nkulikwa
JF-Expert Member
- Jul 21, 2015
- 721
- 813
Baba wa Taifa aliweka umoja, amani na upendo kama Nguzo kuu za taifa, taratibu tumeanza kusahau kabisa nakudhani umoja, amani na upendo wa kila chama pekee ni muhimu kuliko Taifa, kufanya hivyo ni kupotea. Kama vyama vingi vingekuwa haramu kamwe asingeruhusu asilani; lakini baada ya kujaribu mfumo wa Chama kimoja aligundua umoja katika tofauti una nguvu kuliko umoja wa kimoja na mawazo ya kimoja akaona ni vema kabisa kuwa na vyama vingi na kusema ccm ivilee vyama hivi mpk vikomae kabisa! Kesho ni fumbo kwa binadamu. Ni muhimu kujenga umoja wa taifa na kuondoa Chuki ya kivyama,kidini na kikabila! Maana Leo uko Chama hiki kesho hujui utakuwa Chama gani? Leo Watu wana kusifu kwa hicho na hicho kikiondoka utakuwa wewe ni pekee na mpweke.