Tumalizane na Mmiliki wa Dowans uzembe ulikuwa wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumalizane na Mmiliki wa Dowans uzembe ulikuwa wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Feb 21, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hatimaye mmiliki wa kampuni ya Dowans amejitokeza hadharani kuja kudai chake!!
  Kimsingi mpaka sasa naamini huyu ndiye mmiliki wa Dowans. Kama kuna mtu ambaye ana vielelezo/maelezo tofauti na maelezo ya Al Adawi avitoe. Hili jambo ni lakisheria na kama tutaendeleza siasa na ushabiki ni wazi kuwa tutajiingiza kwenye matatizo makubwa. kama ambavyo bwana Adawi ametahadharisha wakati anaongea na waandishi wa habari. Hukumu ya ICC iko wazi na nilichogundua mimi ni udhaifu na uzembe wa viongozi wetu kuingia mikataba kichwakichwa baadaye wanakuja kuikana kupitia mlango wa siasa. maelezo ya bwana Adawi yalikuwa wazi na sikuona kuwa kuna swali lililomtatiza kulijibu, aidha bwana Adawi amesha tahadharisha kuwa hatavumilia tena kuona mtu yeyote ana chafua jina la kampuni yake na ametishia kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote atakaye jaribu kuchafua jina la kampuni yake.
  Pamoja na maelezo hayo lawama kubwa nawatupia viongozi wetu kwa kutuficha ukweli, Bwana Al Adawi ameeleza bayana kuwa Rostam ndiye aliyemuomba aje awekeze hapa Tanzania sitaki kuamini kuwa kwa ukaribu wa Rostam na viongozi wa juu haiwezekani kutowaambia mmiliki wa Dowans, mara zote viongozi tunaowaamini walikataa katakata kutomjua mtu huyu, sijui kama kulikuwa na haja ya kumficha mtu huyu, hiyo dhambi hapa siioni, usiri huu ndiyo umetufikisha hapa tulipo, sasa mmiliki kajitokeza na kakiri wazi kuwa yeye ndiye mmiliki aidha ameeleza wazi kuwa mkataba wa tanesco na Dowans kwa pamoja walikubaliana kuondoa kifungu cha kukata rufaa inapotokea mmoja kashidwa, bado hayo ni mambo ambayo watanzania hawaambiwi na tanesco wamefunga mdomo wakati watanzania wenye upofu katika jambo hili wakitimua mbio mahakamani, nafikiri kuna hali ya kutupiana lawama kati ya tanesco na serikali, naamini kuna kutakiana mabaya hapa kati ya tanesco na serikali bila kujali aibu na madhara yatakayotupata badaaye, haya ni masikitiko makubwa sana!!! ila yote ni yote mmiliki kaja tusianze tena hadithi tutakuwa tunazidi kujichimbia shimo kama kuna muafaka wowote tuutafute ili tusije itwa tanzania tunaukorofi katika biashara!!! ''katika hizo bilioni 94 tunazodaiwa ndani yake kuna deni linalofikia kiasi cha bilioni 25 ambazo ni malipo halali wanayodaiwa tanesco na Dowans baada ya kuuza umeme wao kwa wateja. Watanzania tuwe makini sana katika jambo hili ambalo lina sintofajamu nyingi. Nionavyo uhalali wa mmiliki wa Dowans sio muhimu sana kwetu watanzania kitu cha muhimu ni kuhakikisha kuwa tatizo kama hili halitokei tena!!! Kama ni uzembe tumeufanya sisi wenyewe tumalizane na Al Adawi ili tujenge nchi yetu, maana kutokana na hukumu ya ICC hatuna pa kukimbilia lazima pesa ya watu ilipwe iwe tunataka au hatutaki.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Mkuu ongeza font wengi wetu mboga kuu ni maharage!!!
   
 3. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Anold uzembe ulikuwa wa kwako na mafisadi wenzako.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu katumwa. Kadri siku zinavyopita tutawaona wengi watakaokuja kwa ngozi ya kondoo kumbe ni fisi,
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Dear Anold

  Wewe umesema ukweli (ingawa) mchungu ambao watanzania hatutaki kuusikia na ambao "watawala" wetu hawataki kutuambia. Ukweli ni kwamba mkataba kati ya TANESCO na DOWNS ulikuwa wa kifisadi na tangia mwanzo ulisukwa ili wanjanja wachache wachote hayo mapesa. JK alikuwa anamfahamu mmiliki wa DOWNS, RA analikuwa akimfahamu, Ngeleja naye pia. Mwisho wake walifahamu kwamba DOWNS lazima DOWNS ichote hayo mabilioni. The writting was already on the wall.

  Kampuni ya REX iliyoshauri kuvunja mkataba ilikuwepo strategically kwasababu ilitaka DOWNS walipwe hizo pesa.

  Hukumu imeshatolewa na ICC hakuna longolongo lazima pesa hizo zilipwe kwani ndivyo tulivyo saini mkataba kifisadi. Tunavyozidi kuchelewa kulipa kila mwezi tunatozwa riba ya 7% ya denil la mwezi. 7% x 94bilioni = 6.5 bilioni. Hivyo mwezi utakaofuata tutalipa riba ya 7% x 100.5 Bilioni. = 7.04 bilioni. Maana yake kama tutachelewa kulipa at least kwa miezi miwili tu tutalipa jumla ya Tsh 107.7 bilion (lucrative bussiness eeh). Tukishindwa mali zetu zilizoko nje balozi nk zitakamatwa na kupigwa mnada wenzetu hawana masihala na sheria hata kama ulijinyonga mwenyewe kafie mbali na upuuzi wako.

  Ukweli ni kwamba hili deni halikwepeki, mkenge tuliingia wenyewe. Tatizo kubwa ni kwamba wale wote waliongia mkataba huu wa kifisadi wachukuliwe hatua kwa mjibu wa sheria za nchi. Lakini JK hawezi kufanya hivyo kwasababu na yeye ni mojawapo wa genge hili, We're dummed tulipe tu kwani tunayataka wenyewe.
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu una uhakika gani kuwa huyu ndiye mmiliki halali?
  Kama yeye ndiye mmiliki halali kwa nini akatae kupigwa picha? Kuna kitu hapa.
  Mbona katika majina tuliyotajiwa na Ngeleja la huyu bwana halikuwemo? Huoni kama kuna kitu hapo?
  Suala hili tusilichukulie kirahisi kama utakavyo..!
   
 7. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  RA amekuja kivingine, all what Al hadawi amesema yaliandaliwa toka mwanzo na RA, so mimi bado siamini katika alichosema huyo mwarabu mwizi! All these are RA doings! kweli jamaa amedhamilia kuikamua hii nchi kwa faida yake na kizazi chake!
   
 8. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Interest in Kwa mwaka hivyo basi hiyo 6.5 Mill gawanya kwa 12 upate kwa mwezi. Usitutishe.
   
 9. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Nimekua nikisema sana wabongo kwa kuongea hatujambo.SHERIA HAIJUI MAMBO YA SIASA.
  Nilisema mwanzo jk ana tabia ya kukaa kimya na kuacha watu waongee tani yao.KIKO WAPI SASA tajiri ndo huyo katia timu,bado mazezeta wanang'ang'ania rostam.chuki za kipuuzi hazitufikishi popote YOU WAIT AND SEE
   
 10. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,928
  Likes Received: 1,033
  Trophy Points: 280
  Tena kama ametumwa, akawaambie mafisadi wenzake kuwa hawakubali mpaka pachimbike hapa.
   
 11. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,928
  Likes Received: 1,033
  Trophy Points: 280
  Hivi wee kajamaa una mauchungu na nchi kweli!!!!!!!!!!!!!!!????????????????
  Na wewe nikikukamata ni:frusty: kibano tu.
   
 12. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #12
  Feb 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wadanganyika Mpo :)
  mtambo wa Dowans umewashwa leo mchana,baada ya ule wa songas kupata moto,bado mnabisha tu.kumbuka kuwa uchaguzi wa mwaka huu umetumia pesa nyingi sana,Chama Tawala hakina miradi mikubwa ya kusupport kampeni kubwa kama hyo,so pesa zimetoka wapi?
  its over the Fat lady has sang . mwarabu amekuja ,Mh.Dakata ameondoka kushughulikia maswala ya uchakachuaji wa ivory cost.
  sasa mwenye akili ajiulize.
  1-hakujua kuwa mwenye Dowans Anakuja kuongea na Tanesco?
  2-Mazishi ya gongolamboto na mabomu hayajakamilika
  3-Kipi ni bora kwa taifa hili kwenda Kuandaa ujumbe wa Ivory Cost au kusimamia mjadala wa Dowans and Mabomu ya Gongo la Mboto
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Are lawyers not governed by professional ethics? Can Tanganyika Law Society investigate the role of this firm in relation to TShs. 94 million and take disciplinary measures if REX acted against ethics?
   
 14. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  mitambo hiyo inatakiwa kutifshwa na huyo mwarabu kupigwa pi baada ya kualala segerea siku 7 kwa kutuletea mchezo ndani ya nchi yetu
   
 15. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Hahaaa ama kweli mazumbukuku wako wengi nchi hii.Tanzania tunataka umeme FULL STOP.it doesnt matter umetoka wapi.kama kuna wajanja humu wanapata loophole ya kumake money so be it.provided kwamba hawatuuzii umeme HEWA
   
 16. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Hahaaa ama kweli mazumbukuku wako wengi nchi hii.Tanzania tunataka umeme FULL STOP.it doesnt matter umetoka wapi.kama kuna wajanja humu wanapata loophole ya kumake money so be it.provided kwamba hawatuuzii umeme HEWA
   
 17. s

  salisalum JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Utafiti wa taasisi ya UWEZO (Uwezo.net) inaonyesha kuwa watoto 3 kati ya 10 wanaomaliza Darasa la saba hawawezi kufanya hesabu za darasa la pili. Aliyetupa mahesabu ya riba hapo juu huenda akawa miongoni mwa hawa watatu waliomaliza darasa la saba bila kuwa na uwezo wa kufanya hata hesabu za darasa la pili. Wanatupa shida sana kwenye ulimwengu wa kazi. Unakuta mtu anabwabwaja maneno mengi ukimwambia jambo la hesabu tu kidogo anakimbilia, oh mimi sikusoma hesabu. Hesabu ni za lazima kwa kila mtu japo hizi za mabano, Gawanya, Zidisha, Jumlisha na Toa (MAGAZIJUTO).

  Hebu sote tujaribu haka kaswali: Baba Juma alirudi nyumbani na ndizi moja. Aliwakuta watoto wake wanne Juma, Gati, Yona na Seki wakimsubiri kwa hamu. Kwa upendo wake kwa watoto wote akakata ndizi hiyo na kuwagawia vipande vinne vilivyo sawa. Watato watatu wakubwa yaani Juma, Gati, na Yona walimpenda sana mdogo wao Seki wakaamua kumgawia tena sehemu ya vipande vyao. Juma akampa nusu ya kipande chake, Gati akampa robo ya kipande chake, na yona akampa sehemu ya tatu ya kipande chake.

  Swali: Je mtoto mdogo Seki alipata asilimia ngapi ya ndizi yote?

  Kidokezo: Uli uweze kufanya swali hili kirahisi dhania (assume) Seki ni Rostam na Juma, Gati na Yona ni wapiga kura wote wa Igunga, na Baba Juma ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Watanzania (siyo Wa-Tanzania).

  Watakaojibu hilo sawa nitaandaa mkutano nao tujadili swala la Dowans kwa upana zaidi. Na tuta-share minutes kwa wana JF wote.
   
 18. S

  Sinamatata Member

  #18
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana bw. Jatropha kwa kupendekeza huyu mwarabu kuwekwa Segerea. Nafikiri hili liko sahihi, lakini je sheria inasemaje. Na ninani ataamua wakati Bw. Safari tayari huko Ivory Coast!
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Hahaaa ama kweli mazumbukuku wako wengi nchi hii.Tanzania tunataka umeme FULL STOP.it doesnt matter umetoka wapi.kama kuna wajanja humu wanapata loophole ya kumake money so be it.provided kwamba hawatuuzii umeme HEWA
   
 20. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mwarabu huyo
   
Loading...