Tulivyokuwa tukiiba almasi mgodi wa Mwadui na wenzetu kuuawa

mkuu barafu katikati ya miaka ya 90 kulikuwa na mbeshi mmoja alikuwa maarufu sana inasemekana aliua mbwa wa mwadui kwa kumchana mdomo alikuwa anaishi kama si idukilo basi utemini alikuwa mfupi na ananguvu sana unaweza nikumbusha jina lake
 
nakumbuka sana kawawa kwa kamanda jirani na idara ya shamba kwenye matunda na manguruweni kama unaenda dairy farm kwa mzee mwaipaja kuelekea air port jirana na chuo cha kilimo karibu na sanamu la williamson na mbuyu wake
Pale kwenye sanamu mlkuwa manakusanyika sikukuu kwenye ile bustani.Mkawa kama Ulaya
 
kama ntakuwa nimekosea jina mkuu barafu utanisahihisha alikuwa anaitwa BUDOYA unamkumbuka?
Daaaah!!!! dabadest umemjuaje Budoya??Naomba nisielezee sana juu ya mtu huyu,maana nina mengi sana ya hatari ya kumuelezea huyu jamaa....Nimetoka na machozi
 
nieleze kidogo khsu huyu budoya eti alikuwa anapaka mafuta ya simba ili mbwa wa mwadui wamuogope,vp ulivyopita pale maganzo daya yupo na tagi tajiri?
 
maskini mwadui kwisha habari yake imebaki story,wapi swai mikate,wapi hiporaiti moshi,wapi dkt tosiri,wapi chekingo na kabondo mapilot wetu enzi hzo,wapi mwalimu mutembei na mwalimu musa wa ts,wapi mwalimu gontako na mwalimu kachuchuru wa mwadui sec,wapi mwalimu kasoyaga wa mwadui mashariki,wapi mzee ngoromole,mzee ndaki konda wa mabasi ya mwadui,wapi idara ya shamba,wapi dairy farm,wapi golf,wapi ujamaa c,wapi posta na simu,daaah kweli mwadui ilikuwa nzuri sana,mzee wetu muhali,mzee wetu bugome,mzee kimolo,mzee kailembo dj mwakapesa,mzee hincha
Chekingo, pakata, mutembei na mwalimu kasoyaga R.I.P.
 
nieleze kidogo khsu huyu budoya eti alikuwa anapaka mafuta ya simba ili mbwa wa mwadui wamuogope,vp ulivyopita pale maganzo daya yupo na tagi tajiri?
Duuuh!!Yule mtu ni hatari sana,alikuwa na dawa hatari sana za kienyeji;sio unanukia mafuta ya Simba,bali unaonekana kama Simba na mbwa wote wanakukimbia...Ni habari nzito ambazo kwa sasa tunazihifadhi mpaka ipite walau miaka kadhaa

Kuna habari zikiaimuliwa watu hawataamini na zitazua taharuki,lkn achana na kazi ya ubeshi na kuiba almasi,ina mambo mengi sana
 
na kama atakuwa humu atanikumbuka maana alikuwa na akina china wa kawawa jkt mafinga ambao sisi tuliwaleta wachezaji wetu na gari la jeshi na nikawa karibu nae kupiga story za mwadui na baba yake chekingo na chambuso ambaye ni baba wa rajabu chambuso aliyekuwa mwongoza ndege za mwadui mzee chambuso
 
ni kweli mzee wa beba dunia(barafu) vitu vingine watu hawataamini na itakuwa ngumu kuwaelewesha khs kuiba almasi,ni kitu ngumu sana inahitaji ujasiri na laiti tungejua kuwa vibarua wa mchana ndo hao wabeshi wa usiku tusinge waruhusu kufanya vibarua ndani ya mgodi
 
na ngoma za wasukuma(mbina) zilivyochangia kuwafanya wabeshi kujiamini kuhusu uchawi na kuiba,maana mamanju wengi walikuwa wanaamini uchawi na wateja wao wengi walikuwa wabeshi,mamanju kama tagala,inagha nk,walikuwa noma kwa mbina
 
hapoMkuu kwenye kulinda nguzo za umeme umeme umenikumbusha mbali sana..tulikuwa tunalinda zamu ya masaa mawili mawili kila bweni, shy bush ikiwa na mabweni matano.. kipindi hicho nipo bweni la , mh. D. Kafulilaa akiwa bweni la tembo.. tukitoka kulinda nguzo tunashuhudia mioto ya wachawi wa utemini wakicheza live kwenye viwanja vya shule...aisee kweli walisema kuwa uyaone
wakinga wanaita vipembe
 
Mkuu huyu alikuwa Meneja,alitusumbua sana kwa kuunda Kikosi cha mbwa na Farasi waliokuwa wanapata mafunzo toka Nje ya nchi.Baada ya Ubaguzi wa rangi kuisha,wale mbwa wakawa wanaletwa toka South Africa,ile "specie" ya mbwa waliokuwa wanatumika kuuwa watu weusi wakati wa maandamano ya ubaguzi wa rangi S.Africa.

Wale mbwa ndio waliletwa wakiwa na mafunzo makari sana na walikuwa mbwa katiri sana sana.Jamaa zetu wengi walikufa kwa kuumwa na wale mbwa.Ninamkumbuka huyo Meneja akiitwa Sylivester Mipawa.Kumbe sasa ni diwani?Duuuh.... kituli one mpe salamu anko wako mzee wa benzi
Mzee alikua na benz yake matata na alikua ananyoa way flani hivi amazing...kawa diwani? Kweli maisha hayana adabu kutoka mining manager mpk diwani ...duh
 
Dah, pole sana mkuu kwa msoto wa maisha, ama kwa hakika story yako imenivutia sana, imenipa somo kubwa sana la kujifunza japo ni story inayotisha inatia huruma na pia inasisimua kwa kuwa in true story, pole sana mkuu.
Umejichanganya na maelezo yangu, kutoka kwenye maelezo yako, hapo ndipo aliishi mwl kachuchuru mwanzoni. Baada ya hapo Kuna nyumba nyingine alihamia maaneo ya na pale alipoishi mwanzoni. Mimi sio mtoto wa Gordon ndugu.
 
Mzee alikua na benz yake matata na alikua ananyoa way flani hivi amazing...kawa diwani? Kweli maisha hayana adabu kutoka mining manager mpk diwani ...duh
Na bila shaka atakuwa diwani wa chama dola
 
Back
Top Bottom