Tulivyojengwa JKT 1970

Tulivyojengwa JKT 1970

Joined
Nov 11, 2007
Posts
10
Reaction score
74
RUVU JKT
HIFADHI YA MAISHA YANGU: (NAKUMBUKA NATAFAKARI SANA, NASONONEKA)

1.1 Ni kwanza kondoka kwetu, napenda hilo mjuwe;
1.2 Niko Ruvu nathubutu, kujenga Taifa liwe,
1.3 Kishapo nirudi kwetu, mengineyo nipangiwe,
1.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

2.1 Ninang'arisha viatu, na magwanda niyafuwe,
2.2 Kisha nibebe mtutu, shabaha nijaribiwe,
2.3 Kamwe sitouwa mtu, ila nchi ivamiwe,
2.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

3.1 Ubongo siote kutu, twenda elimu tugawe,
3.2 Twafundisha watukutu, pia wazazi wenyewe,
3.3 Ghafla twaona chatu, wacha mbio tuzitowe,
3.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

4.1 Ruvu Chini shamba letu, ardhi tuitibuwe,
4.2 Tunapanda kila kitu, mpunga na njugumawe,
4.3 Shamba kamwe si msitu, bora mazao yakuwe,
4.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

5.1 Twabeba mapanga yetu, wasitutishe nguruwe,
5.2 Mashoka yaliyo butu, inabidi tuyanowe,
5.3 Tuwezefyeka misitu, mpingo tuuondowe,
5.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

6.1 Ufugaji kazi yetu, wavivu msitujuwe,
6.2 Tule nyama kefu yetu, na maziwa tukamuwe,
6.3 Ngozi nazo ni sapatu, pia jamvi zikaliwe,
6.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

7.1 Afande yu mwanagutu, anenayo muambiwe?
7.2 Adhani atenda utu, siutaki udadawe,
7.3 Tanga nina wangu Fatu, mwambeni asinijuwe,
7.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

8.1 Walojawa ukurutu, wataka waabudiwe?
8.2 Eti sisi 'recruit', adabu sawa tutiwe,
8.3 Liko wapi kosa letu, hadi haya tutendewe?
8.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

9.1 Imara fuadi zetu, nchi hii tu wenyewe,
9.2 Uzalendo sifa yetu, si sawa tuonelewe,
9.3 Wengi wetu Wabantu, haiswihi tuchezewe!
9.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

10.1 Twangoja majibu yetu, ili vyuo tupangiwe,
10.2 Tukanowe vichwa vyetu, mambo mengi tuyajuwe,
10.3 Tuijenge nchi yetu, uchumi wake ukuwe,
10.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

11.1 Sitobadilika katu, pendo langu kwako wewe,
11.2 Tanga wewe u mwenetu, sina wako mfanowe,
11.3 Sitokucheza upatu, daima mimi ni wewe,
11.4 Nimeshakuaga kwetu, lolote Mola naliwe!

Omari R. Nundu
D Coy, RUVU JKT
27 Disemba 1970
 
Mzee vipi na mashairi ya mwaka 1970? unatuletea ujumbe gani hapa Mzee wetu.

Nakumbuka jinsi Naibu Waziri alivyokuzunguka mbuyu hadi ukapiga yowe hadharani!!!
Mzee alifanyiwa Fitina mbaya sana. nadhani utu mzima na busara zilimponza, asiwaone wengine kila balaza la mawaziri wamo wengi pale washirikina

sasa ye alileta za inshalaah!!!
 
Pole waziri mtimuliwa.... JKT ulienda lakini huwezi kujenga nchi peke yako
 
11.2 Mapenzi ya kiongozi kwa TANGA yako juu zaidi ya TAIFA.
 
hongera kwa utunzi mzuri
mr nundu hiyo JKT haikukusaidia kuwa mzalendo,ndio maana wengi waliopitia JKT wameshindwa kuonyesha uzalendo zaidi ya uroho na ubinafsi
 
Kila mmoja wetu ana uhuru wa kusema na jambo usilolijuwa ni usiku wa kiza hivyo tahadhari ni muhimu kwani ulimi hauna mfupa. Ni tabia murua ya binadamu kuchunguza kujuwa ukweli, kujiridhisha, kuamini halafu ndio kueneza.

Ukifanya vinginevyo unapungukiwa na sifa za ukhalifa duniani. Matokeo unaendeleza chuki kuhusu Fulani kitu ambacho ni sifa ya viumbe wengine sio binadamu!
 
as long as ukiwa chama cha escrow is nearly impossible kuwa msafi maana hawana refarii ni full faulo
 
Omar Nundu at his best ...watu wote vichwa utawala wa Kikwete wanafanyiwa fitna anashindwa kuwatetea ...
Sasa mkuu ulitaka awatetee vipi? ni wakati hawa unaowaita vichwa nao watambue kufanya kazi na serikali tapeli na fisadi sio kazi rahisi. Hiyo ndio test ya kwanza hao 'vichwa' walisihindwa kudhihirisha 'ukichwa' wao hata kabla ya kula viapo vya kazi.
 
Mzee Nundu,

Mi nashauri tu kua ni vizuri ukaandika kitabu au vitabu kufumbua hayo yaliyoko moyoni mwako, ukaainisha hoja na matukio kinagaubaga ili sisi wananchi tukupate kwa ufasaha.

Haya mashairi ni mazuri lakini hayatupi picha ya nini unataka kusema!
 
Omar Nundu at his best ...watu wote vichwa utawala wa Kikwete wanafanyiwa fitna anashindwa kuwatetea ...

Mkuu there is something that the rest of us might not be in a position to know about this Ex-Minister. Kwa siasa zinavyokwenda inawezekana alikuwa hana au ana makosa. Tujuze kidogo tujue...kuliko kuwa na habari nusu nusu za wenye vipaza sauti.
 
Kila mmoja wetu ana uhuru wa kusema na jambo usilolijuwa ni usiku wa kiza hivyo tahadhari ni muhimu kwani ulimi hauna mfupa. Ni tabia murua ya binadamu kuchunguza kujuwa ukweli, kujiridhisha, kuamini halafu ndio kueneza. Ukifanya vinginevyo unapungukiwa na sifa za ukhalifa duniani. Matokeo unaendeleza chuki kuhusu Fulani kitu ambacho ni sifa ya viumbe wengine sio binadamu!

Ushauri wa kuandika kitabu si wa kupuuzwa kwenye jamii ambayo mambo yanayosemwa sio lazima yawe yale yaliotendeka.
 
Back
Top Bottom