TUME ni chombo maalumu kinachoundwa na idadi fulani ya wajumbe kwa ajili ya kufuatilia jambo au tukio fulani kwa lengo la kutafuta ukweli fulani. Lengo la kuziunda tume ni kutaka mapendekezo yatolewayo yasaidie kurekebisha jambo au kuanzisha jambo fulani nakadharika.
Kwa wenzetu tume ikiundwa inafanya kazi yake kwa uadilifu na kutoa majibu ya uchunguzi. Katika majibu hayo huwepo MAPENDEKEZO ya nini kifanyike. Kinachofuata ni utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na tume.
Kwetu jambo hili ni tofauti. Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia tume zikiundwa lakini majibu ya tume hizi hayajatangazwa hadharani kama ambavyo uundwaji wake ulitangazwa hadharani. Kwa hiyo, hatujua majibu au
mapendekezo ya tume kadha wa kadha ambazo zimekwisha kuundwa hadi sasa. Pia tume ambazo zilifanikiwa kutoa majibu yake - mapendekezo yaliyotolewa hayajafanyiwa kazi hadi sasa. Nitatolea mfano wa Tume ya Makwetta ya mwaka 1980 alipozunguka nchi nzima ya Tanzania ili kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu lugha ya kufundishia. Majibu ya tume hiyo ni kwamba, asilimia 80 ya Watanzania walitaka Kiswahili kiwe ni lugha ya kufundishia taaluma mbalimbali katika nchi ya Tanzania. Mapendekezo ya tume ya Makweta yalikuwa ni kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu. Mapendekezo ya tume ya Makwetta hayajatekelezwa hadi sasa huu ni muongo watatu.
Kwa hiyo, kuanzia sasa yanapotokea matatizo au jambo lolote tusiunde tume tena. Kama ni mtu amefanya kosa fulani au amesababisha kosa fulani kutendeka kwa namna moja au nyingine, mtu huyu akamatwe na kushitakiwa. Polisi na vyombo vya usalama ndio wafanye kazi ya kuchunguza na kuutafuta ukweli. Mtuhumiwa akishitakiwa atajitetea mahakamani na atapata fursa ya kupinga au kukubali yanayomkabili.
Kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyompa raia wake haki ya 'kutoa maoni'...nami natoa maoni yangu au mtazamo wangu kuhusu tume hizi zinazoundwa kila siku. HAKUNA HAJA YA TUME!!!