Tume ya Uchaguzi kitanzini Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Uchaguzi kitanzini Igunga

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nngu007, Oct 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 12 October 2011

  [​IMG][​IMG]

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaweza "kutiwa kitanzini" iwapo itathibitika kuwa ilichakachua daftari la wapigakura katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Igunga, MwanaHALISI limeelezwa.

  Taarifa kutoka ndani ya serikali, NEC na mashirika huru ya uangalizi wa uchaguzi nchini, zinaonyesha kwamba idadi ya wapigakura waliomo ndani ya daftari la wapigakura la mwaka 2010 na wale waliotajwa katika uchaguzi mdogo wa Igunga, inapishana tena kwa mbali.

  Gazeti hili lilimtafuta mkurugenzi wa uchaguzi, Rajavu Kiravu kuzungumzia suala hili, lakini alielekeza mwandishi kuwasiliana na Rajabu Kiboko. Jitihada za kumpata Kiboko hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.


  Kwa mujibu wa taarifa na takwimu zilizopo, mdau yeyote wa uchaguzi katika jimbo la Igunga, aweza kuiburuza NEC mahakamani; na mwanasheshia mmoja aliyeongea kwa sharti la kutotaka kutajwa jina gazeti ameongeza, "...kuiburuza mahakamani na kuishinda."


  Kuna taarifa za kuondoa majina ya wapigakura; kuongeza majina ya wengine na kuonekana, angalau kwa namba moja ya shahada isiyokuwa na jina mbele yake.

  Hata hivyo, idadi ya wapigakura wa Igunga na wale wanaotajwa na NEC kwenye uchaguzi mkuu uliopita, inapingana na idadi ya watu waliomo ndani ya daftari lenyewe, idadi ya takwimu za idadi ya watu nchini na hata mazingira halisi ya nchi.

  Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja takribani miezi 10 baada ya vyombo vya habari kuanika kile vilichoita, "Mkakati wa wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010." NEC ilituhumiwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa kupika matokeo.


  Kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu iliopita, awali NEC ilitangaza kuwapo wapigakura 20,137,303 kabla ya kuipunguza idadi hiyo hadi wapigakura 19.6 milioni, ambayo bado ilipingwa na baadhi ya wanaharakati na vyama vya siasa.

  Wakati idadi hiyo ikistukiwa na vyama, NEC ilidai waliojitokeza siku ya uchaguzi walikuwa ni 8,626,283 (42.8%); wapigakura zaidi 11,511,020 (57.2) hawakujitokeza kupigakura.

  MwanaHALISI limetaarifiwa kuwa kazi ya kuingiza wapigakura hewa na kuondoa baadhi ya majina imefanyika kwa ustadi mkubwa, kwa kuhusisha NEC na wataalam wenye ujuzi katika mawasiliano ya kompyuta (IT).


  Taarifa zinaonyesha kwenye kata ya Mbutu peke yake, wapigakura zaidi 2500 waliongezwa kwenye dafari hilo kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga. Jimbo la Igunga lina jumla ya kata 26.


  Kwa mujibu wa uchunguzi wa MwanaHALISI, daftari la wapigakura lililotumika kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana, linaonyesha wapigakura waliopo kwenye kituo cha Shule ya Msingi Mwabakima C, kata ya Mbutu, ni 382, lakini daftari lililotolewa na NEC kwa vyama vyote vya siasa katika uchaguzi mdogo wa Igunga, limetaja wapigakura 393.


  Daftari hilo lenye wapigakura 382 lilitolewa na NEC, 18 Oktoba 2010.

  Kwenye kituo hiki peke yake, daftari linaonyesha ongezeko la wapigakura 11, wakati ambapo NEC haikuwahi kufanya marekebisho yeyote kwenye daftari la wapigakura kati ya 23 Septemba 2010 na 18 Oktoba 2010, wala wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo wa Igunga.

  NEC inasema katika maelezo yake yaliyo mbele ya daftari hilo, "Daftari hili litatumika kuanzia 15 Oktoba 2010 hadi itakapotangazwa vinginevyo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi."


  Kati ya wakati huo na sasa NEC haijatangaza kusitishwa kwa matumizi ya daftari hilo.


  Kwenye kituo cha Mwambakima shule ya Msingi -3, chenye Na. 00015059, idadi ya wapigakura imeongezeka kutoka 393 waliotajwa na NEC, 18 Oktoba 2010 hadi wapigakura 419 waliotajwa kwenye uchaguzi mdogo.


  Katika orodha hiyo yupo mpigakura mmoja ambaye hana jina, wapigakura 10 wameondolewa, wapigakura watatu fomu zao zimefutwa, huku wapigakura saba wakiondolewa bila kuelezwa sababu.


  Matokeo ya uchaguzi mdogo katika kituo hicho yalikuwa kama ifuatavyo: Chama cha AFP kilipata kura 1, CCM 72, CHADEMA 71, CUF 2 na wengine wote waliosalia walipata 0.


  "Unajua ukiliangalia kwa makini daftari hili la wapigakura, utaweza kugundua madudu mengi. Kwanza, kuna wapigakura waliondolewa kinyume cha taratibu, lakini pili kuna wapigakura wameondolewa hapa na kupelekwa kwingine, huku wengine wengi wakiondolewa moja kwa moja," anaeleza mtaalamu mmoja wa IT anayefahamu kinachotendeka ndani ya NEC.


  Anasema, "Katika baadhi ya maeneo baadhi ya wapigakura wameondolewa huku majina yao yakiwa tayari yapo kwenye orodha ya wapigakura. Kwa mfano, wapo wapigakura ambao walikuwa wakiandikishwa na mabalozi wa CCM na huku shahada zao zikionekana, lakini ilipofika uchaguzi majina yao hayakuweza kuonekana. Hii yote inaonyesha jinsi taifa hili linavyoweza kuingia kwenye machafuko..."


  MwanaHALISI limegundua wapigakura waliongezeka katika kituo cha Mwambakima shule ya Msingi -3 na namba zao za shahada zikiwa kwkenye mabano.


  Hao ni Ngasa Mipawa (29611765), Ngolo Seni (29611909), Nhandi Hungilu (29611919), Nhwani Mlega (47371897), Nkinda Magembe (47371805), Peter John (29611911), Rahel Lunili (05148812) na Rahel Nhabi Buluba(24150227).


  Wengine walioongezwa kwenye daftari hilo, ni Samwel Kingi (29611760), Say Mwitagula (29611768), Sesilia Ntugwa (47371813), Shija Masanilo Tungu (24150219), Shija Chenge (29611905), Shija Itaalamu (29611770), Silvanus Mangwesi Buluba (47371821), Therezia Charles (47371814) na Tui Peter(29611915).

  Wapigakura wengine walioongezwa, ni Wande Kashinje (47371885), Zainabu Ramadhani (47371822), Zengo Buganda Saganda(7371893) na mtu ambaye hakutajwa jina wala picha yake haimo kwenye daftari mwenye kadi ya kupigia kura Na. 29611769.

  Wapigakura walioondolewa kwenye daftari bila kutolewa sababu ni pamoja na Nchambi Joseph Ntugwa (24150228), Ng'ombeyapi Machiya (05148590), Nhabi John (05148492), Njile Samwel (05148633), Nkwaya Malelemba (05148394), Nsiya Gusu ( 05148927), Poya Magoma (05148462) na Rahel Maduka (05148858).


  Vyanzo vya taarifa vinasema kuingizwa kwa wapigakura wapya kwenye uchaguzi wa Igunga, kulikwenda sambamba na maandalizi yaliyofanywa na CCM ya kupeleka wapigakura hewa zaidi ya 500 waliodaiwa kuingia ndani ya vyumba vya kupigia kura wakiwa tayari na kura zilizopigwa.


  Uchaguzi wa Igunga ulikuwa na ushindani mkubwa kati ya vyama vya CHADEMA na CCM. Hadi sasa wapo wanaoamini kwamba iwapo uchaguzi huo ungeendeshwa katika mazingira huru na haki, upinzani ungeibuka na ushindi.


  Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, NEC ilitaja wapigakura wa Igunga pekee kuwa 177, 077 huku kwenye uchaguzi mdogo wakitajwa wapigakura171,019.


  Idadi hiyo ina tofauti ya karibu kura 6000, kutoka wapigakura wa mwaka jana (2010).


  Aidha, wakati msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Igunga, Protace Magayane akitangaza idadi ya wapigakura wa uchaguzi mdogo kuwa ni 171,019, dafatri la wapigakura lililotolewa kwa vyama vya siasa 23 Septemba 2010, linaonyesha wapigakura wa Igunga ni 170,586 tu.


  Kuna mikanganyiko inayozaa shaka na ambayo yaweza kuigharimu NEC au viongozi wake na hata CCM.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tanzania tuna wasomi wengi toka kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha Dar es salaam; kwanini kati ya hao wasomi hapo chuoni wasiwe viongozi na makatibu katika Tume yetu ya Uchaguzi? Ile iwe huru kama ya Kenya?

  Sio kuchagua Vizee vilivyochoka? Kweli kama tume ya Uchaguzi ikiwa huru kweli kweli BYE BYE CCM...

  Let's wait and see haya matatokeo...
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hahahaaaaaaaaa! nadhani nuji kwamba 'Politics always takes a course different from that inspired by majority people"
   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,801
  Likes Received: 6,311
  Trophy Points: 280
  Kuingia kwenye uchaguzi wa 2015 kwa tume hii ya sasa na kutegemea kwamba CCM itang'olewa madarakani is utter naivity. Sijui ni nani atatuongoza kwenye mwongozo wa kudai Tume huru ya Uchaguzi kabla ya 2015.

  CCM na serikali yake wanajua faida wanayoipata sasa na kamwe hawatakuwa wa kwanza kutaka utaratibu huu ubadirike. Wenzetu nchi jirani wanaweza, kwanini sisi hatuwezi??
   
 5. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Bado nape anatamba nduh! kama ndio uchakachuaji ndio ulivyo hawa watu hawana nia ya kuongoza vizuri majimbo na nchi nia yao ni ubinafsi tu so njia zote zitatumika kuendelea kuwa juu..

  Mwenyezi Mungu tu ndie atatuokoa na hawa Waovu
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwanini chadema isipite kata zote 26 ikakusanya majina ya watu wote waliokataliwa kupiga kura ili iwe na ushahidi wa kutosha kwa maana wananbidi wawe na idadi ya wapiga kura waliokataliwa ili ionekane kama idadi yao ikngeweza kubadili matokeo kwahiyo ushauri wangu kwa chadema ikusanye majina ya wanachama wao wote ambao walizuiwa kupiga kura kw ajili ya kufikisha mahakamani.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hii inaonyesha ndio last link ya CCM controlling our beloved Country
   
 8. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mpaka hapa tulipofika sasa na hii ccm huwa napata shida sana kuelewa kwanini watanzania wanaipigia kura ccm.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Tuhuma na ushahidi uliopo hapo ni very credible; hatua stahiki zichukuliwe.

  Yaani ccm wamafanikiwa sana hasa chini ya Kikwete kuharibu kila taasisi au jina jema Tz iliokuwa nayo. Hata neno "tume" halina maana tena kama vile neno "uchaguzi" lilivyopoteza mashiko. Nasubiri taarifa rasmi ya CDM kwa hili na yote yalijiri Igunga.
   
 10. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Panapokuwa na uchaguzi daftari la wapiga kura hupelekwa CCM, kisha huanza kuchakachua majina kwa kutumia IT wao wakisaidiana Usalama wa Taifa pamoja na NEC, ndiyo maana majina hubandikwa siku moja kabula. Hiki ni kichekesho na kituko cha aina yake.
   
Loading...