Trilioni 48 na bado analipwa 80% ya mshahara wa rais wa sasa. Posho anapokea, marupurupu na kila kitu anabeba!
-Watu wa TRA/TPA wamekatwa na mamilioni ya pesa majumbani kwao, wanapelekwa mahakamani ila wanarudi kwa dhamana na wanakaa kwenye majumba waliyokaa kwa kuiibia serikali.
-Afsa wa TRA kagundulika ana nyumba 75, ameachishwa kazi ila yupo uraiani anatanua kwa pesa alizoiibia serikali.

HII NCHI KAMA SIO TUNA LAANA BASI SISI NI MAZEZETA WA KUTUPWA NA WANASIASA WANACHEZA NA AKILI ZETU KILA SIKU SISU TUKIBAKI TUKISEMA TUNAMUACHIA MUNGU!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom