Ukimpenda mtu hautakubali kuharibu maisha take ya baadae, hautamuacha akajihusisha na mambo yanayoharibu au kuchangia kuharibu tabia njema.
Mfano, toka nilipokua shule nilidhamiria kutokujihusisha na mapenzi ya aina yeyote kabla ya ndoa, nikiamini kwamba yeyote ntakaemfanyia hivyo ni kuharibu future yake kwa vile sikua tayari kuoa kwa wakati huo.
Hautakubali kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya kwa vile zinaharibu vijana wetu na taifa kwa ujumla.
Hautajihusisha na ufisadi na rushwa kwa sababu utawakosesha watu haki zao stahiki.
Lakini ili kuyaweza haya yote, hofu ya Mungu inahitajika sana.
Tumaini language liko kwa Mungu pekee, na nna amino kwamba nilikuja duniani bila chochote na ntaondoka nikiwa sina kitu. Haina haja ya kuchukia watu au kuwasababishia matatizo wengine.
Kuwa na Amani na watu wote ni vigumu sana, lakini inawezekana.
Tupende familia zetu na kuwajali wengine, hapo ndipo tutakapokua na Amani na furaha ya kweli na inayodumu.