Tume ya warioba zanzibar


A

abdul 28

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2012
Messages
325
Points
0
A

abdul 28

JF-Expert Member
Joined May 29, 2012
325 0
[h=1]Kilichotokea kwenye kukusanya maoni Zanzibar kwa jicho la aliyeshuhudia[/h]Posted by khelef on Monday, December 10, 2012 · Leave a Comment


Hii ni simulizi ya Ahmed Omar, ambaye ni mfuatiliaji wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi kwa ajili ya katiba mpya na ambaye amekuwa mara kwa mara akitutumia takwimu za maoni hayo humu kwenye mitandao ya jamii. Ahmed alikuwepo kwenye maeneo ya matukio ya leo mjini Zanzibar na anaelezea alichokishuhudia na tafsiri yake kwacho. Zanzibar Daima inachapisha usimulizi wake kama taarifa kutoka kwa shahidi wa awali.
“Nikiwa mdau na mfuatiliaji wa zoezi zima nilifika kituoni saa 6.30 mchana wakiwa watu wachache wanawasili pole pole. Mara nilianza kuona makundi makubwa ya vijana na akina mama wakiwasili na kujipanga mbele katika jukwaa linalotegemewa kutumiwa kwa shughuli hio.

“Makundi hayo yaliongezeka hadi kufikia kiasi cha watu elfu moja hivi (1000). Muda wa kuwasili tume ylipokaribia kelele zilianza kusikika “nendeni mkatoe maoni huko huko kwenu Tomondo, Draja Bovu na Pemba, hapa Magomeni hapawahusu nyinyi” “watizame wamekuja kujijaza pale mbele kama vile ni jimbo lao, tunasema hapa hapatolewei maoni leo” Hizo zilikuwa ni kauli za wafuasi wa CCM wakilalamikia wingi wa wafuasi wa MKATABA waliowahi katika nafasi za mbele wakijikuta wao kuwachwa nyuma.“Mabishano yalianza kusikika baina ya wananchi, wana CCM wakidai wamevamiwa na watu wasiohusika katika eneo lao na wanamkataba wakidai sheria ya mabadiliko ya katiba haijaweka sharti mtu kutoa maoni katika eneo la shehia yake, na hivyo kitu muhimu ni mtu kutokutoa maoni mara mbili jambo ambalo ni sahihi.


“Ghafla tulimshuhudia mwakilishi wa jimbo hilo Salmin Awadh akiwasili huku akiwa makali sana akiunga mkono madai ya wana CCM wenzake kwamba waliowahi nafasi za mbele wote hawastahili kutoa maoni hapo na wanapaswa kuondoka au mchakato hautaendeshwa.“Tume baada ya kuwasili ilishuhudia hali hiyo ikiendelea na ndipo ilipoanza kulikabili suala hili. Salmin Awadh alimwita mjumbe wa tume Bi Fatma ambae ni mwana CCM na kumshawishi kuufuta mkutano huo wa kutoa maoni kwa madai yake. Bi Fatma aliyakubali madai hayo na ndipo alipomfuata mwenyekiti wa tume Profesa Baregu na kumpa ushauri huo wa kuufuta mkutano huo wa kutoa maoni.


“Mjumbe mwengine wa Tume Bwana Ali Saleh alishauri kuwa hakuna haja ya kuufuta mkutano huo kwa kuwa kila mwananchi anaweza kutoa maoni yake popote na kwa kuwa katika kituo hapakuwa na fujo bali ni mabishano ambayo yalihitaji ufafanuzi wa tume na mambo kuwekwa sawa.“Wajumbe wa tume walikutana pembeni kwa dakika kadhaa na kujadili nini kifanyike ndipo ghafla ilipotoka kauli ya mwenyekiti kwamba utowaji maoni katika kituo hicho umefutwa kutokana na kuhofiwa vurugu. Hapa tujiulize “kumbe vurugu ni kujitokeza mbele watu wenye maoni kinyume na CCM katika foleni ya kutoa maoni?’


“Hivi Bi Fatmaa ameambiwa na nani kama watanzania wanatoa maoni ya mabadiliko ya katuba katika shehia zao tu. Vituo na Shehia zimepangwa ili kuweza kuwafikia watu kirahisi na si vinginevyo. Unaweza kutoa maoni hata kwa kwenda ofisi za tume mwenyeo Dar es Salaam, kwa kuwatumia barua, kwa mitandao ya simu na internet nk. Hakuna kipengele kinachosema mtoa maoni awe eneo lake ndipo atoe maoni.

“Kwa nini leo tume imekubaliana na upotoshaji huu mkubwa wa mwana CCM, Salmin Awadh kwa malengo binafsi ya kisiasa? Mhe Kikwete iangalie vizuri tume yako ama jambo hli ulilolileta kwa nia njema wataliharibu na kumalizika kwa maafa makubwa. Hatukubali kuona baadhi ya vyama vya siasa hususan chama cha CCM kuwa na ushawishi kwa tume. Hala hala mjiti na macho.”
 

Forum statistics

Threads 1,284,370
Members 494,064
Posts 30,822,861
Top