Joel kaigarula
Member
- Jun 3, 2014
- 28
- 16
Tuanze na nukuu ifuatayo ya mwezi februari mwaka jana (2013):
Kama sehemu ya kuimarisha utendaji kazi, mamlaka hiyo ya vitambulisho vya taifa imeanzisha ushirikiano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ambayo inakusudia kuvitumia vitambulisho hivyo katika uchaguzi mkuu ujao. Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu alisema ushirikiano huo itasaidia kuboresha kazi za utoaji vitambulisho na kwamba utakamilika kwa wakati. Hata hivyo alisema bado ofisi yake inakabiliwa na tatizo la vitendea kazi na kuiomba serikali kuongeza bajeti. chanzo: Mwananchi
Leo hii hali ni hivi:
It was therefore a shock to Nida officials that NEC went ahead and advertised for the BVR tender in contravention of the agreement that Nida would provide the hi-tech registration for use by all the other State organs.
In the Bagamoyo meeting, it was agreed that NEC should use the Nida cards in the coming elections it was also agreed that the government should meet the full budgetary requirements as presented by Nida so that the voter registration deadline is met, the source explained.Chanzo: The citizen
Tutarudi katika hizo siasa baadae, ila kwa sasa maoni yangu:
Ingawa tume ya uchaguzi(NEC) ina wajibu wa kurekebisha daftari la wapiga kura, ilitakiwa watumie vitambulisho vile vile vya zamani badala ya vipya, kwani eventually kitambulisho cha mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) chenye taarifa za kibiometriki (sahihi, alama za vidole etc) kingeweza kuwa kitambulisho cha mpiga kura, na kuwa mbadala wa hivi tulivyonavyo sasa hivi. Hakukuwa na haja kwa tume kuanzisha vitambulisho vya biometriki wakati tayari NIDA inavitengeneza. Matumizi ya vitambulisho vya taifa kupiga kura sio jambo la ajabu au geni, tayari baadhi ya nchi America kusini zinatumia vitambulisho vya utaifa kwa shughuli hiyo.
Kutoka tovuti ya NIDA lengo mojawapo la kitambulisho cha taifa ni:
Kusaidia kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura nchini
Kikatiba, mtu anayestahili kupiga kura anatakiwa kuwa na sifa ya uraia wa Tanzania na pia awe umri wa miaka 18 na zaidi.Mchakato wa NIDA utakapokamilika tutakuwa na taarifa za raia wote wa Tanzania. Hivyo kupata daftari la wapiga kura itahitaji ku-query database ya NIDA tukitumia vigezo hivyo (raia? + Miaka 18 na zaidi?) na papo hapo tutapata orodha ya watanzania wote ambao wako eligible to vote (i.e daftari la wapiga kura kama tunavyolifahamu sasa ). Orodha hii sasa ndio ambayo NEC wangekuwa wana-access kupitia mtandao pale wanapofanya uhakiki wa vitambulisho kwa kuscan. Hivyo mpiga kura halali angeweza kujiandikisha popote alipo kwa wakati wa uchaguzi, tofauti na mfumo wa sasa wa madaftari unaolazimisha mpiga kura ajiandikishe katika makazi yake ya kudumu. Kinadharia: unakwenda na kitambulisho chako kituoni, kinakuwa scanned, kama upo kwenye list ( ile result ya query) namba yako inarekodiwa hapo kituoni na uko tayari kupiga kura.
Vile vile kwa vile zoezi la usajili wa vitambulisho vya taifa la NIDA ni endelevu, na wana vituo nchi nzima, daftari litaboreshwa kila siku raia anapojisajili au anapovuka miaka 18, halitabanwa na huu utaratibu wa sasa wa kuboresha mara mbili kila baada ya miaka 5 kupitia NEC. Hivyo wakati wa uchaguzi daftari toka NIDA ndilo litakuwa sahihi zaidi (up-to-date) kuliko hili la NEC.
Faida ya vitambulisho vya NIDA ni nini ikiwa tume ya uchaguzi inahitaji tena kuendesha zoezi lile lile la usajili wa biometriki: kuchukua alama za vidole, picha na saini? Kwa nini tusiendelee na vitambulisho hivi vya sasa vya kura, wakati tunasubiri vya taifa, ili kuondoa gharama ya kuanzisha vitambulisho vipya vya mabilioni ambao utadumu muda mfupi? Vitambulisho vya kura havitumiki sehemu nyingine yoyote zaidi ya uchaguzi. Lazima huko mbeleni, watatokea viongozi wasikivu watakaoliona hili na wataunganisha mifumo hii kama ilivyopangwa na kitambulisho cha NEC kitakuwa hakitumiki tena na hivyo tutakuwa tumepoteza bilioni 293 bila sababu.
Turudi kwenye zile siasa pale mwanzo:
1. NIDA na NEC walishakubaliana hapo mwanzo kuwa na mfumo mmoja, na lengo mojawapo la kuanzisha vitambulisho vya taifa ni kuisadia NEC katika suala la uandikishaji wapiga kura. kimetokea nini hapa kati kati mpaka NEC leo hii wawe na ulazima wa kuanzisha vitambulisho vyao vya biometric parallel na vile vya NIDA, badala ya kuendelea na vile vya zamani kusubiri vya NIDA ambavyo vitakuwa na facilities zile zile wanazozipigia chapuo sasa hivi (fingerprints, etc). Ulazima wa kurekebisha daftari la wapiga kura upo kwani ni matakwa ya kisheria, lakini ulazima wa kutumia vitambulisho vya biometric wakati huu mimi siuoni.
2. Iko hoja kuwa zoezi la NIDA linakwenda taratibu sana na hivyo kuna hofu kwamba vitambulisho havitakuwa tayari kabla ya uchaguzi. Hoja hii inaleta swali lifuatalo: NIDA tayari wameanza mchakato wao na baadhi ya mikoa tayari wameshamaliza kuchukua taarifa. NEC hawajaanza. Inakuwaje NEC wawe na uhakika wa kumaliza zoezi hilo hilo kabla ya NIDA? Huo ufanisi wa ajabu kwanini NIDA hawana? NEC wanatoa wapi bilioni 293 fasta wakati NIDA tunaambiwa hawana fedha za kutosha?
3. Mradi wa NIDA unaendeshwa na kampuni ya Iris corporation ambayo ilishinda tenda. Tume ya uchaguzi NEC ilipotangaza tenda yake kampuni hii hii ilishiriki lakini NEC waliikataa wakachagua nyingine. Kampuni hii ikashitaki na mamlaka ikaamua tenda irudiwe. Badala ya NEC kurudia tenda, NEC ikaamua kufanya utaratibu wa single-sourcing (kuteua moja kwa moja bila tenda) na kuamua kuiteua kampuni ya Litho Tech Exports toka Canada. Katika ile tenda iliyofutwa na mamlaka ya tenda kutokana na kesi, Litho tech ilitoa quotation ya dola milioni 84, katika hii single-sourcing ambapo iliteuliwa peke yake bila ushindani quotation sasa ni dola mil 117. Tofauti ya dola mil 33.
Mfano mzuri: Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) wameshirikiana na NIDA kuandaa vitambulisho vyao vipya kwa ajili ya wanachama wake.
"MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umepata kibali cha kutumia alama za vidole zilizotumika katika kutengeneza vitambulisho vya taifa kuokoa fedha ambazo zingetumika katika mchakato huo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanul Humba katika kongamano la nane la waandishi wa habari linalofanyika mkoani Mtwara.
Tumekamilisha mchakato wa kutoa vitambulisho vipya kwa wanachama wetu lakini tunawashukuru wenzetu wa NIDA wamekubali tutumie zile alama za vidole ambazo wao walishazikusanya katika ule mchakato wa kutengeneza vitambulisho vya taifa."
Chanzo: Bima ya afya yakamilisha vitambulisho vipya - Mwanzo
Ushirikiano kama huu umeshindikana vipi kati ya NEC na NIDA na kulazimu kutumia bil zaidi ya 200?
Habari hii imetoka: Bofyatz.com:: Tanzanian tech blog.