Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kwa takribani wiki moja nilikuwa nje ya mtandao wa Facebook kutokana na HUJUMA za "watu" wachache walioamua kureport akaunti yangu kwa kudai kuwa ninaandika mambo ambayo ni kinyume na "Facebook policies". Zaidi ya watu 100 walinireport hali iliyosababisha Facebook kunipa 'ban' ya muda ili waweze kureview taarifa zilizolalamikiwa.
Kutokana na tukio hili niliamua kufanya ufuatiliaji na kugundua kuna vijana walioamua kureport akaunti za watu wanaodaiwa kuwa ni "wakosoaji" wa serikali. Jumapili ya tarehe 05 June, zaidi ya akaunti 5 zilifungiwa na zote ni za watu wanaodhaniwa kuwa "wakosoaji".
Akaunti ya Kwinyara Kwinyara ilifungiwa saa 3 usiku, akaunti ya Allan Bway ilifungiwa saa 5 usiku na ilipofika saa 6 usiku akaunti yangu ilifungiwa. Huu ni ushahidi tosha kuwa waliomripoti Kwinyara ndio walioniripoti mimi na ndio waliomripoti Allan pamoja na watu wengine waliofungiwa.
Kwahiyo haihitaji "degree" kujua huu ni mpango uliosukwa. (An organized mission). Lakini kati ya wote mimi ndiye niliyepewa adhabu kubwa zaidi ya kufungiwa wiki moja. Wengine "vifungo" vyao vilikua ni chini ya hapo.
Haikuwa rahisi kukabiliana na hali hiyo ya kutengwa na jamii yangu. Haikuwa rahisi kukubali kunyamazishwa kwa sababu tu kuna watu hawafurahishwi na ninayoyaandika. Haikuwa rahisi kukubali kukosa fursa ya kujadili bajeti na matukio mengine muhimu ya kitaifa yaliyotokea.
Lakini hatimaye kifungo kimeisha na nimerejea. Nina mambo kadhaa ya kuwaeleza vijana walioripoti akaunti yangu ikafungiwa.
#Mosi; nimewasamehe.
#Pili; Wajifunze hesabu. Nliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kwa kawaida kumreport mtu facebook na akafungiwa kunahitaji kuanzia watu 50 na kuendelea. Vijana walioniripoti ni takribani 100.
Hapa Facebook nina marafiki karibu 5,000 na "Followers" 40,000. Kwahiyo jumla nina jamii ya watu 45,000 ambayo imenyimwa haki ya kusikia mambo mbalimbali kutoka kwangu kwa takribani wiki moja au zaidi.
Nikiiambia jamii hii ilipize kisasi kwkureport akaunti za vijana wa CCM, maana yake ni kwamba jumla ya vijana 900 watafungiwa akaunti zao (45,000/50). Kwahiyo ndani ya siku moja tu akaunti zote za vijana wa CCM zinaweza kufungwa na wao wakaonja "machungu" ya kukaa nje ya mtandao huu kwa muda.
Jamii hii ina nguvu kubwa. Si jamii ya kubeza. Watu 45,000 ni mara mbili ya kura ambazo Shein alidaiwa kumshinda nazo Maalim Seif (tofauti ya kura). Kwahiyo jamii hii ikiamua kufanya "revange" hakuna kijana wa Lumumba atakayepona. Let them be informed.!
#Tatu; Kama walionireport walitumwa basi aliyewatuma hana akili (ni zwazwa). Na kama walijiorganize wenyewe basi wao ni mazwazwa wa kiwango cha juu mno. Ikiwa maandiko yangu yanawakera kuniripoti sio suluhisho la kudumu; maana nitafungiwa kwa muda na nitarudi tena kuendelea kuwakera.
"Only fool can find temporary solution for the permernent problem". Ningewaona wana akili kaama wangeweza kuniripoti nikafungiwa milele. Lakini hata kama ningefungiwa milele bado ningekua na fursa ya kufungua akaunti nyingine na kuendelea kuwakera. So nawashauri wasirudie tena uzwazwa wa aina hii.
I'm back. The partner in critical thinking is back. Wenye chuki tafuteni mbinu nyingine za kufunga midomo ya "watu wenye akili" sio mbinu hizi za kijinga.!
Malisa G.J