Hatimaye mmiliki wa kampuni ya Dowans amejitokeza hadharani kuja kudai chake!!
Kimsingi mpaka sasa naamini huyu ndiye mmiliki wa Dowans. Kama kuna mtu ambaye ana vielelezo/maelezo tofauti na maelezo ya Al Adawi avitoe. Hili jambo ni lakisheria na kama tutaendeleza siasa na ushabiki ni wazi kuwa tutajiingiza kwenye matatizo makubwa. kama ambavyo bwana Adawi ametahadharisha wakati anaongea na waandishi wa habari. Hukumu ya ICC iko wazi na nilichogundua mimi ni udhaifu na uzembe wa viongozi wetu kuingia mikataba kichwakichwa baadaye wanakuja kuikana kupitia mlango wa siasa. maelezo ya bwana Adawi yalikuwa wazi na sikuona kuwa kuna swali lililomtatiza kulijibu, aidha bwana Adawi amesha tahadharisha kuwa hatavumilia tena kuona mtu yeyote ana chafua jina la kampuni yake na ametishia kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote atakaye jaribu kuchafua jina la kampuni yake.
Pamoja na maelezo hayo lawama kubwa nawatupia viongozi wetu kwa kutuficha ukweli, Bwana Al Adawi ameeleza bayana kuwa Rostam ndiye aliyemuomba aje awekeze hapa Tanzania sitaki kuamini kuwa kwa ukaribu wa Rostam na viongozi wa juu haiwezekani kutowaambia mmiliki wa Dowans, mara zote viongozi tunaowaamini walikataa katakata kutomjua mtu huyu, sijui kama kulikuwa na haja ya kumficha mtu huyu, hiyo dhambi hapa siioni, usiri huu ndiyo umetufikisha hapa tulipo, sasa mmiliki kajitokeza na kakiri wazi kuwa yeye ndiye mmiliki aidha ameeleza wazi kuwa mkataba wa tanesco na Dowans kwa pamoja walikubaliana kuondoa kifungu cha kukata rufaa inapotokea mmoja kashidwa, bado hayo ni mambo ambayo watanzania hawaambiwi na tanesco wamefunga mdomo wakati watanzania wenye upofu katika jambo hili wakitimua mbio mahakamani, nafikiri kuna hali ya kutupiana lawama kati ya tanesco na serikali, naamini kuna kutakiana mabaya hapa kati ya tanesco na serikali bila kujali aibu na madhara yatakayotupata badaaye, haya ni masikitiko makubwa sana!!! ila yote ni yote mmiliki kaja tusianze tena hadithi tutakuwa tunazidi kujichimbia shimo kama kuna muafaka wowote tuutafute ili tusije itwa tanzania tunaukorofi katika biashara!!! ''katika hizo bilioni 94 tunazodaiwa ndani yake kuna deni linalofikia kiasi cha bilioni 25 ambazo ni malipo halali wanayodaiwa tanesco na Dowans baada ya kuuza umeme wao kwa wateja. Watanzania tuwe makini sana katika jambo hili ambalo lina sintofajamu nyingi. Nionavyo uhalali wa mmiliki wa Dowans sio muhimu sana kwetu watanzania kitu cha muhimu ni kuhakikisha kuwa tatizo kama hili halitokei tena!!! Kama ni uzembe tumeufanya sisi wenyewe tumalizane na Al Adawi ili tujenge nchi yetu, maana kutokana na hukumu ya ICC hatuna pa kukimbilia lazima pesa ya watu ilipwe iwe tunataka au hatutaki.