2070
JF-Expert Member
- May 9, 2019
- 451
- 483
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania: Tume imekamilisha uboreshwaji wa daftari la wapiga kura kwa awamu mbili, awamu ya kwanza ilianza tarehe July 20 2024 na kukamilika March 25, 2025, na awamu ya pili ilianza May 1, 2025 na kukamilika July 4, 2025. Jumla ya Idadi ya wapiga kura wapya ni Millioni saba laki sita aroubaini moja elfu mia tano tisini na mbili wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura sawa na 136.79% ya makadirio ya awali. Jumla ya wapiga kura Millioni nne laki mbili tisini moja elfu mia sita tisini na tisa wameboresha taarifa zao sawa na 98.23% ya makadirio ya awali. Wapiga kura Tisini na tisa elfu mia saba aroubaini na nne wameondolewa katika daftari kwa kupoteza sifa sawa na 16.78% ya makadirio ya awali. Wapiga kura elfu nane mia saba na tatu wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Jumla ya Vituo Idadi ya Vituo Tisini na tisa elfu mia kumi na moja vitatumika kwa kupiga kura. Vituo Tisini na saba elfu miatatu aroubaini tisa vitatumika kupiga kura Tanzania bara na vituo elfu mbili mia tano sitini na mbili vitatumika kupiga kura kwa Tanzania Zanzibar.Idadi hii ni sawa na ongezeko la 22.49% ya vituo vilivyotumika kwenye uchaguzi 2020.
Chanzo: Tume ya uchaguzi Tanzania