PreGE2025 Tume, serikali na vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi

PreGE2025 Tume, serikali na vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Kailima, R. K akifafanua jambo.

Na Mwandishi Wetu Dodoma.


Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, vyama vya siasa na Serikali kesho tarehe 12 Aprili, 2025 wanatarajiwa kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na vyombo vya habari mkoani Dodoma leo tarehe 11 Aprili, 2025 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhan amesema chama cha siasa ambacho hakitasaini maadili hayo hakitaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Ndugu. Kailima amesema maadili hayo yameandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 162 (1), (2) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024 ambacho kinaitaka Tume baada ya kushauriana na vyama vyote vya siasa na Serikali, kuandaa na kuchapisha katika Gazeti la Serikali Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zitakazoainisha maadili ya vyama vya siasa, Serikali na Tume wakati wa kampeni za uchaguzi na uchaguzi na utaratibu wa utekelezaji wake.

Amesema kifungu hicho kinaelekeza kuwa kanuni za maadili zitasainiwa na kila chama cha siasa, kila mgombea kabla hajawasilisha fomu ya uteuzi, Serikali na Tume na zitapaswa kuzingatiwa na wahusika wote waliosaini.

Ameongeza kuwa tayari maandalizi yote muhimu yameshafanyika na mawasiliano yameshafanyika baina ya Tume, Serikali na vyama vya siasa na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasili kwa wahusika jijini Dodoma kwa ajili ya kusaini kanuni hizo za maadili kesho.

Amefafanua kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku moja tu na kwamba baada ya hapo chama ambacho hakijasaini kanuni hizo za maadili hakitapata fursa ya kusimamisha wagombea.

Katika hatua nyingine, Kailima amesema Tume inaendelea vizuri na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kwamba tayari imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kwamba maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwa awamu ya pili yanaendelea ambapo Tume inatarajiwa kutangaza ratiba ya zoezi hilo hivi karibuni.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, ambacho kinaipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili, kati ya uchaguzi mkuu mmoja uliomalizika na siku moja kabla ya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi mkuu unaofuatia.

Tayari Tume imekamilisha awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari ambao ulifanyika nchi nzima kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 hadi tarehe 25 Machi, 2025.​
 
wanasaini nini wakati wanatakiwa wawe nyumbani iundwe tume huru na sio hii ya saamia ya kisanii? yaani huyo mwanga mchakachuaji kailima anarudishwa tena hapo tume kwa kazi maalum ya kuchakachua kura ili saamia apite, ikumbukwe huyo mwanga ndio alibadilisha kura za lowassa kuwa za mwendazake yaani viceversa mzee wa watu akaonekana kashindwa, bahti nzuri woote wamesharudi kwa baba, masiisiiemu yako kwenye panic mode wameambiwa hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi wanaweweseka yaani viti havikaliki, leteni Tume huru ya kweli muone kama mtapata hata kiti cha udiwani. SHAME shit hole country
 
Watu wazima kuita tume huru ya uchaguzi ni matumizi mabaya ya akili
 
Back
Top Bottom