Tume ya uchaguzi yalalamikiwa na upinzani; CCM yaiunga mkono

H

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
263
Points
0
H

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
263 0
Na Exuper Kachenje

VYAMA vya siasa vya CUF na Chadema vimeelezea wasi wasi wao kuhusu uwezo wa kiutendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba havina imani nayo.

Hayo yalisemwa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika, walipokuwa wakizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano uliokutanisha NEC na vyama vyote vya siasa nchini.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilishana mawazo kuelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.

"Tuna matatizo na tume ya uchaguzi. Hatuna imani na tume, uwezo wake ni mdogo hasa kiufundi. Tuna masikitiko makubwa, NEC inatuangusha katika kuleta demokrasia," alisema Profesa Lipumba.

Alisema pamoja na mambo mengine, tume hiyo imeshindwa kutekeleza matakwa ya kidemokrasia kwa vyama vya siasa na wananchi na katika uendeshaji wa uchaguzi na daftari la kudumu la wapiga kura.

Lipumba alisema mara kadhaa NEC imeshindwa kutoa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa, ili kuhakiki wapiga kura kabla ya uchaguzi. jambo ambalo alisema linafifisha demokrasia.

Kwa upande wake, Mnyika wa Chadema alisema NEC imeonyesha udhaifu mkubwa katika utendaji wake na kwamba hilo linathibitishwa na namna ilivyoendesha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Alisema uchaguzi huo uligubikwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurudiwa kwa majina, jambo linaloonyesha kuwa tume hiyo ina udhaifu katika utendaji.

Alisema matatizo mengine ya NEC ni gharama kubwa za uendeshaji shughuli zake na kasi ndogo ya uandikishaji wapiga kura wapya.

Mnyika alibainisha kuwa NEC imekuwa ikitumia Sh10,000 kama gharama ya kuandikisha kila mpiga kura na kwamba imekwishaandikisha wapiga kura wapya 2.8 milioni.

Alisema hata hivyo ongezeko la idadi ya wapiga kura tangu mwaka 2005 ni kati ya watu milioni tano hadi nane.

Alisema Chadema kwa kutambua udhaifu uliopo katika NEC, imewasilisha mawazo yake kutaka mabadiliko ya kikatiba na sheria mbalimbali za uchaguzi zitakazosaidia kuwepo kwa tume huru na uchaguzi wa haki.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dar es Salaam, John Guninita alisema chama chake kina imani na NEC na kwamba jambo la msingi kwa vyama vya siasa,ni kufuata na kutekeleza sheria na taratibu za tume.

Source: Mwananchi

...........ndiyohiyo
 
Last edited by a moderator:
C

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Messages
1,330
Points
0
C

Chuma

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2006
1,330 0
Kaka NdiyoNdiyo Wewe Na Mwenzako Bubu Mnaboa mnapo kuta kila nukta ktk gazeti mnakuja kujaza thread hapa..na watu tunakosa mwelekeo wa kinachojadiliwa...ma-thread mengi kaka mchwa!!!
 
H

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
263
Points
0
H

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
263 0
Kaka NdiyoNdiyo Wewe Na Mwenzako Bubu Mnaboa mnapo kuta kila nukta ktk gazeti mnakuja kujaza thread hapa..na watu tunakosa mwelekeo wa kinachojadiliwa...ma-thread mengi kaka mchwa!!!
Kama wewe na mfuasi wa CUF au CHADEMA nimekuboa kwa kuleta habari ya CCM kuwapasha viongozi wako sina jinsi ya kukusaidia

.......ndiyohiyo
 
AljuniorTz

AljuniorTz

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2009
Messages
544
Points
195
AljuniorTz

AljuniorTz

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2009
544 195
Na Exuper Kachenje

VYAMA vya siasa vya CUF na Chadema vimeelezea wasi wasi wao kuhusu uwezo wa kiutendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba havina imani nayo.

Hayo yalisemwa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika, walipokuwa wakizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano uliokutanisha NEC na vyama vyote vya siasa nchini.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilishana mawazo kuelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.

"Tuna matatizo na tume ya uchaguzi. Hatuna imani na tume, uwezo wake ni mdogo hasa kiufundi. Tuna masikitiko makubwa, NEC inatuangusha katika kuleta demokrasia," alisema Profesa Lipumba.

Alisema pamoja na mambo mengine, tume hiyo imeshindwa kutekeleza matakwa ya kidemokrasia kwa vyama vya siasa na wananchi na katika uendeshaji wa uchaguzi na daftari la kudumu la wapiga kura.

Lipumba alisema mara kadhaa NEC imeshindwa kutoa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa, ili kuhakiki wapiga kura kabla ya uchaguzi. jambo ambalo alisema linafifisha demokrasia.

Kwa upande wake, Mnyika wa Chadema alisema NEC imeonyesha udhaifu mkubwa katika utendaji wake na kwamba hilo linathibitishwa na namna ilivyoendesha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Alisema uchaguzi huo uligubikwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurudiwa kwa majina, jambo linaloonyesha kuwa tume hiyo ina udhaifu katika utendaji.

Alisema matatizo mengine ya NEC ni gharama kubwa za uendeshaji shughuli zake na kasi ndogo ya uandikishaji wapiga kura wapya.

Mnyika alibainisha kuwa NEC imekuwa ikitumia Sh10,000 kama gharama ya kuandikisha kila mpiga kura na kwamba imekwishaandikisha wapiga kura wapya 2.8 milioni.

Alisema hata hivyo ongezeko la idadi ya wapiga kura tangu mwaka 2005 ni kati ya watu milioni tano hadi nane.

Alisema Chadema kwa kutambua udhaifu uliopo katika NEC, imewasilisha mawazo yake kutaka mabadiliko ya kikatiba na sheria mbalimbali za uchaguzi zitakazosaidia kuwepo kwa tume huru na uchaguzi wa haki.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dar es Salaam, John Guninita alisema chama chake kina imani na NEC na kwamba jambo la msingi kwa vyama vya siasa,ni kufuata na kutekeleza sheria na taratibu za tume.

Source: Mwananchi

...........ndiyohiyo
Ni bora heading yako ungeandika CUF na CHADEMA Waipasha NEC; ingeleta maana ziadi.
Sehemu kubwa ya stori ni weakness wanazoziona wapinzani kwa tume ya uchaguzi na baadhi wamezitaja ktk kikao hicho.

Hicho kipengele cha mwisho, hayo ni maoni ya Guninita kwa Wapinzani dhidi ya tume. Hiyo mipasho iko wapi???
 
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
2,776
Points
1,195
R

Rwabugiri

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
2,776 1,195
Kama wewe na mfuasi wa CUF au CHADEMA nimekuboa kwa kuleta habari ya CCM kuwapasha viongozi wako sina jinsi ya kukusaidia

.......ndiyohiyo
Ndugu Habarindiyo hiyo,
Naona unajichanganya, ukisoma habari mbona haionyeshi hiyo mipasho? sana sana cuf na chadema wameisanura NEC ilivyo hovyo.. sasa hizo pumba za Guninita kwamba yeye ana imani, ili hali mapungufu yamewekwa wazi we unaona ni sawa?

No wonder ushabiki upofu wa namna hii umetufikisha hapa tulipo! Haihitaji masters kuelewa kwamba Guninita alicho ongea ni blah blah.. zilizo tufikisha hapa tulipo!
 
M

Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Messages
1,287
Points
0
M

Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2008
1,287 0
Sexed story ndio hii na hata mwandishi hajui anaanidika nini; otherwise be wise to present sio unajaza ugoro usioeleweka hapa; Chadema an CUF ndio waliipasha NEC na CCM ikatoa maoni yake dhidi ya vyama hivyo; du shule zetu pia zinatofautiana sana na hapa ni wazi udhaifu wa mtu huonekana
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,402
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,402 0
Nyie hamjui? Habrindiyohiyo ni mmoja wa wale ma-agent wa mafisadi wanaopenyeza thread humu za kuwatetea na kuviponda vyama vya upinzani vinavyowaumbua kwa ufisadi wao -- kwa malipo of course. Hapa namtoa Bubu kwani yeye anaonekana ni mpiganaji wa dhati.

Kusema kweli hiyo thread haina maana yoyote na ningewashauri wana JF wenzangu, wale serious -- wazipuuze hizo thread, wasizicomment kabisa.
 
Mwiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
7,613
Points
1,250
Mwiba

Mwiba

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
7,613 1,250
Hivi vyama vya upinzani navyo vimejaa ujinga ,sasa si wakati wa kupatana na NEC ya uchaguzi ,huu ni wakati wa kuipinga moja kwa moja bila kusita au kurudi nyuma ni kuikataa kwa maana ya kuikataa kwa vitendo na kuutangaza uovu wake hadharani ,sasa mnatoa mapendekezo ili iweje ? Wayakubali ,wayapitie wayaongeze ,maana mnaposema mapendekezo wana hiari yao kuyafuata au kuyakataa na kwa wachovu wa Sultani CCM solution yao ni kulinda Chama Cha CCM kwa hali yeyote na kwa vile mliotoa ni mapendekezo watasema tu wakati hautoshi tumebakiza mwaka mmoja na gharama za kufanya marekebisho ni kubwa hivyo kutokana na hali ya uchumi duniani wafadhili hawatokuwa na uwezo wa kutusaidia ,very simple answer na watakuwa wamefunga kazi.

Jamani kunatakikana nguvu za ziada katika kukabiliana na Tume hii ya Uchaguzi si kwa kupelekewa mapendekezo ni kufanyika ulazimisho wa lazima kuwa Tume ibadilishwe na ibadilike kusiwe na mjadala wa kubembelezana .hilo ni kosa na kutoa mwanya kwa Sultani CCM kutumia nyenzo zake ambazo ni hao waliomo kwenye Tume.

Upinzani ni lazima utangaze kwa nia safi kabisa kuwa hawana imani na Tume ya Uchaguzi na WaTanzania wote wasikie na kuungwe mkono kwa maandamano ya Nchi nzima ,ili kuutambulisha ulimwengu kuwa WaTanzania wanaikataa Tume ya Uchaguzi inayoundwa na wanachama wa Chama kimoja (Aidha waliotokana katika mfumo na kuwemo kwenye Chama kimoja cha CCM ) Hivyo hawakubaliki ni lazima Tume ishirikishe wadau wote kwa kiwango sawa katika wajumbe wanaowakilisha.

Ila kwa Tume hii watatoa ushindi wa kupanga kwa vyama vya upinzani kama Uchaguzi mkuu ulioipita.
 
Forum statistics

Threads 1,284,203
Members 493,978
Posts 30,817,141
Top