Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 13
Na Exuper Kachenje
VYAMA vya siasa vya CUF na Chadema vimeelezea wasi wasi wao kuhusu uwezo wa kiutendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwamba havina imani nayo.
Hayo yalisemwa juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika, walipokuwa wakizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano uliokutanisha NEC na vyama vyote vya siasa nchini.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubadilishana mawazo kuelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
"Tuna matatizo na tume ya uchaguzi. Hatuna imani na tume, uwezo wake ni mdogo hasa kiufundi. Tuna masikitiko makubwa, NEC inatuangusha katika kuleta demokrasia," alisema Profesa Lipumba.
Alisema pamoja na mambo mengine, tume hiyo imeshindwa kutekeleza matakwa ya kidemokrasia kwa vyama vya siasa na wananchi na katika uendeshaji wa uchaguzi na daftari la kudumu la wapiga kura.
Lipumba alisema mara kadhaa NEC imeshindwa kutoa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vyama vya siasa, ili kuhakiki wapiga kura kabla ya uchaguzi. jambo ambalo alisema linafifisha demokrasia.
Kwa upande wake, Mnyika wa Chadema alisema NEC imeonyesha udhaifu mkubwa katika utendaji wake na kwamba hilo linathibitishwa na namna ilivyoendesha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Alisema uchaguzi huo uligubikwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurudiwa kwa majina, jambo linaloonyesha kuwa tume hiyo ina udhaifu katika utendaji.
Alisema matatizo mengine ya NEC ni gharama kubwa za uendeshaji shughuli zake na kasi ndogo ya uandikishaji wapiga kura wapya.
Mnyika alibainisha kuwa NEC imekuwa ikitumia Sh10,000 kama gharama ya kuandikisha kila mpiga kura na kwamba imekwishaandikisha wapiga kura wapya 2.8 milioni.
Alisema hata hivyo ongezeko la idadi ya wapiga kura tangu mwaka 2005 ni kati ya watu milioni tano hadi nane.
Alisema Chadema kwa kutambua udhaifu uliopo katika NEC, imewasilisha mawazo yake kutaka mabadiliko ya kikatiba na sheria mbalimbali za uchaguzi zitakazosaidia kuwepo kwa tume huru na uchaguzi wa haki.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dar es Salaam, John Guninita alisema chama chake kina imani na NEC na kwamba jambo la msingi kwa vyama vya siasa,ni kufuata na kutekeleza sheria na taratibu za tume.
Source: Mwananchi
...........ndiyohiyo

Last edited by a moderator: