PreGE2025 Tume ya Uchaguzi: Vyama 18 kati ya 19 vyasaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Visivyosaini havitaruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu

PreGE2025 Tume ya Uchaguzi: Vyama 18 kati ya 19 vyasaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Visivyosaini havitaruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Dodoma: Zoezi la Utiaji Saini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi Aprili 12, 2025


Vyama 18 vya Siasa Vyasaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi 2025

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima, amesema kuwa jumla ya vyama 18 vya siasa vimeridhia na kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa mwaka 2025.

Vyama vilivyosaini kanuni hizo ni:
  1. AAFP
  2. ACT-Wazalendo
  3. ADA-TADEA
  4. ADC
  5. CCK
  6. CCM
  7. CHAUMA
  8. CUF
  9. MAKINI
  10. DP
  11. NCCR-Mageuzi
  12. NLD
  13. NRA
  14. SAU
  15. TLP
  16. UDP
  17. UMD
  18. UPDP


Vyama ambavyo havijasaini havitashiri uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, ametangaza kuwa vyama vya siasa ambavyo havitasaini au vitakataa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi havitaruhusiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika Jumamosi, Aprili 12, 2025 jijini Dodoma, ambacho kilihusisha utiaji saini wa kanuni hizo, Jaji Mwambegele alieleza kuwa kifungu cha 162(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2024 kimeweka sharti la lazima kwa kila chama na mgombea kusaini na kutekeleza kanuni za maadili kabla ya kuwasilisha fomu za uteuzi.

“Kabla ya mgombea yeyote au chama chochote kuwasilisha fomu za uteuzi, ni lazima wawe wamesaini kanuni za maadili ya uchaguzi, pamoja na kuonyesha dhamira ya kuzifuata katika kipindi chote cha kampeni na mchakato mzima wa uchaguzi,” alibainisha Jaji Mwambegele.

Ameeleza kuwa hatua ya kusaini kanuni hizo si ya hiari bali ni hitaji la kisheria linalolenga kuhakikisha kuwa kila mdau wa uchaguzi anazingatia misingi ya maadili, kwa ajili ya kuendesha kampeni na uchaguzi kwa njia ya haki, amani na usawa.

“Lengo kuu ni kuthibitisha kwa pamoja kuwa vyama vyote na wagombea wapo tayari kuendesha uchaguzi kwa kuzingatia maadili, taratibu na sheria zilizowekwa,” aliongeza.

Kikao hicho ni sehemu ya mchakato wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, ambapo vyama vya siasa vilialikwa kushiriki katika tukio hilo muhimu mbele ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kama ishara ya mshikamano na uwajibikaji katika kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
 
HAkuna yeyote mwenye akili timamu, mwenye dhamira njema na Taifa lake, mkweli wa nafsi, kauli na vitendo, anayweza kwenda kusaini huo ushetani.

Kitakuwa ni kikao cha waovu kuidhinisha ushetani.

Ni sawa uitwe na jambazi sugu kwenda kusaini taratibu za kujenga jamii yenye maadili.
 
Dodoma: Zoezi la Utiaji Saini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi Aprili 12, 2025


huyo muhuni mwenye kofia mkononi ndiye aliyewaita kuweka saini ya maadili dodoma ni uhuni wa kishamba
Screenshot_20250412_101734.jpg
 
Katika mtazamo wa Siasa za Dunia na demokrasia , hii ni failure kubwa Sana kwa taifa . Vyama vya upinzani si majengo ,si ule usajili wa chama . Hii ni Imani kubwa waliyo nayo watu wengi.

Sasa kama hutaweza kwenda na watu wa aina hii basi hili ni anguko la ccm na serikali yake.

Aidha naweza kusema huu ndiyo uasi mkubwa kuliko wote . Utaona watu wapo kimya kumbe wamekwisha kuasi. Chadema itaanguka anguko la imani yaani wanaanguka wakiwa na nguvu ya kuinuka.

CCM inatamani kwenda mbele na chadema . Lakini mbele huko hakujulikani na hawana uhakika. Most of the time wanatenda wasiyoyapenda na kupenda wasiyoyatenda . Ccm wakijidanganya kuwa uimara wao unajengwa na wao walivyo Hilo ni kosa . Huwezi ukawa tajiri katikati ya maskini na ukawachukia maskini . Watakuondoa tu na kuhamia porini na Mali zako watachukua
 
Hahahaahhaha

Aisee kweli Mungu yupo kazini. Hili tukio waliliandaa kama igizo ila kwa namna walivyoliigiza inaonekana kabisa kuwa wanaigiza.

Eti ufafanuzi utatolewa kwa maandishi watu wasaini kwanza.🤣🤣🤣

Yaaani watu wasipewe ufafanuzi alafu wanaambiwq wasaini🤣🤣🤣

Hii nchi ina upumbavu wa kiwango cha kusikitisha.

Hongereni Chadema kujitenga na huu ushetani.
 
Back
Top Bottom