Tulivyokuwa tukiiba almasi mgodi wa Mwadui na wenzetu kuuawa

Sisi ndio tulikuwa tunaishi pale kabla kachuchuru hajahamia.
Kabla ya mwl Kachuchuru ile nyumba aliishi mzee Gordon labda utakua we ni mtoto wake... watu mwadui sio tumeishi tu bali tumezaliwa na kukulia pale... kiboko ya wabeshi alikua marehemu mzee Kirahi Oguma alikua polisi chini ya kamanda mzee Mbelwa, enzi hizo Mwadui kweli mwadui miaka ya 80 kurudi nyuma.
 
Dah, pole sana mkuu kwa msoto wa maisha, ama kwa hakika story yako imenivutia sana, imenipa somo kubwa sana la kujifunza japo ni story inayotisha inatia huruma na pia inasisimua kwa kuwa in true story, pole sana mkuu.
 
Du yaani una nikumbusha mwadui ni sehemu niliyokulia kwa kweli maisha ya mgodini miaka hiyi ya 80 ni Kama vile uko ulaya kumbe nyie ndio mlikuwa wezi du poleni Mara mlijigeuza fisi
Aaaa nyie watoto wa mgodini mlikuwa mnakula raha sana;na mlijisahau mkadhani mtaishi mle milele.Duka kubwa unakutana na nyama za kutoka Daily Farm na mikate,maziwa ya token mlangoni,ukitembelea recreation club ndio balaa...hizi mambo ndio zilitupa hasira sana tuliokaa kandokando ya mgodi mpaka tukawa tunavamia kuiba.

Utakuwa mtoto wa Boidi ya Juu au ya Chini?Au Alamasi Road?
 
Kabla ya mwl Kachuchuru ile nyumba aliishi mzee Gordon labda utakua we ni mtoto wake... watu mwadui sio tumeishi tu bali tumezaliwa na kukulia pale... kiboko ya wabeshi alikua marehemu mzee Kirahi Oguma alikua polisi chini ya kamanda mzee Mbelwa, enzi hizo Mwadui kweli mwadui miaka ya 80 kurudi nyuma.
Kulikuwa na kikosi hatari sana cha mbwa na farasi,na walikuwa wakifanyia mazoezi kule Line Polisi kama unaelekea kijiji cha Utemini,kweli Mwadui ilikuwa kama Ulaya.

Maziwa kedekede,nyama za kutosha na mabasi ya kuzunguka ndani ya mgodi,toka Kampaundi mpaka Alamasi Road.Kuna boss alikuwa anaitwa Mipawa,huyu aliunda kikosi hatari sana cha mbwa na farasi;walitusumbua sana hasa njia yetu ya kupitia Songwa,Bwawani mpaka Mgodini.

Mkuu ww wa TS,Mwaseco au Agriculture?Umenikumbusha mbali,team ya mpira na marefa kina Mzee Mshangama sisi tukija kushangaa mpira kupitia geti kubwa kwa ruhusa maalumu,halafu jioni tunarudi kama wabeshi.Kweli maisha ni safari ndefu
 
Naamini story zetu wengine tukizimwaga wengi wenu mtaona ni kufikirika. Kwa miaka ya 90 Magazo usipime kabisa na wafanya magendo wengi walikuwa ni waarabu. Maisha we acha tu, mfano unaweza kuamini kuwa Magu alianza kupiga kampeni nyumba hadi nyumba enzi hizo kwa kutumia baskeli (kama anavyoitaga Mr Nice) maana hata uwezo wa kuwa na pikipiki suzuki za enzi hizo hakuwa nazo ila sasa angalia alivyo mkuu wa nchi na anaheshimika kwa kila mtu. Watu tumetoka mbali hata wengine hatukutegemea kujiunga JF
Longo
 
Hii ilikuwa ni miaka ya '90 mwanzoni, tukitokea pembezoni mwa mgodi wa Mwadui, tulifahamika kwa jina la "Wabeshi".

Zana zetu za kazi ilikuwa ni sululu, chepe na majembe yaliyonolewa sana, tulikabiliana na jeshi la polisi la mgodi wa Mwadui waliokuwa na kikosi cha farasi na mbwa wenye uweredi mkubwa sana na mafunzo ya hali ya juu.

Nakumbuka siku rafiki zangu wawili walivyouwawa kwa kuumwa na mbwa sehemu za siri na jirani yangu Jilingumika Masufulia alivyopigwa risasi ya kichwa akivuka fensi ya mgodi wa Mwadui.

Almasi tuliibatiza jina la "ng'ana", na ilikuwa hauwezi kwenda kuiba bila kuchanjwa chale za kwapani na matakoni. Mganga wetu mkubwa alikuwa ni Mzee maarufu sana wa Kijiji cha MWIGUMBI, Nje kidogo ya mgodi, huyu ndio mzee aliyetupa dawa na kinga wakati wa kwenda kuiba almasi,wakati huo nikiwa na miaka kama 16 tu hivi, nimemaliza darasa la saba shule ya msingi Luhumbo. Tajiri wetu mkubwa alikuwa mwarabu wa Maganzo maarufu kwa jina la Abeid, huyu alitupikia vitumbua na chai kabla ya kwenda mgodini kuiba almasi, na chote tulichokipata tulipeleka kwake kama tajili na kupata ujira wetu.

Tajiri Abeid hakuwa mtu "rahisi rahisi", yeye mganga wake alikuwa anatokea kijiji cha Idukilo, mganga hatari sana aliyekuwa na madawa ya kisukuma ambayo yaliwabadilisha watu na kuwa mbwa mwitu au nyani pindi walipoingia ndani ya mgodi kuiba, tajiri Abeid alikuwa anaishi kijiji cha Maganzo, akiwa na duka la bidhaa la kuzugia,lakini deal zake kubwa ilikuwa ni kununua almasi na kuziuza kwa matajili wakubwa wa Mwanza na Shinyanga mjini.

Almasi zote tulizopeleka kwa Abaeid zilikuwa zinatunzwa na mbuzi dume, beberu mkubwa aliyekuwa anazimeza na kuzihifadhi tumboni hadi mteja atakapokuja,hata polisi wakifika na ku-search vipi,wasiongeziona almasi kwani beberu alikuwanazo tumboni,hakuwa beberu wa kawaida maana alikuwa na chumba chake na alilala ktk godoro. Mbuzi hakula nyasi wala majani ya miti, bali vitumbua, chai, ugali na "maparage". Kipindi hicho hatukuwa na ruhusa ya kuongea juu ya mbuzi yule, tulimuogopa na kumtii zaidi hata ya kiongozi wa msafara wa wabeshi.

Tajiri wa uhakika alikuwa Fantomu wa maeneo ya Mipa,huyu hakuonana na sisi wabeshi maana tulikuwa watu "wadogo" sana, bali alipitia kwa Abeid na waarabu wengine wa Maganzo.

Maisha ya kuwa "mbeshi" yalikuwa magumu sana,maana kifo na kujeruhiwa ilikuwa ni njenje,tuliuwa na kuuwawa. Polisi, mbwa na farasi waliokuja bila tahadhari waliuwawa kwa chepe zilizonolewa na mapanga. Tukio moja nalokumbuka ni la mwenzetu Masunga kumuua mbwa wa polisi kwa kumkata na chepe mdomoni na kuutenganisha mdomo pande mbili.

Wenzetu wengi walikufa tukiwa bwawani tukiiba,wengi walizama kwenye tope liliotokana na mabaki ya kusafishwa kwa almasi ambayo sisi tulikuwa tunakwenda kuchota na kuchekecha upya,bwawa hili la tope zito lilukuwa karibu na "sorting area" ambayo ililindwa kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kwa imani ya chale za mganga wa MWIGUMBI na Idukilo watu wengi tulikuwa na ujasiri wa kukatiza kila mahali bila hofu.

Wengi waliojeruhiwa na kuumizwa walilazwa ktk hospitali ya Mwadui.Siku nilipoamua kuacha "kazi" hii na kurudi shule,ilikuwa ni siku hatari sana... binamu yangu kipenzi Luhende alipigwa risasi ya kichwa na ubongo kutawanyika, mbele ya macho yangu Luhende alikufa bila hata kuomba maji. Askari wakiwa umbali wa kama mita 100,sisi tukiwa na makarai yetu na chekecheke tukiambaaambaa pembeni ya reli maeneo ya SONGWA ktk njia ya mzunguko kuelekea Maganzo tuliwekwa katikati yao na kuuliwa baadhi yetu. Katika kundi la wabeshi kumi, saba walikufa hapo hapo..watatu walifia hospitali na mimi pekee nilipona baada ya kujitumbukiza kwenye bwawa la maji ya kunywea mifugo, niliogolea chinichini kwa chini na kuibukia upande wa matete, ambapo nilikaa ndani ya maji zaidi ya masaa 12 bila kutoka..nikiwa nimetoa pua tu na kujishikiza kwenye "msitu" wa matete.

Kikosi cha polisi wenye mbwa na farasi walizingira bwawa lile mpaka usiku wa kiza kinene, wakaamini nimeshakufa na kuzama hivyo wangefika kesho yake kukuta ninaelea baadaya kufa.Katikati ya kadhia ile ndipo nilpoona kazi ya ubeshi si lolote si chochote, zaidi ya mwili kujaa chale za tako mpaka kwapani.

Pesa tuliyopata ilishia mnadani Maganzo,ambapo tulikula na kunywa. Hatimaye niliamua kurudi kijijini Luhumbo,nikakariri tena darasa la saba kwa jina la mtoto wa mjomba aliyeacha shule na kwenda kuchunga na kulima vibarua maeneo ya Muhunze. Nilikuwa mkubwa kuliko wote darasani lakini sikukata tamaa. Nilisoma kwa mwaka mmoja wa darasa la saba kwa bidii na usongo na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na shule ya Tabora Wavulana.

Kwa mara ya kwanza napanda train kwa "warrant" ya serikali, station ndogo ya Songwa kupitia Shinyanga kuelekea Tabora. Nakutana na Afande Chacha kwenye geti la Tabora boys, ananipokea kwa kichurachura na bakora za mgongo bila sababu, wakati huo Tabora Wavulana ipo chini ya jeshi. Mwanzo naona maisha ya ubeshi ni afadhali kuliko shule ya aina hii..mchakamchaka na Afande Chacha kila asubuhi kupitia Kwihala mpaka Kipalapala.Juma la kwanza natamani kutoroka lakini sijui mahali pa kuelekea, shule ipo nje ya mji na mfukoni sina nauli.Baada ya mwezi ndani ya kombati ya kijani mwanajeshi,inatangazwa disko ya "welcome form one".

Disko langu la kwanza maishani,nakutana na watu wenye lafudhi nzuri na Kiswahili kilichonyooka, mimi nashindwa kuongea mbele za watu sbb lafudhi yangu ni "ngumu" kusikika na kueleweka. Ninapata marafiki toka pande mbalimbali za Tanzania. Kapufi wa Mpanda na Mwaisengela wa Mbeya wanakuwa marafiki zangu kwenye bweni la Kimweri. Miaka minne ndani ya Tabora,wao wanaita Mboka Manyema..ninabahatika kurudishwa tena kidato cha tano na cha sita,baadae naamua kuingia Jeshi bila kwenda chuo Kikuu. Ninalitumikia jeshi kwa muda mrefu, safari yangu ya Lebanoni kusiamamia amani inanirudisha nyumbani na kukuta mke wangu akiwa na mimba ya miezi sita na mimi nilikuwa nje kwa mwaka mzima.

Nikukumbuka nilipotoka,shida na vurugu za kuwa mbeshi....Oooops!!! Naona dunia sio mahali salama pa kuishi
Charles Kihiyo mgosi
 
Kulikuwa na kikosi hatari sana cha mbwa na farasi,na walikuwa wakifanyia mazoezi kule Line Polisi kama unaelekea kijiji cha Utemini,kweli Mwadui ilikuwa kama Ulaya.

Maziwa kedekede,nyama za kutosha na mabasi ya kuzunguka ndani ya mgodi,toka Kampaundi mpaka Alamasi Road.Kuna boss alikuwa anaitwa Mipawa,huyu aliunda kikosi hatari sana cha mbwa na farasi;walitusumbua sana hasa njia yetu ya kupitia Songwa,Bwawani mpaka Mgodini.

Mkuu ww wa TS,Mwaseco au Agriculture?Umenikumbusha mbali,team ya mpira na marefa kina Mzee Mshangama sisi tukija kushangaa mpira kupitia geti kubwa kwa ruhusa maalumu,halafu jioni tunarudi kama wabeshi.Kweli maisha ni safari ndefu
Hatari sana...babu yangu mzee Mipawa siku hizi ni diwani wa kata ya SayuSayu-Maswa.
 
Mwadui boidi ya huu na nimezaliwa hapo na kusoma hapo
Basi wewe mkuu mbaswike utakuwa ulisoma ama Mwadui A au Mwadui B.Kwa mwalimu Nyabi,Ntantulu,Masunga na Miss Lewis....Nyie watoto wa mwadui mlikuwa mnatukebehi sana wabeshi nyie...
 
Mkuu,Barafu nmekupa salute..umeuza ile chumvi ya NYALAJA!!?
Mkuu Ntaluke.N. salute pia kwako,maana unapita mulemule nilimopite.Nisipouza chumvi ya Nyalaja sasa ntakuwaje mbeshi??Yaani unataja misamiati hatari sana ya miaka hiyoooo....Umenikumbusha mbali sana mpaka nakumbuka jamaa zangu waliotangulia mbele za haki...Asante sana mkuu
 
Hatari sana...babu yangu mzee Mipawa siku hizi ni diwani wa kata ya SayuSayu-Maswa.
Mkuu huyu alikuwa Meneja,alitusumbua sana kwa kuunda Kikosi cha mbwa na Farasi waliokuwa wanapata mafunzo toka Nje ya nchi.Baada ya Ubaguzi wa rangi kuisha,wale mbwa wakawa wanaletwa toka South Africa,ile "specie" ya mbwa waliokuwa wanatumika kuuwa watu weusi wakati wa maandamano ya ubaguzi wa rangi S.Africa.

Wale mbwa ndio waliletwa wakiwa na mafunzo makari sana na walikuwa mbwa katiri sana sana.Jamaa zetu wengi walikufa kwa kuumwa na wale mbwa.Ninamkumbuka huyo Meneja akiitwa Sylivester Mipawa.Kumbe sasa ni diwani?Duuuh.... kituli one mpe salamu anko wako mzee wa benzi
 
maskini mwadui kwisha habari yake imebaki story,wapi swai mikate,wapi hiporaiti moshi,wapi dkt tosiri,wapi chekingo na kabondo mapilot wetu enzi hzo,wapi mwalimu mutembei na mwalimu musa wa ts,wapi mwalimu gontako na mwalimu kachuchuru wa mwadui sec,wapi mwalimu kasoyaga wa mwadui mashariki,wapi mzee ngoromole,mzee ndaki konda wa mabasi ya mwadui,wapi idara ya shamba,wapi dairy farm,wapi golf,wapi ujamaa c,wapi posta na simu,daaah kweli mwadui ilikuwa nzuri sana,mzee wetu muhali,mzee wetu bugome,mzee kimolo,mzee kailembo dj mwakapesa,mzee hincha
 
Mzee Hiporaiti moshi yupo Dar anakula shushu taratibu
 
Umesahau Mashine Kubwa na duka kubwa!!Songwa Club na Twiga Hostel,Team ya Mwadui na kina Mshangama.

Sema watoto wa Mwadui mlikuwa na dharau sana kama mnaishi Ulaya
 
Back
Top Bottom