Isike Moses
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 2,789
- 4,243
Ghana ndiyo Taifa linalo tolewa mfano wa kuwa na Demokrasia safi ya Uchaguzi wa kisiasa Africa. Hoja hii inatokana na kile kinachoelezwa kuwa uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi (EC). Kwa mujibu wa Katiba ya Ghana ya 1992 imeweka namna tume hiyo inaundwa, majukumu yake, chanzo chake cha fedha na ukomo wa wajumbe. Rais kwa kushirikisha Baraza Kuu la Nchi (Council of State) na Bunge ndiyo mamlaka zinazofanya kazi ya kuunda Tume yenye wajumbe saba (7). Baraza Kuu hilo linajumuisha wajumbe kutoka taaisisi mbalimbali binafsi, asasi za kiraia, vyama vyote vya siasa na watu binafasi. Lazima mchakato uwe wa majadiliano ya kina,kwa hiyo Rais siyo mwenye maamuzi ya mwisho ya uteuzi wa wajumbe hao.
Baada ya Tume yenye wajumbe 7 kuundwa, katiba inaeleza kinga kwa wajumbe wote kuwa; 1. Kila mjumbe akishateuliwa, hawezi kuondolewa hadi atimize umri wa miaka sabini. 2. Ikiwa mjumbe ataumwa basi chombo huru cha madaktari kitaundwa ili kuchunguza na kutoa taarifa kama anafaa kuendelea au hapana (incapacity) 3. Kama mjumbe ametenda kosa kwa mujibu wa sheria, pia chombo huru cha kimahakama kitaundwa na kutoa taarifa 4. Fedha za kuendesha shughuri za Tume hazitoki kwa huruma /hisani ya Rais bali kuna Consolidated Account ya Tume ambayo Rais hana mamlaka nayo. Hii ni akaunti ambayo sehemu ya mapato ya nchi yanaingizwa moja kwa moja kama makusanyo ya kodi n.k kama yanavyoingizwa Hazina ya Taifa (Treasure).Mishahara na gharama zingine zinatoka kwenye akaunti hiyo ya pamoja. Yani Rais hawezi kusema msiingize pesa kule au punguzeni pesa za Tume. 5. Wajumbe hawalazimishwi kutenda kwa maelekezo au shurti toka kwa mtu au chombo chochote. Yani Mfano Rais aseme 'Ole wenu mumtangaze mpinzani mshindi'! Kwao Ghana hili ni kosa na linatosha kuondoa uhalali wa matokeo ya uchaguzi.
Katika kuipa Tume uhuru na uwezo zaidi wa kiutendaji, Ghana wakaunda kamati maalumu yenye wajumbe kutoka vyama vyote vya siasa (Inter-Party Advisory Committee). Moja ya jukumu kubwa ni kufanya vikao kujadili madhaifu na kushauri Tume namna bora zaidi ya kuendesha uchaguzi. Mwaka 2012, IPAC ilishauri kuwa Tume ione umuhimu wa kuendelea kuandikisha wapiga kura hata kama kampeni tayari zimeanza,hii ilifanya raia wengi zaidi kushiriki upigaji kura.
…………………………………………..
TUME YETU
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, sura ya tatu, sehemu ya pili ibara ya 74 (1-15) inataja uwepo wa Tume ya Taifa ya uchaguzi,muundo na majukumu yake. Inaeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua wajumbe (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi Mkuu wa uchaguzi na wengine) wa Tume na ndiye mwenye mamlaka ya kutengua teuzi zao. Katiba imeweka sababu zinazoweza kutumiwa na Rais kumuondoa madarakani mjumbe/wajumbe wa Tume; Ibara ya 74 (5) inataja kuwa Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
Moja ya sifa kuu ya kuwa mjumbe wa Tume ni sharti usiwe mwanachama wa chama chochote cha siasa bali unabakiza HAKI ya kupiga kura; Ibara ndogo ya (14) inataja kuwa itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kwamba kila mmoja wao atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii. Ibara ya 15 inaendelea kueleza kuwa kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (14) watu wanaohusika na uchaguzi ni-
(a) Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(b) Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
(c) Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi,
(d) Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na watumishi wote wa Tume ya Uchaguzi,
(e) Wasimamizi wote wa Uchaguzi katika miji na wilaya zote.
NOTE: Wakurugenzi wa wilaya (DED) ndiyo wasimamizi wa shughuri za uchaguzi kwa Tanzania. Hawa ni makada wa chama cha siasa na ni wateule wa Rais wa moja kwa moja.
Tujadili…….