Tume ya Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mizambwa, Apr 24, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Watanzania tumeshuhudia TUME nyimgi zikiundwa na Marais. Nakumbuka Raisi Mwinyi aliunda Tume ya Maoni ya Wananchi kuhusu Vyama Vingi. Na matokeo yake tulielezwa na yakafanyiwa kazi.

  Rais Mkapa aliunda Tume nyingi mfano tume ya Rushwa iliyoongozwa na jaji Warioba; na nyingi siwezi hata kuzitaja. Matokeo yake aliyajua mwenyewe kwani hayakuwekwa hadharani

  Rais Kikwete ameunda na anaendelea kuunda Tume nyingi na matokeo yake hatuelezwi na pia hayafanyiwi kazi. Mfano tume ya hivi karibuni kuhusu Mgomo wa Madaktari. Na taarifa alikabidhiwa Spika wa Bunge. Tulitaraji tutaelezwa Bunge lililoishia jana. lakini nayo kimya.

  Tume ya kufuatilia mauaji ya Songea, hadi leo kimya. Afande Chagonja na timu yake wamesharudi.


  Je, wadau kuna umuhimu gani wa kuunda hizi tume? Je, pesa zinazotumika zimepitishwa na Bunge lipi?  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 2. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 256
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Na hata hii tume ya katiba mpya, usitarajie kitu kipya. Mkubwa Akija kukuta kipengele kinachosema "Rais na mawaziri waliobainika kuiba pindi walipokuwa madarakani lazima washtakiwe". Katiba itatupwa hiyo....
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ni kitu kigumu sana kutangaza maoni ya tume iwapo hata wewe kama rais unaguswa. Kwa mfano mauaji ya Songea hata Rais anahusika.
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Kweli lazima ataifunika tu. Akikuta yanayomkaba hatokubali. Vinginevyo atajifanya kama hakuliona na lisiwekwe katika katiba


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Tume ni tactic mkuu,

  Joto linakuwa kubwa na usipounda tume hakitaeleweka. sio tanganyika tu sehemu nyingi hii kitu inatumiwa sana kupunguza munkari.

  Nabii gani mtarajiwa usiojua mambo madogo kama haya
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  NDUGU UNATAKA KUNIVUNJA MBAVU KWA KICHEKO, hunihurumii hizi MBAVU nilivyokonda na kuwa mifupa mitupu!!!

  Utabiri wangu unaonyesha kuwa Tulipo ni Pabaya na Tunakoelekea ni Pabaya zaidi.

  Hivyo tuchunguze umuhimu wa hizi tume zisizo kuwa na majibu.


  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...