Tume ya "Uchaguzi" yaendelea kuchapa usingizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya "Uchaguzi" yaendelea kuchapa usingizi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ujengelele, Oct 3, 2010.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mawaziri wakiuka sheria ya maadili ya uchaguzi Saturday, 02 October 2010 07:34
  Salim Said
  MAWAZIRI na watendaji wakuu wa serikali wanaongoza kwa kukiuka Sheria ya Gharama za Uchaguzi na Maadili ya mwaka 2010 katika kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini, Mwananchi imebaini.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati; Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrance Masha na naibu wake, Balozi Khamis Kagasheki na Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wassira wamekiuka sheria hizo kwa kutangaza ahadi, misaada na miradi ya serikali.

  Kifungu cha 3.3 cha Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2010 kinaeleza kuwa watendaji wa serikali hawaruhusiwi kutangaza ahadi yoyote ya serikali, kutoa misaada au kutangaza miradi mpaka kumalizika kwa kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

  Kifungu hicho kinasomeka"Kuanzia kipindi cha kampeni mpaka kutangazwa kwa matokeo, mawaziri, watendaji na mamlaka nyingine za serikali hazitakiwi “(i) kutangaza katika vyombo vya habari au kwa namna yoyote misaada au ahadi ya aina yoyote na (ii) kutoa ahadi za shughuli za maendeleo ya jamii kwa mfano kujenga barabara, kusambaza maji au mambo mengine kama hayo.”

  Kwa mujibu wa sheria za Gharama za Uchaguzi na Maadili ya Uchaguzi za mwaka 2010, mawaziri hawa hawapaswi kutoa matamko yoyote katika kipindi hiki kutokana na ukweli kwamba wapinzani wao kwenye kinyang'anyiro cha ubunge hawana uwezo huo wa kuzungumzia mikakati ya serikali na hivyo kufanya hivyo kunawapa nguvu ya ziada kwenye kampeni zao dhidi ya wenzao.

  Lakini katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu hivi tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 20 mwaka huu, baadhi ya mawaziri, watendaji na mamlaka mbalimbali za serikali zimeonekana kupuuza waziwazi maadili hayo yaliyosainiwa na serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na vyama vyote vya siasa.

  Baadhi ya mawaziri hao ni Ngeleja, Chiligati, Mkulo na Waziri, Masha na Kagasheki pamoja na Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wassira ambao walitoa matamko mbalimbali kuhusu mipango ya serikali katika shughuli tofauti.

  September 17, 2010 mwaka huu, Waziri Wassira, ambaye anawania ubunge wa Jimbo la Bunda, alitangaza kwamba serikali imetenga Sh23.8 bilioni kwa ajili ya kununua tani 200,000 za mahindi yaliyolundikana kwa wakulima baada ya kukosekana kwa fedha za kununulia.

  Wassira alisema Rais Jakaya Kikwete ameagiza tani 400,000 za mahindi zinunuliwe ikiwa ni lengo la serikali katika kuyahifadhi mahindi hayo ambayo uzalishaji wake umeongezeka katika kipindi cha mwaka.

  “Serikali imeshatoa fedha hizo ili kuweza kununua tani hizo katika kipindi cha msimu huu,” alisema Waziri Wasira.

  “Tayari serikali imeshanunua tani 52,000 za mahindi katika kipindi cha msimu huu hivyo ifikapo mwisho wa mwezi huu jumla ya tani 105,000 za mahindi zitakuwa zimeshanunuliwa na serikali.”
  Waziri Wassira alisema hifadhi ya taifa hivi sasa ya ina tani 52,000 za mahindi zilizonunuliwa msimu huu na nyingine tani 47,000 za mahindi za awali. Hata hivyo alisema uwezo wake wa kuhifadhi ni tani 240,000.

  Waziri mwingine ni Chiligati ambaye alitoa miezi sita kwa idara inayoshughulikia utoaji wa hati za vijiji kuhakikisha vijiji vyote vilivyopimwa na kutokuwa na migogoro ya mipaka, vinapatiwa hati zao.

  Pia aliahidi kwamba kwa vijiji vyenye migogoro ya mipaka, wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) na Halmashauri husika watamaliza migogoro hiyo kadiri iwezekanavyo ili vipatiwe hati.

  Ngeleja, ambaye wizara yake inahusika na madini na nidhati, aliahidi Septemba 20 mwaka huu kuwa utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ya Kiwira, mkoani Mbeya utaanza karibuni baada ya serikali kupata Sh500 bilioni kutoka Serikali ya Watu wa China.

  “Mradi wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe uko katika mchakato wa kufufuliwa baada ya kurejeshwa serikalini. Tayari tumeshapata fedha kutoka China ambazo zitagharamia mradi huo,” alisema Ngeleja.

  Mbali ya taarifa hiyo, Septemba 17 mwaka huu Waziri Ngeleja alisema serikali inakusudia kuongeza uwezo katika uzalishaji wa umeme unaotumia nguvu za maji, ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa huduma za umeme nchini.

  Ngeleja aliyasema hayo alipokuwa akifungua kongamano la 22 la Afrika kuhusu ufuaji wa umeme wa maji.

  Akitumia wadhifa wake wa unaibu waziri, Khamis Kagasheki aliwataka wazazi kuwekeza zaidi katika elimu ya watoto Septemba 13 mwaka huu.

  Naye Waziri Masha naye Septemba mwaka huu alithibitisha uraia wa aliyekuwa mgombea ubunge wa Nzega mkoani Tabora kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe.

  Waziri wa Fedha na Uchumi Mkulo Septemba 4 mwaka huu alisema sekta ya mawasiliano nchini imekuwa kwa kiwango cha asilimia 20.5 mwaka 2009 tofauti na asilimia 20.4 mwaka 2007.
   
 2. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,954
  Likes Received: 1,770
  Trophy Points: 280
  kwani sheria ya uchaguzi si inasemekana imewekwa kwa vyama vya upinzani tu....we huoni hata kiongozi wao mkuu aliyeisaina ndio alikuwa kuivunja...lakini pia swala la umakini kwa ccm ni dogo na unaweza kuta hawajui kilichoandikwa mule ama hawajakielewawa..ndio maana hata midahalo wameshindwa ku attend..maana hawajui walichofanya katika vipindi vyao....
   
Loading...