Tume ya Katiba mpya, ni jambo gani ungetaka tukakusemee kwenye mikutano inayoendelea?

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
WanaJF,
Jumamosi, Mungu akinijalia nitahudhuria mkutano wa kwanza wa Tume ya Katiba watakapokuwa Kisarawe,pwani. Jambo hilo tunalifanya makusudi ili tupanguze yale tuliyo nayo kabla hatujapata fursa nyingine Dsm.

Kwa kuwa zoezi hili linaenda kwa kasi sana, na kwa kuwa hatuna uhakika kama tunaweza kusema kila kitu wakija hapa Dsm, na kwa kuwa hawaendi kila mahali (nina maanisha kila kata au mtaa wako) na
kwa kuwa baadhi yetu wanajf ni waajiriwa na tuko busy na hamtapata nafasi hii adimu sana na,
kwa kuwa tayari kuna malalamiko ya wakuu wa wilaya kuwaandaa watu na kuwafundisha kitu cha kusema, na kwa kuwa baadhi ya wana Jf wako nje ya nchi na wanaitakia mema nchi yetu (mf mwanakijiji etc)
Hivyo basi, kwa heshima na unyenyekevu tunaomba tukakuwakilishie hoja yako unayoona ni muhimu sana kupitia jukwaa letu murua na ambayo unahisi ni muhimu ikajumuishwa katika katiba mpya.

Tumejipanga kuhakikisha kuwa kila hoja muhimu inayoboresha muskabali wa watanzania wote bila kujali mipaka vyama, dini, kabila inawasilishwa kwenye tume husika bila upendeleo.

1) IKUMBUKWE; Vyama vinazaliwa na kufa lakini Taifa letu lipo hadi mwisho wa Dunia, hivyo ni matarajio yangu kuwa ushabiki wa kidini na kisiasa hautakuwepo ktk mjadala huu.

2) Fafanua vizuri hoja yako ili ieleweke vizuri, kiasi kwamba mwana JF ye yote ambaye atapata fursa ya kuhudhuria mikutano hii ya Katiba aweze kuelezea vizuri kwa niaba yako (siyo lazima sisi).
Sisi (kama watanzania kwanza kabla ya kuwa wanachadema) tunajitahidi kuratibu vizuri kila mahali lakini siyo garantii kuwa tutawasilisha kila jambo.

Kwa hiyo, napendekezo uzi huu hapa JF uwe kisima cha kuchukua mawazo mapya kwa kila mwana jf kutoa hoja hapa ama kuchota mawazo mapya na kuyawasilisha ktk tume husika kwa kuwa tunatofautiana uwezo wa kuibua mambo yenye maslahi kwa nchi yetu, Pili,inawezekana hoja yako mimi sikubaliani nayo, hivyo yule mwenye mawazo kama yako atayawasilisha kwa niaba yako.

NB; Paw,Silencer, PainKiller, Roulette, Fang, Buchanan, Cookie ni matarajio yangu kuwa uzi huu mtaupa muda kidogo ili tupate mawazo mengi kwa maslahi ya nchi yetu.

Regards
Aweda, Mikael
 
Wazo zuri mkuu linalojenga fikra za kila mtanzania mwenye nia njema kwa nchi yetu bila kujali itikadi na udini,tujenge nchi yetu. Maoni ya kwenye tume ya katiba ni haya; 1.kupunguza madaraka ya rais, 2.mwanasheria,jaji mkuu-wasiteuliwe vitazamwe vigezo,3.nafasi ya wabunge wa viti maalum iondolewe,wakuu wa wilaya na mikoa wasiwepo
 
Wabunge wawajibike moja kwa moja kwa wananchi waliowachagua ili utendaji wao usiporidhisha basi wawaondoe, polisi wapunguziwe nguvu waliyonayo tangu wanapomkamata mtuhumiwa mpaka kufikishwa mahakamani asipigwe wala kuonewa, askari wa usalama barabarani waondolewe madaraka makubwa waliyonayo ya kukamata gari, kumnyanganya dereva funguo na leseni mpaka wanapoamua, uundwe mfumo mpya wa utawala tuwe na majimbo na kila jimbo ljitegemee na rasilimali zao wenyewe.

Siku yenye matukio ya kitaifa kama sensa, kupiga kura, sherehe za maadhimisho mbalimbali zote zifanyike siku za kazi ili wanachi washiriki badala ya sasa ambapo zinafanyika siku za Jumapili amabapo watu wanakuwa wameenda ibada kukutana na Mungu wao.

Kwa hiyo zifanyike siku za Kazi kama Jumatatu nk.
 
1. Mawaziri wasitokane na wabunge ili wabunge wafanye kazi yao ya uwakilishi kwa nafasi. 2. Spika wa bunge asitokane na vyama ili bunge liweze kuendeshwa kwa usawa. 3. Tume huru ya uchaguzi(raisi asihusike kwenye uundwaji wake) 4. Watanzania wengi sana wamekua wakikosa haki ya kupiga kura hasa kutokana uhamaji/uhamiaji na ukuaji wa binadamu. Ianishwe kwenye katiba hata unapotokea uchaguzi mdogo wahusika wa eneo la uchaguzi waboreshewe taarifa na uandikishaji mpya.
 
Michael, mchango wangu tafadhali:

1. Serikali ya Tangayika irudi pamoja bendera yake, wimbo na mamla kamili kuhusu mambo ya Tanganyika.

2. Rais lazima apate 50+1% ya kura zilizopigwa

3. Kuwepo na nafasi mbili tu za viti maalum kwa ajili ya walemavu i.e mwanamke mmoja na mwanaume mmoja. Basi. Viti maalum nje ya hapo vifutwe kabisa kabisa kabisa.

4. Baraza la mawaziri lisizidi 18 (maximum)

5. Wakuu wa mikoa wapatikane kwa kura. Tufute wakuu wa wilaya na badala yake kuwepo na local council officials ambao wataomba kazi, kufanyiwa udahili na wapewe contract za kazi based on perfomace.

6. Kila anapochaguliwa rais mpya, automatically mabalozi (ambassadors) wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wana-step down. Kila rais apate fursa ya kusuka upya team nzima ili kutimiza yale aliyoahidi kwenye campaign. Huwezi kuwa na ambassador ambaye ni swaiba wa mshindani wako na alipewa kazi na msindani wako. Huku ni kutegana.

7. Kiongozi yoyote wa umma akikumbwa na kashfa ya kimaadili i.e rushwa, matumizi mabya ya madaraka, etc. sharti asimame pembeni haraka ili kupisha uchunguzi huru, mambo ya hukumu au innocency baadae.

8. Spika wa bunge na Naibu wake lazima wawe na degree ya sheria from a recognised institution. Spika/Naibu Spika anaweza kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini asiwe mjumbe wa kamati yoyote ndani ya chama chake e.g NEC, CC etc. Hivyo hivyo, katibu wa bunge lazima awe na degree ya sheria lakini pia awe na experience kwenye mambo ya sheria.

9. Judge mkuu, mwanasheria mkuu na DCI lazima wafanyiwe vetting/clearance na bunge. Sambamba na hili majaji wote na watendaji wakuu wa mahakama wapatikane kwa kufanyiwa udahili (kwa uwazi mbele ya umma/tv.) na record zao za nyuma ziangaliwa ili kujua kama wanasimamia haki au la. Ni muhimu kuhakikisha mhimili huu unakuwa huru.
 
Wazo zuri mkuu linalojenga fikra za kila mtanzania mwenye nia njema kwa nchi yetu bila kujali itikadi na udini,tujenge nchi yetu. Maoni ya kwenye tume ya katiba ni haya; 1.kupunguza madaraka ya rais, 2.mwanasheria,jaji mkuu-wasiteuliwe vitazamwe vigezo,3.nafasi ya wabunge wa viti maalum iondolewe,wakuu wa wilaya na mikoa wasiwepo

Kapo,
Mawazo yako ni mazuri, lakini ukisema mkuu wa mkoa na wilaya waondolewe nataka vile vile nisikie pendekezo lako nafasi hiyo awepo nani? Au wasiwepo bila replacement? Pili pengine ulitaka kusema kuwa abaki mkurugenzi wa wilaya peke yake? Je, mkiti wa Halmashauri na mkurugenzi nani mkubwa? Nahitaji maelekezo yako zaidi. Kumbuka, Ninaya printi haya mawazo yenu na kuwapa vijana wengine hiyo be very clear and to the point.
Napendekeza tutumie zaidi kiswahili ili msinipe kazi ya kuwatafsiria wawasilishaji wa hoja hizi.
 
1. Madaraka ya rais yapunguzwe

2. Bunge ndio liwe chombo kikubwa zaidi cha kutoa maamuzi na sio rais. Bunge liwe na madaraka ya kuwajibisha mtendaji yeyote wa serikali ikiwa ni pamoja na rais.

3. Ili kuondoa nafasi ya rushwa kwenye mikataba mikubwa, mikataba hiyo isitiwe saini bila kupitia bungeni. Vivyo hivyo kwa halmashauri.

4. Kiongozi awe na uhuru kwa kuhama chama chake cha siasa bila kupoteza nafasi yake ya uongozi, mfano Malawi Mutharika alijiondoa UDF ya Muluzi akaanzisha DPP, makamu wake Joyce Banda naye baadaye akajiondoa DPP akaanzisha PP.

5. Wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe kwa sababu hawawajibiki kwa wananchi bali kwa Rais aliyewateua. Kazi zao zifanywe na wenyeviti wa anowajibika moja kwa moja kwa wananchi. Kuwepo kwao kunalinda zaidi maslahi ya chama tawala katika ngazi hizo.

6. Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar wapewe uhuru wa kujadili na kuamua muungano wanaoutaka.

7. (Sina hakika kama hili ni la katiba lakini linaniboa sana) Mji mkuu wa nchi ni wapi? Kama kweli ni Dodoma basi rais, waziri mkuu na wizara zote wahamie Dodoma haraka iwezekanavyo. Au kama haiwezekani basi tufute mara moja mpango wa Dodoma mambo yote yafanyike Dar. Haiwezekeni kujenga mji mkuu kwa miaka ishirini. Kuwa na miji mikuu miwili ni kuongeza gharama bila sababu yeyote ile.
 
Binafsi napendekeza ngazi ya wilaya iwe na Mkiti wa wilaya atakaye chaguliwa kwa kura si madiwani na anawajibika kwa wananchi. Mkiti huyo huyo ndiyo awe Mkiti wa madiwani ( DC futilia mbali)
Pili, mkurugenzi mtendaji wa wilaya awe chini ya Mkiti wa wilaya.
Tatu Rais asiwe na mteule ktk ngazi ya wilaya.
Nne, tuwe na serikali ya Majimbo na serikali ndogo ya Kitaifa itakayokuwa na wizara chache kama fedha,( Elimu?), mambo ya nje na ulinzi. Masuala ya afya, genda, serikali za mitaa nk zibakie ktk serikali ndogo za majimbo.
Tano, tufute Mikoa ya sasa badala yake tuwe mikoa mikoa mipya mikubwa (majimbo ) ambayo ndiyo itakuwa na Bunge dogo ya ngazi hiyo. Ukiangalia TRA, Polisi, Mfumo wa TANROAD, MAHAKAMA, na mapendekezo ya juzi ya waziri wa maji utaona kuwa, yote yanalenga ktk kupunguza majukumu ya kitaifa na kubakisha machache ktk ngazi ya kitaifa.
Sita, serikali ya Tanganyika irudi kwanza kabla ya yote.
 
Madaraka ya Rais yapunguzwe maana yake ni nani? Hivi ktk hili tunaongea lugha moja kweli? Naomba ufafanuzi maana linasemwa na wengi. Tunahitaji uelewa mmoja ( Common understanding) :yawn:
 
Madaraka ya rais yapunguzwe, napendekeza yafuatayo:

Rais asiwe above the law, uwepo uwezekano wa rais kuwajibishwa na chombo kingine, mimi napendekeza bunge.

Rais asiteue majaji na wakurungenzi, hawa wanapohitajika nafasi zitangazwe, watume maombi na wapitie usaili. Hii itaondoa mambo ya kupeana zawadi ya vyeo au kulindana.

Nikirudi kwenye bunge, napendekeza kura za kupitisha bajeti au maamuzi mengine bungeni ziwe za kila mbunge binafsi, sio mfumo wa sasa wabunge wanaitikia kwa mkumbo tu "ndiyoooo". Na kura hizo ZISIWE za siri. Wananchi tuna haki ya kujua mbunge tuliyemchagua amepiga kura gani ili akirudi kwetu nasi pia tuweze kumwajibisha.
 
Madaraka ya Rais yapunguzwe maana yake ni nani? Hivi ktk hili tunaongea lugha moja kweli? Naomba ufafanuzi maana linasemwa na wengi. Tunahitaji uelewa mmoja ( Common understanding) :yawn:

Kwangu mimi, sitaki kuona rais anateuwa wakuu/watendaji kwenye mhimili mwingine wa dola e.g Mahakama. Mahakama iwekewe utaratibu wake pembeni kabisa wa kupata watendaji wakuu including, jaji mkuu, prosecutor etc. Na hawa wafanyiwe vetting/clearance na wawakilishi wa wananchi yaani bunge kabla ya baada ya kupata mchujo toka kikosi kazi ya kudahili watendaji wa mhimili.

Pia rais asihusike kabisa kuteua wakuu wa mashirika ya umma. DGs wa haya mashirika wapikane kwa njia za ushindani wa ajira.

Sambamba na hili wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wapatikane kupitia bunge. Rais anaweza kupendekeza majina lakini wabunge ndio sauti ya mwisho kama aliyependekezwa anafaa au la.

(sijui hili kama ni la kikatiba) lakini ningependa kuona uwazi zaidi juu watu wanaomtembelea rais, na viongozi wengine wa umma including wabunge. Wananchi wajue ni mkubwa gani alienda kuonana na mkubwa yupi.

Kazi za kamati za bunge zifanywe kwa uwazi na mbele ya vyombo vya habari. Wakati kamati za bunge zinahoji watendaji wakuu vyombo vya habari viruhusiwe kuonesha except kwa mambo ya usalama wa nchi kama ambavyo itabainishwa.

Kila waziri lazima ahojiwe na kamati husika ya bunge (kila mwaka) kuhusu utendaji wa kazi wizarani kwake. Na mahojiano hayo yawekwe wazi.
 
Kapo,
Mawazo yako ni mazuri, lakini ukisema mkuu wa mkoa na wilaya waondolewe nataka vile vile nisikie pendekezo lako nafasi hiyo awepo nani? Au wasiwepo bila replacement? Pili pengine ulitaka kusema kuwa abaki mkurugenzi wa wilaya peke yake? Je, mkiti wa Halmashauri na mkurugenzi nani mkubwa? Nahitaji maelekezo yako zaidi. Kumbuka, Ninaya printi haya mawazo yenu na kuwapa vijana wengine hiyo be very clear and to the point.
Napendekeza tutumie zaidi kiswahili ili msinipe kazi ya kuwatafsiria wawasilishaji wa hoja hizi.
kuwe mbadala ambaye atapigiwa kura hapa napendekeza serikali iwe na mfumo wa kimajimbo,pia tume ya uchaguzi iwe huru isiteuliwe na rais,makatibu wa wizara wasiteuliwe,wananchi wawe na haki ya kuwaengua diwani au mbunge asiewajibika kwa kupiga kura kutokua na imani nao
 
Hukumu kwa viongozi wa mali za umma.
1.akithibitika apigwe risasi hadharani.
2.afilisiwe na mali zirudishwe serekalini.
3.pawepo na kikomo cha uchunguzi na uendeshaji wa kesi zao,eg kesi za uchaguzi.

* wabunge wasizidi 150
*idadi ya mawaziri isizidi 18
*nafasi za wakuu wa wilaya zifutwe.
 
Kwangu mimi, sitaki kuona rais anateuwa wakuu/watendaji kwenye mhimili mwingine wa dola e.g Mahakama. Mahakama iwekewe utaratibu wake pembeni kabisa wa kupata watendaji wakuu including, jaji mkuu, prosecutor etc. Na hawa wafanyiwe vetting/clearance na wawakilishi wa wananchi yaani bunge kabla ya baada ya kupata mchujo toka kikosi kazi ya kudahili watendaji wa mhimili.

Pia rais asihusike kabisa kuteua wakuu wa mashirika ya umma. DGs wa haya mashirika wapikane kwa njia za ushindani wa ajira.

Sambamba na hili wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wapatikane kupitia bunge. Rais anaweza kupendekeza majina lakini wabunge ndio sauti ya mwisho kama aliyependekezwa anafaa au la.

(sijui hili kama ni la kikatiba) lakini ningependa kuona uwazi zaidi juu watu wanaomtembelea rais, na viongozi wengine wa umma including wabunge. Wananchi wajue ni mkubwa gani alienda kuonana na mkubwa yupi.

Sasa naona tuko pamoja,
Ninaongeza pia kuwa
Kazi za kamati za bunge zifanywe kwa uwazi na mbele ya vyombo vya habari. Wakati kamati za bunge zinahoji watendaji wakuu vyombo vya habari viruhusiwe kuonesha except kwa mambo ya usalama wa nchi kama ambavyo itabainishwa.

Kila waziri lazima ahojiwe na kamati husika ya bunge (kila mwaka) kuhusu utendaji wa kazi wizarani kwake. Na mahojiano hayo yawekwe wazi.

Kwenye Red,
FJM Hivi ni lazima Rais apendekeze halafu wabunge wapitishe JINA mmoja? Kwanini tusiseme kuwa Wataomba kazi kwa utaratibu tofauti kabisa wa kuchaguliwa bungeni ili wawe huru. Hapa namaanisha wakuu wa Polisi, mkiti wa tume ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Takukuru, DCI nk. Ni swali la ufahamu tu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hii ni katiba ya Muungano ,halafu wewe unasema Tanganyika irudi ,mawazo yako yatatupwa ndani ya debe au mfuko mweusi.

Ni bora useme ni lazima Katiba iainishe uwepo wa Tanganyika kama dola kamili na Zanzibar kama dola kamili zenye mipaka yao na mambo kibao.

Serikali ya Muungano iwepo kwa kuwepo kwa Tanganyika na Zanzibar
 
1. MUUNGANO wa Serikali 3 Tangayika, ZNZ na Union Govt
2. Mgombea binafsi aruhusiwe
3. RCs DC, vyeo hivi vifutwe
4. CJ achaguliwe na muhimili wa mahakama kwa kuomba na kusailiwa sio kuteuliwa Rais
5. Wabunge wasichaguliwe kuwa Mawaziri, RCs, DCs
6. Rais ateue mawaziri (WASIO WABUNGE) na wathibitishe na Bunge
7. Katiba itamuke Idadi ya WIZARA na MUUNDO wake. Sio kila Rais kujiundia Wizara zake.
8. Cheo cha PM kiondoke tubakiwe na RAIS na VP Kama Marekani
9. Rais lazima apate > 50% ya kura zilizopigwa.
10. Mgombea ubunge lazima awe at least na degree Moja na diwani at least awe amemaliza Form IV
12. Ubunge wa Vitu maalumu ufutwe
13. Sheria 40 kandamizi zilizotajwa kwenye tume ya Nyalali zifutwe
14. Tume huru ya Uchaguzi (NEC)
15. Matokeo ya Urais yaweze kuhojiwa mahakamni
 
Kuna hili la mipaka ya dola kwa wabunge wa vyama vyote sawia. Sasa hivi kuna uzi mpya umeanza Polisi wapo mlangoni kwa Bunge wakitaka kumdaka J Mnyika. Sijui kama wameshapata ruhusa ya Speaker. Au ruhusa kwa Chama tawala tu? Hili naomba mawazo yenu pia.
 
Mkuu kwanza wanatakiwa watoe nafasi ya watu kutoka maoni yako kwa njia ya simu, kwa kuwa simu zimesajiriwa itakuwa rahisi kutokuwepo kutoa maoni mara mbili

Sheria ya usalama wa taifa ibadilishwe na ijadiliwe na wataalamu, si wabunge peke yao. Iendane na hali ya sasa, ili TISS ifanye kazi ya usalama wa taifa.

Rais awe na ratiba maalum na utaratibu maalum wa kusafiri, sio asafiri anavyopenda na kila anakopenda, na anayependa kusafiri naye.

Ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa isiwe zawadi, na usitolewe kwa utashi wa rais.

Vyama vyote vya siasa viwe na vigezo vinavyopitishwa kitaifa vya wagombea ubunge, hadi urais

Wenyeviti wa vyama pia wawe na vigezo vya kitaifa

Wabunge ni lazima wawe na at least degree, kama wapo kwenye jimbo husika, kama hawapo basi hata wasio na degree waruhusiwe.
 
Kuna hili la mipaka ya dola kwa wabunge wa vyama vyote sawia. Sasa hivi kuna uzi mpya umeanza Polisi wapo mlangoni kwa Bunge wakitaka kumdaka J Mnyika. Sijui kama wameshapata ruhusa ya Speaker. Au ruhusa kwa Chama tawala tu? Hili naomba mawazo yenu pia.
Rusheni kideo japo cha simu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom