Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA)

talentbrain

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,187
759
Habari wana taaluma wa Sheria.

Ninakuja na ombi langu kwenu la msaada wa mawazo ya kisheria juu ya adhma yangu ya kufungua shauri katika tume tajwa hapo juu. Ukweli ni kwamba mwajiri kaniachisha kazi kinyama bila kunipa stahili zangu.

Kwakuwa mimi ni layman katika sheria, na kwakuwa nimeshindwa kupata pesa za kuajiri mwanasheria anisaidie na kwakuwa sikuwa mwanachama wa vyama vya wafanyakazi japo hapo miaka kadhaa nilikuwa mwanachama wa TUICO. Nimedhamiria nijisimamie mwenyewe katika kufuatilia haki zangu.

Sasa wadau, naombeni malekezo ya kufuata katika kufungua shauri hili na ikiwezekana nitaomba ushauri wa kisheria ni mambo gani nayotakiwa kuyadai kulingana na circumstance yangu.

Sitaweza kueleza hapa ilivyokuwa, ila niko tayari kumueleza mwanasheria yeyote atayetaka kunisaidia kwa kunifuata PM. Nafanya hivi ili kuepusha mambo ambayo nadhani mnayaelewa.

Natanguliza shukurani.

NB: Kama kuna makosa ya kiuandishi niwieni radhi.
 
Back
Top Bottom