Tumechoka kuonewa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumechoka kuonewa na Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Oct 10, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Sisi ni watanzania katika nchi huru
  Tumechoka kuonewa na polisi
  Tumechoka kubambikiwa kesi za uongo
  Tumechoka kupigwa ili kutuliza frustration za ugumu wa maisha ya askari
  Tumechoka kutozwa rushwa kwa kila jambo linalohitaji huduma ya polisi
  Tumechoka kusikia uongo wa polisi kila wanapokiuka haki zetu
  Tumechoka kuwa chanzo cha kitoweo cha askari wa usalama barabarani
  Tumechoka kuzika ndugu zetu na rafiki zetu wanaofia mikononi mwa polisi
  Tumechoka kuuguza majeraha yanayotokana na polisi
  Tumechoka kukataliwa haki yetu ya dhamana kwa ubinafsi wa polisi badala ya sheria
  Tumechoka polisi kutumiwa na matajiri wachache kutunyima haki zetu
  Tumechoka kuona polisi wakigeuzwa kuwa chombo cha ukatili cha wanasiasa
  Tumechoka kuona polisi wakijifanya miungu wadogo katika kushughulika na raia
  Tumechoka kuchukuliwa na polisi kama watu tusio na uwezo wa kufikiri
  Tumechoka kuona haki zetu za kiraia zikiwekwa mikononi mwa polisi pasipo utashi wetu

  Si unyonge wetu uliotufanya tukubali kuonewe na polisi muda wote huu, tuna nguvu ya wingi wetu
  Si ujinga wetu unaotufanya tudhalilishwe na polisi katika nchi yetu wenyewe, tuna uvumilivu
  Si umasikini wetu unaotufanya tuwavumilie polisi muda wote huu, tuna amani

  Lakini sasa tunasema basi inatosha
   
 2. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unayosema ni kweli. Mimi nilipata kuishi jirani na nyumba ya maiti pale Muhimbili miaka ya 80-90 nilikuwa nashanga sana kuona polisi wakileta maiti pale karibu usiku kucha.Nilikuwa najiuliza kama ni ajali mbona sizisikii katika radio na kusoma katika magazeti? Sasa nimeamini polisi wanaua watu wengi bila taarifa kuwa wazi.
  Haya mauaji ya Mwangosi yamedhihirisha haya, ushahidi wa picha halisi sio picha duka umeonyesha marehemu akiwa katikati ya polisi huku wakiwa wamekamata silaha na bado serikali inasema hawahusiki na kifo cha marehemu. Je ni watu wangapi wanafia mikononi mwa polisi bila kuwa na ushahidi angalau wa picha kama huu? na je kama wahusika wangekuwa kutoka chama tofauti na CCM wangesema hawahusiki na mauaji?
  Hali kama hii inajenga chuki katika jamii na ndio maana katika nchi zenye matukio ya ugaidi mambo yalianza hivi hivi. Tuepushe nchi yetu kuingia katika machafuko yasiyo na sababu.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,532
  Likes Received: 5,680
  Trophy Points: 280
  Jeshi lote la kuvunja liundwe upya!!!
   
 4. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  MTALIA MPAKA MTOE MACHOZI YA DAMU,dawa ya hawa polisi wetu ni kwa nguvu zote KULIBWAGA CCM mwaka 2015 na pia KUBADILISHA SHERIA KANDAMIZI!!
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  As long as jeshi la polisi wanaajili failures katika mitihani-div 4 and 0, then utendaji wapolisi hautabadilika. Ukiacha akina Kaqmuhanda ambao wanatafuta kuifurahisha CCM, with education naamini tunaweza kulibadilisha jeshi letu. lazima katiba itamke wazi kuhusu polisi na ukatili wao.
   
 6. Shixi889

  Shixi889 JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ina maana kua na mapolisi failures ndio sababu ya kuwa chombo chenye mamlaka ya kuonea mpaka kuua raia??sio kwamba muundo na uongozi wao kua mbaya na kufuata matakwa ya wakubwa wao??? sio kuwa na serikali yenye kutumia vyombo vya usalama kwa maslai yao binafsi??sio sheria mbovu zinazowakinga wao kama vyombo husika vya ulinzi??
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Yote hayo uliyoyasema yana mantiki kubwa, very true!. lakini mtu aliyeelimika, na sio mitulinga ya kwata, na songa mbele kuruta, anaweza aka-reason kuwa hili nisilifanye! Naamini aliyemuua mwangosi elimu yake ni duni, huwezi fanya hivyo kwa mtu ambaye uneshamdhibiti na ni mwandishi wahabari unamjua fika , hana silaha etc. Poor reasoning. Kumbambikia mtu kesi, sidhani kama university graduate polis anaweza fanya hivyo- I stand to be corrected, labda siwajui vizuri polis. Hawa wa chaspa mguu siwaamini hata! Moreover wengi wao bado ni darasa la saba!
   
 8. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hatuna jeshi la polisi! IGP ni shemeji wa dhaifu! jeshi halina nidhamu! wanababimbikia watu kesi,Jeshi linanuka rushwa! kuingia kituo cha polisi bure kutoka na hela.Jeshi la polisi ni tawi la magamba!
   
 9. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Wakuu mie nimeathiriwa na utendaji wa Polisi kiasi kwamba kweli nina chuki na askari yeyote ninaemuona. Nadhani Watanzania wengi wana hisia kama zangu. Sasa hii ni hatari sana, kwa watu ambao twapaswa kuwaona Polisi kama walinda amani na usalama.

  Juzi hapa kuna askari alinikamata na insurance iliyopita muda wake, maana nilikuwa nimejisahau, alinidai chochote nikamjibu wazi, kwamba ni heri aniandikie faini nikalipe isaidie mapato ya nchi hata kama ni mara kumi ya kiasi ambacho angetaka, kuliko kumpa yeye binafsi akatumie na familia yake! Nilisema hivi wazo la kwanza kichwani likiwa ni chuki yangu kwake binafsi kutokana na utendaji wa Polisi na si rushwa aliyotaka!

  Iringa wanasema uhusiano wa polisi na waandishi wa habari umeharibika. Mie nasema uhusano wa Polisi na raia wa Tanzania kwa ujumla umeharibika!
   
 10. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna askari waliombambikizia mama mjane kesi. Wakamptupa rumande bila kujali ukiwa alionao wa kufiwa na mumewe gafla aliyemwachia watoto saba akiwapo wa mwaka mmja na miezi. Mama huyo analilia rumande. Watoto wake wanasota bila baba wala mama. Mhusika wa kesi alitoa rushwa ya kutosha kwa polisi wakamwachia na kumchua huyu mjane maskini asiye na mtetezi na kumfungia badala ya yule mhusika.
  Je hawa polisi waliofanya hiki kitendo watasalimika? Kilio cha huyu mjane ambaye amesotea rumande sasa ni mwezi wa tatu kitaliacha hili taifa katika usalama? Kwa uhakika hana cha kufanya isipokuwa kulia na kusali. Ipo siku moja kilio chake kitayafikia masikio ya mwuumba wake. Huyo Mwuumba aafanya nini kwa hawa waliomtendea unyama kama huu masikini huyu? Tusumbiri tuone kwani maandiko yanasema nitakisikia kilio cha majane na yatima. Polisi jiangalieni sana hii rushwa imewapeleka mbali mno!
   
 11. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Haya, jana tu nimeweka hii thread, leo tunasikia Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza, Albert Buchafwe amenusurika kuuawa kwa risasi na Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Nyakato, Abubakar Zebo. Halafu kwa ujinga usio kifani kama vile watanzania wote ni mambumbumbu wa kudanganywa kirahisi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, bila hata kumhoji alieyetaka kuwawa, anasema ana uhakika ni bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiintelijensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na la ofisa huyo. (Na kwa jinsi magari yanavyofanana Tanzania kama polisi wanashambulia gari kwa kuwa tu linafanana na wanalotafuta basi wao ni polisi mbumbumbu kuliko wote duniani)

  Swali la msingi limeulizwa, tangu lini polisi wanatumia magari yao binafsi, kama Suzuki binafsi aliyokuwa nayo huyu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Nyakato, Abubakar Zebo, kwenda kuweka mitego ya kuwakamata majambazi?

  Buchafwe aliyetaka kuuwawa amesema wazi, kwamba huyu askari Abubakar Zebo ana uhusiano wa karibu na mkewe, ambaye wamekuwa na ugomvi naye pamoja na kesi ya kutalikiana mahakamani.

  Yaani tuna jeshi la Polisi limefikia hatua kutumia silaha za dola kwa ajili ya kuua wananchi hadi kwa ajili ya ngono!!! Sijawahi kusikia ufilauni wa kiasi hiki.
   
Loading...