Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Weston Songoro

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Messages
2,793
Likes
494
Points
180
Age
38
Weston Songoro

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2014
2,793 494 180
1.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na maandalizi ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuboresha daftari la wapiga kura ili kuweka taarifa za walengwa wakiwemo watakaopiga kura baada ya kufikisha umri wa kupiga kura.

Aidha, itawahusu walioshindwa kupiga kura katika chaguzi zilizopita kutokana na sababu mbalimbali. Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na Ofisa Uchaguzi wa Tume hiyo, Adam Nyando wakati akikabidhi taarifa za Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa mkoa wa Pwani.

Alisema, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa mwaka 2015, wameanza maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao na si kwamba kwa sasa Tume imelala.

“Watu wanafikiri uchaguzi ukishaisha ndio kazi imekwisha kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi ujao kwani kwa sasa tunaendelea na uboreshaji wa daftari la wapigakura pamoja na kura za maoni,” alisema Nyando.

Alisema uchaguzi uliopita ulikwenda vizuri na hakukuwa na matatizo makubwa licha ya matumizi ya mfumo mpya wa BVR, lakini matokeo yake umekuwa mfumo mzuri na umepata mafanikio makubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, akizungumza alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kufanya uchaguzi mzuri usiokuwa na vurugu wala uvunjifu wa amani.

Ndikilo alisema nchi nyingine kipindi cha uchaguzi ni kipindi kibaya cha uvunjifu wa amani, ikiwa ni pamoja na umwagikaji mkubwa wa damu, hasa kwa pande zisizokubaliana matokeo.

“Uchaguzi ulienda vizuri licha ya changamoto zilizojitokeza za hapa na pale lakini watu walivumiliana na kukubaliana na matokeo kilichobaki sasa ni kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi, kikubwa ni tume kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na usafiri na ucheleweshwaji wa matokeo kwa baadhi ya sehemu,” alisema Ndikilo.

Akikabidhi taarifa hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ofisa Uchaguzi wa mkoa, Shangwe Twamala alisema mkoa huo umepata nakala 47 ambazo zitasambazwa kwa wadau mbalimbali wa uchaguzi.
Alisema taarifa hizo zitasambazwa kwenye ofisi za mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri za miji na wilaya na taasisi za elimu ya juu.

Chanzo: Mpekuzi
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
CCM maandalizi yetu yanaanza baada ya Magufuli kukabidhiwa chama Julai 23
 
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Messages
19,343
Likes
11,644
Points
280
K

kabombe

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2011
19,343 11,644 280
CCM maandalizi yetu yanaanza baada ya Magufuli kukabidhiwa chama Julai 23
Ukawa wapo mahakamani wakitaka bunge liwe live na Tulia ang'olewe na mahakama! Maajabu ya dunia haya
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,875
Likes
50,220
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,875 50,220 280
Wamuingize na Jecha kwenye NEC ili tume iwe na sura ya kitaifa
 
ZILLAHENDER MPEMA

ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2015
Messages
2,057
Likes
4,158
Points
280
ZILLAHENDER MPEMA

ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2015
2,057 4,158 280
Ukawa wapo mahakamani wakitaka bunge liwe live na Tulia ang'olewe na mahakama! Maajabu ya dunia haya
Kama itakavyokuwa ajabu la kidunia kwa wewe kuishi bila kuvuta hewa iitwayo"UKAWA",bila kuitaja ukawa unaweza kufa.
 
Mwana

Mwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Messages
5,061
Likes
1,405
Points
280
Mwana

Mwana

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2010
5,061 1,405 280
Ukawa wapo mahakamani wakitaka bunge liwe live na Tulia ang'olewe na mahakama! Maajabu ya dunia haya
Umeona eeh. Wanadhani mwaka 2020 ni mbali,kazikupoteza muda na tunawalipa mshahara bika kufanya kazi!
 
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Messages
10,029
Likes
7,652
Points
280
Age
31
Victor wa happy

Victor wa happy

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2013
10,029 7,652 280
Wamuingize na Jecha kwenye NEC ili tume iwe na sura ya kitaifa
Na lubuva ametufanyia Nazi nzuri ya kupindua matokeo asistafishwe kwa manufaa ya chama na dola
 
M

Mssassou

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2015
Messages
1,540
Likes
237
Points
160
M

Mssassou

JF-Expert Member
Joined Jun 17, 2015
1,540 237 160
LOWASSA KIPENZI CHA WATU UTASHINDA URAIS
 
maonomakuu

maonomakuu

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Messages
2,519
Likes
979
Points
280
maonomakuu

maonomakuu

JF-Expert Member
Joined Jul 24, 2015
2,519 979 280
Wanasiasa wamekatazwa kufanya siasa Lubuva anaandaa uchaguzi 2020.Duuu ayse tumpate wapi mtu jasiri kama Malema wa Afrika Kusini?
 
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
1,469
Likes
1,809
Points
280
John Cannor

John Cannor

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
1,469 1,809 280
Maandalizi ya CCM kutengenezewa mazingira bora zaidi ya goli la mkono.

Hamtashinda!!
 
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
12,368
Likes
4,002
Points
280
Age
58
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
12,368 4,002 280
1.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na maandalizi ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020 kwa kuboresha daftari la wapiga kura ili kuweka taarifa za walengwa wakiwemo watakaopiga kura baada ya kufikisha umri wa kupiga kura.

Aidha, itawahusu walioshindwa kupiga kura katika chaguzi zilizopita kutokana na sababu mbalimbali. Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na Ofisa Uchaguzi wa Tume hiyo, Adam Nyando wakati akikabidhi taarifa za Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa mkoa wa Pwani.

Alisema, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa mwaka 2015, wameanza maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao na si kwamba kwa sasa Tume imelala.

“Watu wanafikiri uchaguzi ukishaisha ndio kazi imekwisha kumalizika kwa uchaguzi mmoja ni maandalizi ya uchaguzi ujao kwani kwa sasa tunaendelea na uboreshaji wa daftari la wapigakura pamoja na kura za maoni,” alisema Nyando.

Alisema uchaguzi uliopita ulikwenda vizuri na hakukuwa na matatizo makubwa licha ya matumizi ya mfumo mpya wa BVR, lakini matokeo yake umekuwa mfumo mzuri na umepata mafanikio makubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, akizungumza alitumia fursa hiyo kuwapongeza Watanzania kwa kufanya uchaguzi mzuri usiokuwa na vurugu wala uvunjifu wa amani.

Ndikilo alisema nchi nyingine kipindi cha uchaguzi ni kipindi kibaya cha uvunjifu wa amani, ikiwa ni pamoja na umwagikaji mkubwa wa damu, hasa kwa pande zisizokubaliana matokeo.

“Uchaguzi ulienda vizuri licha ya changamoto zilizojitokeza za hapa na pale lakini watu walivumiliana na kukubaliana na matokeo kilichobaki sasa ni kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo wananchi, kikubwa ni tume kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na usafiri na ucheleweshwaji wa matokeo kwa baadhi ya sehemu,” alisema Ndikilo.

Akikabidhi taarifa hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ofisa Uchaguzi wa mkoa, Shangwe Twamala alisema mkoa huo umepata nakala 47 ambazo zitasambazwa kwa wadau mbalimbali wa uchaguzi.
Alisema taarifa hizo zitasambazwa kwenye ofisi za mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri za miji na wilaya na taasisi za elimu ya juu.

Chanzo: Mpekuzi
Na huyu mzee, basi namwachia Mungu
 
Forum statistics

Threads 1,239,056
Members 476,371
Posts 29,340,793