Tumbua Tumbua Yamgeuka Magufuli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za umma, anaandika Regina Mkonde .

Katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi – wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa kuchukua hatua.

Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.

James Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za umma.

Pia kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama serikali ya awamu ya tano inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele? au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.

Wakati akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara hiyo.

Moja kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.

“TANROADS imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.

Mbatia ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya jumla ya Shilingi 5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”

Amesema kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016 (Ukurasa wa 134 na 135).

Dosari nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.

“Utafiti unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.

Mbatia amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.

“Uamuzi wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,” amesema.

Ameitaka serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha lami.

Akizungumzia uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.

“Katika muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani inalikumbusha Bunge kwamba, kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba zipatazo 7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” amesema.

Amesema kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-

ambazo haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.

“Hivi sasa serikali inahitaji kusaka nyumba zaidi ya mara dufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni tarehe 25 April 2008,” amesema.

Mbatia amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya serikali.

“Kamati hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali. Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe nyumba hizo,” amesema.

Mbatia amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge, na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa vitendo,” amesema na kongeza;

“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”

Amesema, sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.

“Tukumbuke kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
 
huyu ambae Lugumi inampiga chenga?
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
Acha kujifanya hujui ww,,kwan Majipu anayotumbua magufuli ni yale yaliyosababishwa na serikali ip? Kama sio ya JK..
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
Kwahiyo mkuu hujaona cha kujadiri kwenye huo UZI? Aise!
 
Hoja za Chadema na UKAWA(kama ipo) ni:
1. Mkataba wa Lugumi
2. Nyumba za serikali kurudishwa
3. Kutetea waliotumbuliwa
4. Kutaka bunge live
Hoja ya nyumba za serikali ilishindwa kwenye kampeni ambapo watu walikuwa wanazungusha mikono na kudeki barabara itaweza sasa hivi?

Mwangalieni Zitto anafanya nini na muige kile afanyacho, hoja zake ni za ujenzi wa taifa na si mipasho kama yakwenu. Siku hizi kila msemaji wa kambi ya upinzani akisimama pasipo kujali ni wa wizara gani hoja ni zile zile toka msemaji wa kwanza.
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
Acha ushamba unacopy thread ili iweje..!
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
Kwa kweli kama hii ndio namna ya kujibu hoja bado tuna safari ndefu sana kama taifa. Yaani wewe huoni madudu yaliyobainishwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani kuwa yanakugharimu wewe mwenyewe, familia yako (kama unayo), na hata wazazi na ndugu zako? Hivi nani ametuloga?-kwani ni lazima tutetee tu hata kama kufanya hivyo ni kwa gharama yetu wenyewe?
 
Chadema, Huo ndio upinzani!!? Kupinga kila kitu anachofanya Rais!!?

Hacheni kumkwamisha bana. Tumuunge mkono na tupige kazi kwa pamoja.
 
DHANA ya utumbuaji majipu sasa imemgeukia Rais John Magufuli kutokana na kuongoza wizara iliyotawala na ubadhirifu wa fedha za umma, anaandika Regina Mkonde .

Katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Dk. Magufili alikuwa Waziri wa Ujenzi – wizara ambayo inatajwa kujaa ubadhirifu wa pesa za umma na kwamba, rais huyo ameshindwa kuchukua hatua.

Kutokana na hali hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imemtaka Rais Magufuli kutumbua majipu yake wake wakati akiwa kwenye wizara hiyo.

James Mbatia, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema, katika wizara hiyo kuna ubadhilifu wa fedha za umma.

Pia kumekuwepo na utendaji mbovu wa watumishi na kwamba, serikali haina mpango wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika kutokana na kutoonesha jitihada.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inajiuliza kama serikali ya awamu ya tano inafanya kazi yake kwa haki, uadilifu, uwazi na usawa kwa wote na hasa kwa kile kinachojulikana kama utumbuaji majipu, swali hapa ni nani amfunge paka kengele? au mkuki mtamu kwa nguruwe mchungu kwa binadamu?” amehoji Mbatia.

Wakati akitoa hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani leo Bungeni mjini Dodoma kuhusu mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mbatia amefafanua baadhi ya dosari zilizofanywa na wizara hiyo.

Moja kati ya dosari hizo ni kitendo cha Wakala wa Barabara nchini TANROADS cha kuitia hasara zaidi ya Sh. 5 bilioni serikali.

“TANROADS imebainika kuwa na utendaji mbovu kama ambavyo mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) alivyobaini juu ya usimamizi mbovu katika mikataba ya ujenzi wa barabaa na madaraja ambapo ilikuwa chini ya iliyokuwa wizara ya ujenzi katika serikali ya awamu ya nne,” amesema.

Mbatia ameongeza kuwa “TANROADS wakati wa kipindi hicho, iliitia hasara serikali ya jumla ya Shilingi 5,616,652,051 kutoka kwenye riba (interest) inayoongezeka kila siku kutokana na TANROADS kuchelewa kuwalipa wakandarasi 11.”

Amesema kuwa, hasara hiyo iligundulika kati ya kipindi cha mwaka 2012 na mwaka 2015 kwa mujibu wa Ripoti ya CAG ya Hesabu za Serikali Kuu wakati wa ukaguzi wa taarifa za fedha kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2015 iliyotolewa mwezi Machi 2016 (Ukurasa wa 134 na 135).

Dosari nyingine ni ile ya serikali kuruhusu matumizi ya matairi yanayofahamika kwa jina la Super single tires ambayo yanaharibu barabara.

“Utafiti unaonesha matairi haya (super single tyres) yanaharibu barabara. Matairi haya yameanza kutumika takribani miaka mitano iliyopita na mzigo uliokuwa unabebwa na matairi 24 sasa unabebwa na matairi 12,” amesema.

Mbatia amesema, uruhusiwaji wa matumizi ya matairi hayo haukuwa wa busara kutokana na kwamba matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa barabara.

“Uamuzi wa kuruhusu matairi haya haukuwa na busara maana barabara zetu hazijabuniwa kuhimili shinikizo la uzito (excessive pressure) linalotokana na matairi hayo,” amesema.

Ameitaka serikali kuzuia mara moja matumizi ya matairi hayo ili kuzinusuru barabara lakini pia kuokoa fedha za walipa kodi zinazotumika kurekebisha mara kwa mara barabara hizo na kunyima fursa maeneo mengine kupata barabara za kiwango cha lami.

Akizungumzia uuzwaji wa nyumba za serikali Mbatia amesema, serikali iliuza nyumba zake kwa bei ya hasara hivyo kuigharimu nchi.

“Katika muktadha huo kambi Rasmi ya Upinzani inalikumbusha Bunge kwamba, kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 Serikali iliuza nyumba zipatazo 7,921 na mpaka mwaka 2008 Serikali ilikuwa imejenga nyumba 650 tu,” amesema.

Amesema kuwa, katika biashara ya kuuza nyumba zilizokuwa mali ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), serikali ilipata Sh. 252,603,000/-

ambazo haziendani na thamani halisi ya nyumba hizo.

“Hivi sasa serikali inahitaji kusaka nyumba zaidi ya mara dufu ya kiasi hicho kujenga nyumba za fidia.

Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzaji wa nyumba za serikali kinyume cha taratibu, serikali itatumia Sh. 677,606,000/- kujenga nyumba mpya ili zirejeshwe kwa Tamisemi, Rejea taarifa ya Serikali Bungeni tarehe 25 April 2008,” amesema.

Mbatia amesema, waliouziwa nyumba hizo, kuna taarifa kuwa kati yao wapo walioziuza na kujipatia faida kubwa kinyume na mikataba ya mauzo hayo,na kwamba KRUB inapendekeza wanyang’anywe nyumba hizo kwa kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Kumbukumbu za taarifa rasmi za Bunge zinaonesha kwamba, serikali ilitoa taarifa ndani ya Bunge hili kuwa, kuna kamati iliundwa kuchunguza mchakato wa mauzo ya nyumba ya serikali.

“Kamati hiyo ilitegemewa kumaliza kazi mwezi Februari, 2007, lakini hadi Bunge la Tisa na Bunge la Kumi linamaliza uhai wake hakuna taarifa iliyotolewa na serikali. Kambi Rasmi ya Upinzani Buneni inaitaka serikali ya awamu ya tano irejeshe nyumba hizo,” amesema.

Mbatia amesema, kuna maadhimio kadhaa yaliyoadhimiwa na bunge ikiwemo kuitaka serikali kurejesha nyumba zilizouzwa kinyume cha taratibu na kwa watu ambao hawakuwa watumishi wa umma.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeiitaka Serikali kutekeleza azimio hilo la Bunge, na kwa njia hiyo ile kauli mbiu ya hapa kazi tu, iweze kutafsiriwa kwa vitendo,” amesema na kongeza;

“Tunajua uuzwaji huo ulisimamiwa na Wizara aliyokuwa akiiongoza yeye na kuna uwezekano mkubwa kwamba alisimamia maamuzi ambayo hakuwa na uwezo wa kuyakiuka.”

Amesema, sasa ni muda sahihi Rais Magufuli kurekebisha kasoro alizozisimamia na katika mchakato huo ili kurejesha imani katika jamii.

“Tukumbuke kuwa Rais Kikwete alielekeza nyumba hizo zirudishwe serikalini lakini alikosa uthubutu wa kusimamia kauli yake,” amesema.
Upinzani wanatia aibu
 
Hoja za Chadema na UKAWA(kama ipo) ni:
1. Mkataba wa Lugumi
2. Nyumba za serikali kurudishwa
3. Kutetea waliotumbuliwa
4. Kutaka bunge live
Hoja ya nyumba za serikali ilishindwa kwenye kampeni ambapo watu walikuwa wanazungusha mikono na kudeki barabara itaweza sasa hivi?

Mwangalieni Zitto anafanya nini na muige kile afanyacho, hoja zake ni za ujenzi wa taifa na si mipasho kama yakwenu. Siku hizi kila msemaji wa kambi ya upinzani akisimama pasipo kujali ni wa wizara gani hoja ni zile zile toka msemaji wa kwanza.
Hivi unajitambua kweli? Hoja ya nyumba za serikali ilishindwaje kwenye kampeni wakati kuna azimio la Bunge kuhusu jambo hilo! Mawazo yako yako kwenye kampeni tu hata hujui hoja iliyoletwa ni kutekeleza azimio la Bunge kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali? Unafaidika nini kutetea uozo wakati sasa tunalazimika kutumia fedha ambazo zingesaidia hata elimu ya watoto wetu kujenga nyumba nyingine tena za serikali kwa gharama ambayo inazidi fedha zilizopatikana baada ya kuuza hizo nyumba!
 
Waziri ni mtu mdoogo sana mbele ya rais kwa mujibu wa katiba waziri anazungukwa na watu waliochaguliwa na rais kama wewe ukiwawajibisha sanasana utaitwa mmbeya na mnoko maana bilashaka huyo rais anamaslah nao-hivi mtu mdogo airport anapata nguvu wapi kumdanganya rais si dharau hizo-hivyo na Magufuli alipata kuwa waziri mnoko au mmesahau jamani
 
Yaani sasa hivi umpinzani wanajitekenya na serikali iliyopita ya jk, mko nyuma ya wakati jamani gari liko mbali, naona magufuli anawatumulia vumbi tuuuu, mmejisahau kuwa tuko awamu ya tano ya uwajibikaji(hapa kazi (quality, reliability, creativity, high performance, deliverence),
ina tija? Au ni sawa na pambio la kumbembeleza malaika alale? Tangu ianze kuhubiriwa imetoa majawabu ya shida zenu? Kwa kiwango gani? Nitashangaa ukiutanguliza uchanga yaani muda wa serikali hii toka ijitawaze kwani hata mkulima huyaona mavuno mengi pale miche aliyoiotesha pindi ichipuapo. Sio vibaya akajitoa boriti badala ya kuhangaika na vijibanzi!
 
Back
Top Bottom