PostGE2025 Tume ya Rais inachunguza nini kwa miezi mitatu?

PostGE2025 Tume ya Rais inachunguza nini kwa miezi mitatu?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601
Tume Tume Uhuru ya Uchunguzi wa matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya uchaguzi iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan imepewa miezi mitatu kutekeleza majukumu yake.

Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Chande Othman ina wajumbe wengine ambao ni pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma.

Wengine ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue Balozi Mstaafu Balozi Radhia Msuya, Balozi Mstaafu Lt. Gen. Paul Meela, Balozi Mstaafu David Kapya na Dkt. Stergomena Lawrence Tax aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kumekuwa na maoni kwamba tume hii hjaiwezi kuwa huru, kwanza kwa sababu Rais Samia aliyeiteua pia analalamikiwa kwenye mambo hayo hayo anayochunguza. Huu ni ukweli, kwama huwezi ukatuhumiwa au ukalalamikiwa, halafu ukajiundia tume kujichunguza.

Serikali haiwezi kukwepa lawama kwa vurugu zilizotokea Oktoba 29 na kuendelea, kwanza kwa sababu taarifa za kuwepo kwa maandamano zilikuwepo na waliokuwa wakiyatangaza walikuwa na malalamiko yao, lakini hawakusikilizwa.

Miongoni mwa malalamiko ambayo, hata CHADEMA walikuwa wakiyasema ni kupatikana kwa mfumo bora wa uchaguzi na ndio maana hata hawakushiriki kabisa. Ni ukweli kwamba mfumo wa uchaguzi uliopo sasa ni wa kuipendelea tu CCM na siyo vinginevyo na ndivyo ilivyofanyika kwenye uchaguzi huu.

Malalamiko mengine ni pamoja matukio ya utekaji kwa wakosoaji wa Serikali. Watu wameimba kila siku lakini Serikali haikuchukua hatua. Miongoni mwa waliokemea matukio hayo ni Askofu Josephat Gwajima, lakini alichoambulia ni kufungiwa kanisa lake, ambalo sasa limefunguliwa.

Serikali iliyasikia malalamiko haya lakini iliyajibu kwa vitisho vya kuwashughulikia kijeshi walalamikaji. Matokeo yake ndiyo hayo ya Oktoba 29.

Kwa hiyo, ilitakiwa Serikali iruhusu tume huru ya kuchunguza haya matukio na kuja na majibu yasiyopendelea upande wowote. Sio lazima iwe tume kutoka nje ya nchi, bali inaweza kuchukua watu kutoka makundi ya dini, asasi za kiraia, waandishi wa habari, viongozi wastaafu. Pia ilitakiwa iwekewe kinga ya kisheria ya kutokuingiliwa kimaamuzi na mtu yoyote yule. Nje ya hapo, tume hii haina uhuru.

Mbali na uhalali wa tume, jambo la kujiuliza ni kuhusu muda iliyopewa wa miezi mitatu, wanachunguza nini kwa muda wote huo? Hata mambo aliyotangaza Rais Samia wakati anaizundua tume hiyo, hayawezi kuchukua muda wote huo.

Kuchunguza kama vijana wanataka nini? Hilo ni swali la wazi, labda kama muuliza swali hatambui wanachotaka. Kuchunguza kama waandamanaji walilipwa fedha, au kuchunguza uhusiano wa vyama vya siasa na Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi? Haya yote ni mambo yaliyo wazi kabisa.

Kimsingi, tume hii imeundwa ili kusahaulisha watu machungu. Watu wana uchungu wa kufiwa na ndugu zao, wengine wamejeruhiwa, achilia mbali waliopoteza mali zao. Tumemsikia Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amenukuliwa akisema Novemba 23, kwaamba wanaotaka kujua idadi ya vifo vilivyotokea, wapeleke maswali hayo kwa Tume Huru ya uchunguzi.

Maana yake hapo ni kwamba Serikali inakiri kwamba kuna watu wameuawa, lakini haitaki wazungumziwe, kwa sababu ni aibu kubwa kwa nchi, hasa kwa jumuiya za kimataifa, ambazo zinainyooshea kidole.
Wakati watu waliofariki wakifichwa idadi yake, tunaona viongozi wa Serikali wakitembelea miundombinu iliyoharibiwa katika vurugu hizo. Je, hizo hazitachunguzwa na hiyo tume? Kama Serikali inaanza kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na kurejesha hali ya kawaida, maana yake inapaswa pia kumaliza kwa kueleza vifo vilivyotokea.

Kinachoonekana ni kwa hii tume ni kujaribu kuchelewesha hata mchakato wa maridhiano, kwa sababu hata Rais Samia alisema ile ahadi yake ya kuunda Tume ya Maridhiano na upatanishi atatitekeleza baada ya tume hii ya sasa kukamilisha kazi yake.

Maana yake hapo ni kuwaziba midomo waandishi wa habari na hata wananchi wa kawaida, wasihoji kuhusu vifo, wasihoji sana Serikali kuhusu ukatili wa vyombo vya ulinzi na usalama, maana wataambiwa hayo mambo yanachunguzwa na tume.

Baada ya miezi hiyo mitatu, watu watakuwa wamesahau, wengine watakuwa wamechoka kufuatilia mambo yaliyofanywa na Serikali. Hapo sasa ndipo wataanza kuzungumzia maridhiano. Kwa maana hiyo hii tume itakuwa imetumika kuisafisha Serikali na lundo la malalamiko yanayoikabili kwa sasa.
 
Hakuna chochote wanachokwenda kukifanya kwa huo muda. Hiyo miezi 3 ni kujaribu kusogeza muda tu.

Tume tayari ishaambiwa nini wakakichunguze .....!!
 
20251121_150943.png
 
Hakuna chochote wanachokwenda kukifanya kwa huo muda. Hiyo miezi 3 ni kujaribu kusogeza muda tu.

Tume tayari ishaambiwa nini wakakichunguze .....!!
Yaani ripoti ya tume iko tayari, inasubiri tu siku ya kusomwa, maana serekeli ndio wameandika wenyewe.
 
Ni upotevu wa muda na upigaji wa pesa.
Hotuba ya Rais kwa wazee wake wa Dar amejibu yote.
Kaongelea sababu ya alizoita vurugu kutokea.
Pia kaongelea sababu ya wafanya vurugu kuuliwa.
Sasa tume aliyoiunda yeye mwenyewe sioni ikija na majibu tofauti na aliyoyasema.
 
Samuya aliishatoa majibu sijui wao wanachunguza nini?
 
Back
Top Bottom