Amanikwenu
Senior Member
- Dec 1, 2009
- 187
- 0
Kutokana na ukweli kuwa hali ya amani na majirani zeu inazidi kuimarika, kuna haja kama nchi kuliwezesha Jeshi letu na kulipa Jukumu rasmi la Kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya taifa hili. Natumaini kukiwapatia vifaa vya kutosha na utaalam unaohitajika na kuwapa Bonde la Rufiji au Kilombero, tutaona mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa chakula hapa nchini ndani ya kipindi kisichozidi miaka mitano. Tukumbuke kuwa zaidi ya asilimia 75% ya kupanda kwa mfumuko wa bei hapa nchini inatokana na kutokuwa na chakula cha kutosha.