PreGE2025 Tume ya Uchaguzi yafafanua wanaojiandikisha zaidi ya mara moja mkoa wa Dar

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nguruka

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Posts
200
Reaction score
131
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi amefafania madai ya uwepo wa wawtu mkoani Dar es Salaam wanaojiandikisha zaidi ya mara moja.

Ndg. Ramadhani Kailima amebainisha nini Tume hufanya baada ya Uboreshaji kukamilika na mwisho wa siku Daftari liliso na watu waliojirudia kutoka kwaajili ya Uchaguzi Mkuu.

1.jpg
2.jpg
 
Attachments

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiendelea kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura mkoani Dar es Salaam, imesema kumejitokeza changamoto ya baadhi ya watu kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti.

IMG_3613.jpeg

INEC imesema hayo leo Machi 20, 2025 katika taarifa kwa umma kuhusu uandikishaji wapigakura mkoani Dar es Salaam, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima.

Amesema baada ya uandikishaji kukamilika katika vituo, Tume huchakata taarifa za watu wote walioandikishwa kupitia mfumo maalumu (Automatic Fingerprint Identification System-AFIS), ambao una uwezo wa kuwabaini wapigakura wote waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

Soma, Pia: Tume ya Uchaguzi: Wapigakura milioni 34.7 wanatarajiwa kushiriki Uchaguzi mkuu Oktoba

Kailima amesema Tume pia hufanya kazi ya kulinganisha sura za watu wote waliopo kwenda daftari lengo likiwa kubaini iwapo kuna waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

Amesema iwapo itabainika mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja jina na taarifa za mtu huyo, hufutwa na mfumo katika vituo vingine na kubakizwa katika kituo cha mwisho alichojiandikisha katika daftari, hivyo, taarifa nyingine zote za awali hufutwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi amefafania madai ya uwepo wa wawtu mkoani Dar es Salaam wanaojiandikisha zaidi ya mara moja.

Ndg. Ramadhani Kailima amebainisha nini Tume hufanya baada ya Uboreshaji kukamilika na mwisho wa siku Daftari liliso na watu waliojirudia kutoka kwaajili ya Uchaguzi Mkuu.

View attachment 3277369View attachment 3277370
Kabla ya kutoa taarifa hii amekubaliana na CCM au?????
 
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiendelea kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura mkoani Dar es Salaam, imesema kumejitokeza changamoto ya baadhi ya watu kujiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti.

View attachment 3277465
INEC imesema hayo leo Machi 20, 2025 katika taarifa kwa umma kuhusu uandikishaji wapigakura mkoani Dar es Salaam, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima.

Amesema baada ya uandikishaji kukamilika katika vituo, Tume huchakata taarifa za watu wote walioandikishwa kupitia mfumo maalumu (Automatic Fingerprint Identification System-AFIS), ambao una uwezo wa kuwabaini wapigakura wote waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

Soma, Pia: Tume ya Uchaguzi: Wapigakura milioni 34.7 wanatarajiwa kushiriki Uchaguzi mkuu Oktoba

Kailima amesema Tume pia hufanya kazi ya kulinganisha sura za watu wote waliopo kwenda daftari lengo likiwa kubaini iwapo kuna waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

Amesema iwapo itabainika mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja jina na taarifa za mtu huyo, hufutwa na mfumo katika vituo vingine na kubakizwa katika kituo cha mwisho alichojiandikisha katika daftari, hivyo, taarifa nyingine zote za awali hufutwa.

Chanzo: Mwananchi
Kwa nini mfumo usitambua double registration mda huo huo mtu anapojiandikisha. This is Tanzania ujinga mwingi
 
Kwamba hiyo tume ina umakini huo wa kuweza kutoa duplicate names? Hawana uwezo huo, na kinachofanyika wanakifahamu.
 
Back
Top Bottom