sanshinda
Member
- Sep 25, 2017
- 79
- 33
Ibara ya 74 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inatamka kwamba,
“Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili
kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) Wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge”.
Ibara ya 74 (7) ya Katiba inasema kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.