Tume ya uchaguzi ilidhalilishwa, Star tv ifutiwe leseni ya kurusha matangazo

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Katika hali isiyo ya kawaida, uchaguzi mdogo wa marudio wa Udiwani kata ya Nyampulukano, jimbo la Sengerema mwaka 2013. Uchaguzi huo mdogo ulikuwa na kashkash nyingi sana na za kukatana na mapanga, siku ya jumapili ambayo ilikuwa ni ndio siku ya kupiga kura, kila chama kilikuwa kinazunguukia vituo vya kupiga kura.

Gari ndogo iliyokuwa inatumiwa na viongozi wa chama cha NCCR Mageuzi ambayo ilikuwa na Katibu wa wilaya wa Nccr Mageuzi wa Sengerema, pia alikuwemo Katibu wa Uenezi wa Vijana Taifa wa NCCR Mageuzi Ndugu Deogratius Kisandu, kwasasa yuko CCM. Na mwanachama mmoja na dreva. Walisimamishwa kona ya kuingia eneo la kupigia kura na waandishi wa habari na maaskari wawili tuliokuwa nao katika uchaguzi huo.

Waandishi waliuliza mbona mnaingia eneo hili, tukawaambia sisi ndio wenye uchaguzi na wasimamizi kupitia chama huku wakichukua video kwa kurekodi mazungumzo.

Cha kushangaza kesho yake Star Tv wakarusha kwenye Taarifa ya habari kwamba wale walikuwa ni Magaidi na majambazi, tena wakimtaja ndg. Deogratius Kisandu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi kutoka Taifa upande wa chama cha Nccr Mageuzi.

Kitendo hiki cha udhalilishaji kuna haja Tume ya Uchaguzi kufungua kesi kudhalilishwa kwa wasimamizi wa uchaguzi, na Wanasiasa kuishitaki Star Tv kwa kupotosha Umma kwa kuzusha Mtanzania mwenzetu ni Gaidi na jambazi, kumbe anasimamia uchaguzi.

Deogratius Kisandu, yeye amekwisha jiandaa kufungua kesi ya udhalilishaji na anataka kulipwa Trioni 5 kama fidia za kumfezehesha kwa jamii.

Taifa linaenda wapi
 

Attachments

  • nccr.jpg
    nccr.jpg
    12.3 KB · Views: 36
Cha kushangaza kesho yake Star Tv wakarusha kwenye Taarifa ya habari kwamba wale walikuwa ni Magaidi na majambazi, tena wakimtaja ndg. Deogratius Kisandu ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi kutoka Taifa upande wa chama cha Nccr Mageuzi.
Mimi sioni wapi Tume ya uchaguzi imedhalilsihwa. Huoni kwa kuwaita Deogratius Kisandu ni gaidi ndiko kulikomfanya ahame NCCR-Mageuzi na kuhamia CCMkwa ajili ya kupata hifadhi?
 
Mmh!! Mkuu Nyoosha Maelezo.

Halafu Kwann Mashtaka Yaanze Sasa Kwa Tukio La 2013? Kisandu Kwa Kuwa Sasa Ni Mwanaccm Asijekuwa Anataka Kututoa Kwenye Reli Ya Kujadili Yanayoendelea Nchini.

Mleta Mada Una Taarifa Hz?
>max Melo Kesi Yake Leo
>lema bado yuko rumande
>ben saanane hajulikani alipo
>miili 7 ya ruvu bado kizungumkuti
>mange kimambi amechoma kadi ya ccm.
TUJADILI HAYA MKUU
 
Back
Top Bottom