Tume ya uchaguzi sasa ni kisima cha kuzalisha viongozi mafisadi!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174
NEC sijui watajitetea vipi baada ya kuhalalisha wizi wa kura za marudio ya madiwani.

Yaliyotokea hayajawahi kutokea na huyu Jaji wao siyo mwadilifu kwani angeliyatengua matokeo yote ambayo polisi walitumika kuwaondoa mawakala wa upinzani kwenye vituo vya kuhesabia kura na pale ambao idadi za kura zimezidi idadi ya waliopiga kura.

Dhana ya majaji kuongoza tume za uchaguzi na Msajili wa vyama vya siasa sasa imedhihirika ni potovu.

Ujaji siyo sifa ya uadilifu hata chembe. Mbali ya ukweli kuwa ni kichocheo cha migongano ya mihimili ya dola hususani Mahakama na Utendaji na kuleta misuguano ya kikatiba.

Viongozi wanaopatikana kwa wizi wa kura ni mafisadi tu na waliowawezesha kama ni polisi, wateule wa Rais na NEC nao lao moya kabisa.

Viongozi wanaopatikana kwa wizi wa kura kamwe hawawezi kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi bali kuendeleza ufisadi.

Nionavyo, NEC sasa kwa muundo wake na kiutendaji ni kisima cha kuzalisha na kuwalea mafisadi.

Mashinikizo ya kutimuliwa makamishina wote wa NEC yabidi yaanze sasa yakiwemo marekebisho ya sheria za uchaguzi kuondoa uwakala wa serikali za mitaa kusimamia chaguzi zetu ambako hugeuka kichinjio dhidi ya haki za kikatiba za wapigakura kujichagulia viongozi wao wenyewe .

NEC lazima iwe na uwakilishi wa vyama vyote vya siasa kulingana na uwiano wa wabunge wao Bungeni na ikome kuwa mtumwa wa CCM.
 
Back
Top Bottom