Mgodi wa Gukona umekuwa ni msiba kwa wakazi wanaozunguka mgodi huo

Sesimba

Senior Member
Dec 20, 2016
189
382
Mnamo tarehe 17 Desemba 2023 Majira ya saa 10 jioni Kijana Ryoba Kisire Kisire alipigwa Risasi na Polisi wanalinda eneo la mgodi huo na Kufariki wakati akipatiwa matibabu hospital ya Nyamwaga Halmashauri ya Tarime Vijijini.

Mazishi yanafanyika leo tarehe 18 Desemba Kitongoji cha Ntarechagini, Kijiji cha Komarera Kata ya Nyamwaga. Aidha Kijana mwingine Anajulikana kwa Jina la Jastin Marwa alipigwa risasi mkononi ambaye hali yake inaendelea vizuri.

Wanajukwaa nimeandika hapa baada ya kuwepo kwa vifo zaidi ya 6 toka nimefika hapa kwa shughuli zangu za kibiashara.

Ukweli ni kwamba, vijana wengi kwa asilimia 100 wanategemea mabaki ya kwenye mdogi huo. Sasa kuna watu ambao wamejimilikisha hayo maeneo na wananufaika kwa hiyo wanawakataza vijana kwenda kuokota mawe ambayo ni masalia yaliyoachwa na mitambo ya Mzungu.

Kwanini nimeandika hapa? Ninaandika hapa kwa sababu kwa kweli kama hakutakuwa na mkakati juu ya jambo hili vijana watakwisha. Hapo ndiyo wamefanya iwe sehemu ya ujira wao kwa kuwa hakuna ajira. Ukweli pia ni kwamba wanakataliwa na kampuni za ulinzi wa mgodi huo sababu ni kwamba wanaogopa kuibiwa mitambo siyo mabaki ya mawe. jambo ambalo linawafanya wawe wanavamia.

Sasa nimekuwa na maswali kadhaa:

1. Sawa tufanye intruders wanavamia na kuiba mabaki, Je ndiyo wanatakiwa kuuawa?
2. Kama mabaki ya mawe hayo mzungu hana kazi nayo kwanini uongozi wa mgodi wasikae pamoja na wanavijiji na Viongozi wao wakubaliane ikibidi hata kuweka siku maalumu za kufanya hivyo ili kuepusha mauaji haya?
3. Hivi wakitokea wakajikusanya vijana wote na kuamua kufanya uharibifu watakuwa wamesababishwa na nani kama siyo hawa polisi?

Wanajukwaa nadhani muhimu sana kuyajadili haya na kutoa mapendkezo ya nini kifanyike.

Asante
 
Vijana wanaouwawa ni wezi kama wezi wengine hawana ruhusa ya kufanya wanachofanya. Tusitetee upumbavu....hata ningekuwa mimi ndio mlinzi siwezi waruhusu waingie kwenye lindo langu kama chooni..chuma chuma tu iwe fundisho kwa ndugu jamaa na marafiki
 
Wewe utakua muislam na mfuasi kindakindaki wa Hammas
 
Eneo limeshazuiwa na mamlaka kwa mtutu wa bunduki,kwanini unalazimisha kujihusisha nalo??

Matatizo mengine yanayowapata watu yana uhusiano mkubwa sana na upumbavu walio nao.

Serikali ya ccm hakuna asiyeijua kama iko tayari kukuua muda wowote,kukaza kwako ni kujitafutia ushujaa bandia.
 
Back
Top Bottom