Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Wazo zuri mkuu linalojenga fikra za kila mtanzania mwenye nia njema kwa nchi yetu bila kujali itikadi na udini,tujenge nchi yetu. Maoni ya kwenye tume ya katiba ni haya; 1.kupunguza madaraka ya rais, 2.mwanasheria,jaji mkuu-wasiteuliwe vitazamwe vigezo,3.nafasi ya wabunge wa viti maalum iondolewe,wakuu wa wilaya na mikoa wasiwepo
Madaraka ya Rais yapunguzwe maana yake ni nani? Hivi ktk hili tunaongea lugha moja kweli? Naomba ufafanuzi maana linasemwa na wengi. Tunahitaji uelewa mmoja ( Common understanding) :yawn:
kuwe mbadala ambaye atapigiwa kura hapa napendekeza serikali iwe na mfumo wa kimajimbo,pia tume ya uchaguzi iwe huru isiteuliwe na rais,makatibu wa wizara wasiteuliwe,wananchi wawe na haki ya kuwaengua diwani au mbunge asiewajibika kwa kupiga kura kutokua na imani naoKapo,
Mawazo yako ni mazuri, lakini ukisema mkuu wa mkoa na wilaya waondolewe nataka vile vile nisikie pendekezo lako nafasi hiyo awepo nani? Au wasiwepo bila replacement? Pili pengine ulitaka kusema kuwa abaki mkurugenzi wa wilaya peke yake? Je, mkiti wa Halmashauri na mkurugenzi nani mkubwa? Nahitaji maelekezo yako zaidi. Kumbuka, Ninaya printi haya mawazo yenu na kuwapa vijana wengine hiyo be very clear and to the point.
Napendekeza tutumie zaidi kiswahili ili msinipe kazi ya kuwatafsiria wawasilishaji wa hoja hizi.
Kwangu mimi, sitaki kuona rais anateuwa wakuu/watendaji kwenye mhimili mwingine wa dola e.g Mahakama. Mahakama iwekewe utaratibu wake pembeni kabisa wa kupata watendaji wakuu including, jaji mkuu, prosecutor etc. Na hawa wafanyiwe vetting/clearance na wawakilishi wa wananchi yaani bunge kabla ya baada ya kupata mchujo toka kikosi kazi ya kudahili watendaji wa mhimili.
Pia rais asihusike kabisa kuteua wakuu wa mashirika ya umma. DGs wa haya mashirika wapikane kwa njia za ushindani wa ajira.
Sambamba na hili wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wapatikane kupitia bunge. Rais anaweza kupendekeza majina lakini wabunge ndio sauti ya mwisho kama aliyependekezwa anafaa au la.
(sijui hili kama ni la kikatiba) lakini ningependa kuona uwazi zaidi juu watu wanaomtembelea rais, na viongozi wengine wa umma including wabunge. Wananchi wajue ni mkubwa gani alienda kuonana na mkubwa yupi.
Sasa naona tuko pamoja,
Ninaongeza pia kuwa
Kazi za kamati za bunge zifanywe kwa uwazi na mbele ya vyombo vya habari. Wakati kamati za bunge zinahoji watendaji wakuu vyombo vya habari viruhusiwe kuonesha except kwa mambo ya usalama wa nchi kama ambavyo itabainishwa.
Kila waziri lazima ahojiwe na kamati husika ya bunge (kila mwaka) kuhusu utendaji wa kazi wizarani kwake. Na mahojiano hayo yawekwe wazi.
Rusheni kideo japo cha simuKuna hili la mipaka ya dola kwa wabunge wa vyama vyote sawia. Sasa hivi kuna uzi mpya umeanza Polisi wapo mlangoni kwa Bunge wakitaka kumdaka J Mnyika. Sijui kama wameshapata ruhusa ya Speaker. Au ruhusa kwa Chama tawala tu? Hili naomba mawazo yenu pia.