Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufumuliwa

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
IMG_20220411_075822_556.jpg

  • Kuajiri watumishi wake hadi ngazi ya Wilaya, kata
  • Sasa rasmi kusimamia uchaguzi Serikali za Mitaa
  • Mapendekezo ya muundo wake yasubiri wadau
===
Kwa mujibu wa Gazeti la Raia Mwema la Aprili 11, 2022 ni kuwa kuna uwezekano mkubwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuundwa upya kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

Aidha, gazeti hilo linaelezwa kuwa taarifa za ndani ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kikosi kazi zinaeleza kuwa tayari mapendekezo ya kuunda upya kwa NEC yameshawasilishwa kwa Rais Samia na ndani ya muda mfupi chombo hicho kitaundwa upya.

Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa kiongozi Mwandamizi ndani ya CCM alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi iliyopo sasa imeonekana machoni mwa watu kuwa imeshindwa kusimamia uchaguzi hasa kutokana na muundo wake uliopo kwa sasa, hivyo kikosi kazi kimependekeza Tume hiyo iwekewe Muundo mpya ikiwamo watendaji wake.

Taarifa juu ya kufumuliwa kwa Tume ya Uchaguzi zinakuja baada kuwapo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya Muundo wa NEC pamoja na Mamlaka ya Tume hiyo kushindwa kusimamia Uchaguzi Huru na Haki.

Zaidi kuhusu taarifa hizi soma hapa chini

1649658622151.png


1649660441173.png

1649660485126.png

1649660516341.png


Chanzo: Raia Mwema
 
Back
Top Bottom