Tuliowahi okota embe dodo tukutane hapa

Nilishawahi kuwekewa sh. Milioni nane kwenye account yangu ya bank ambayo salio langu halisi lilikuwa halizidi laki tano maana pesa yote niliimaalizia kwenye ujenzi. Nilikuja kugundua baada ya kutoa pesa kwenye ATM na kuangalia kiasi kilichobaki. Ile hela ilikaa kama miezi miwili hivi nilikuwa naogopa kuitoa maana bank wana full information kuhusu mimi kama according to process zao za kufungua account. Baadae nikaanza kuchukua kidogo kidogo mpaka nikatumia milioni tatu, siku hiyo nipo kazini sina hili wala lile napigiwa simu na ofisa wa ile bank kutoka makao makuu kuwa na kuambiwa kuwa kwenye account yako kuna hela sh. Milioni nane imeingia kimakosa na umeshatumia sh. Milioni tatu hivyo unatakiwa uirudishe. Nikawajibu nitakwenda kwenye branch yangu niliofungulia account ili wanifanyie reconciliation kabla ya kulipa hilo deni. Jumamosi moja nikaenda pale branch nikaonyeshwa full evidence, nilikuwa nataka kukwepa kulipa hivyo nilikuwa naangalia kweli wana ushahidi wa kutosha. Halafu nikawauliza tatizo hili ni kwangu tu au kuna wenzangu, nikajibiwa wapo wenzio mpo kama mia moja hivi. Nikataka kujua ilikuwaje mpaka tatizo likatokea, wakanijibu kuwa kuna tarehe wakaitaja kuanzia saa moja usiku mpaka saa moja na nusu system ya bank kwenye ATM machine ilijichanganya na kufanya kila anaetoa hela kwa muda huo inazidisha mara ishirini ya ile pesa aliotoa na inaweka kwenye account. Nikakumbuka kuwa ni kweli siku hiyo nilitoa kwenye ATM shilingi laki nne. Nikauliza mbona mmekaa zaidi ya miezi miwili ndio mnatutafuta, wakanijibu kuwa hata wao wenyewe walichelewa kugundua hilo tatizo. Nikawajibu hiyo pesa nimeshatumia nitawalipa kidogo kidogo, nikaambiwe niandike kwa mkono wangu kuwa nitalipa hiyo pesa kama ushahidi. Sijalipa mpaka leo ni mwaka wa tatu sasa na ile account nimeichilia mbali, mwanzoni walisumbua sana kwenye simu ila kwa sasa nadhani watakuwa wameshakata tamaa na kuniorodhesha kwenye bad debts.
 
Nilieenda kariakoo kuchukua Home theatre Sony,wahudumu wakaniuzia Kwa lak 5 wakaifunga fresh,badae mwenye Mali anakuja anawaambia wamechanganya bei n lak 6.5 na maduka ya pemben yalikuwa yanauza had lak 7,coz nilikuwa mteja WA Kwanza na Mali ishafungwa jamaa hakuwa na namna.
Nikasepa na Mali yangu.
 
Niliwahi kuokota dodo mida ya jioni kabisa nikiwa nimeshakata tamaa kbs leo nalalaje na njaa baridi yote hii ya june Arusha. Kila alieniona nalo alilitamani nami nikalilinda lisiniponyoke.
Nilikuja kugundua sio dodo baada ya kufika geto maana tangu naanza kuchapa mzigo mpaka namaliza alikuwa anapokea simu kama yupo kitengo cha huduma kwa wateja vodacom, hamu iliisha na sikurudia tena.
Ulikuwa wa kwanza kwenye orodha yake!
 
Mara mbili, kwanza niliiwekea pesa 200,000 kwenye mashine ya selcom, pesa ikaingia kwenye mashine na bado kwenye airtel money ikabaki na nikaitoa.
Pili jiran yangu dukan alikuja kutoa mpesa 100,000 kabla ya kuchukua pesa akaitwa dukan kwake akaenda nikijua atarudia pesa yake ajabu hakurudi na hata siku zingine alipokuja dukan alikuja kwa mishe zingine tu.
Na wewe ukakaa kimya, humkumbushi jirani!
 
Kuna jamaa alinitumia laki 2 kimakosa,alilia sana kwamba alikuwa anamtumia mwanae hela ya ada iliyobaki na mtoto kule anafukuzwa chuo
,nikamwambia mi sitoi hela yako na nikutumie wapigie voda wenyewe wakurudishie ila mi hela yako sigusi
 
Mie niliokota chini ya mti Morogoro lilikuwa tamu sana na kila nikikumbuka nilivyolila embe dodo lile huwa natabasamu. Nilirudi maskani Mfaranyaki lakini utamu wa lile embe dodo haukuwa wa kawaida hivyo nikalirudia tena Moro. Kufika na kuwauliza wenyeji karibu na ule mwembe maana sikuuona pale nilipookota embe dodo wakaniambia ule mwembe ulikatwa. Nikabaki na masikitiko na kesho yake nikarudi maskani. 😜😜😜

Kuna wakati hadi unashukuru Mungu hata ulie machozi kwa jinsi ulivyo na bahati.

Wengine wamewahi okota fedha, wangine wachumba, wengine kazi.. etc.

Kuna mengine yanatokea kwa uzuri upande wako lakini sio mazuri kwa wengine.

Mfano huna pesa.. unampa mwuza duka buku ununue kitu cha buku ila ajabu anakurudishia elfu 9 akidhani umempa buku 10..

Mimi niliwahi rushiwa laki 5 na wakala wa mpesa hadi leo hawaja ulizia.. na unajua ukitumiwa fedha na wakala haina namba ya simu.. hivyo nipo nasubiri voda wanipigie leo ni mwaka wa 3.

Ebu twambie jambo gani ambalo ulijiona kama mtu mwenye bahati.View attachment 1131288
 
Ukifurahia ulichokiokota ujue huko aliyepoteza analalamika au hata anamwaga chozi.........niliwahi kuokota sh elfu 42, nikafurahi sana, lakini baada ya mwezi mmoja hivi nilikuja kupoteza sh laki 2 na elfu 80........machungu yake yake sitaki kabisa kuyakumbuka, sasa hivi nikiokota hela basi nitakaa eneo lile hata kwa nusu saa ili nikiona mtu anakuja huku anaangzaangaza chini najua ndio mwenye mzigo
Mkuu upo?
 
Mkuu wewe muhongo, inamaana umeokota kwwnye daladala na unakaribia kushuka utaendelea kukaa?
 
Nilikuta nimeekewa laki 9 kwenye account yangu ya bank nikaicha week 2 bila kuigusa nilivyoona bado ipo nikaanza kutoa kidogo kidogo labda ni commission yangu ya mteja wao kwa muda mrefu siwezi jua.
Safi Saana Hio Hela Tulituma Sisi
Wiki moja Tutakuja Kukuchukua Mtu Wetu
 
Nina kimeo na NBC hadi leo toka 2007pale Mlimani city, waliweka kimakosa 500,000 mi nikapita nayo walinisumbua miaka minne mfululizo, sijalipa hadi leo na niliacha rasmi kutumia bank ya NBC
hawaja kufungulia kesi ya wizi?
 
Intereting.. nasoma mtu wa pili aliye ingia mitini na pesa ya bank... inaonekana bank wanapigwa sana na waokota dodo
Nilishawahi kuwekewa sh. Milioni nane kwenye account yangu ya bank ambayo salio langu halisi lilikuwa halizidi laki tano maana pesa yote niliimaalizia kwenye ujenzi. Nilikuja kugundua baada ya kutoa pesa kwenye ATM na kuangalia kiasi kilichobaki. Ile hela ilikaa kama miezi miwili hivi nilikuwa naogopa kuitoa maana bank wana full information kuhusu mimi kama according to process zao za kufungua account. Baadae nikaanza kuchukua kidogo kidogo mpaka nikatumia milioni tatu, siku hiyo nipo kazini sina hili wala lile napigiwa simu na ofisa wa ile bank kutoka makao makuu kuwa na kuambiwa kuwa kwenye account yako kuna hela sh. Milioni nane imeingia kimakosa na umeshatumia sh. Milioni tatu hivyo unatakiwa uirudishe. Nikawajibu nitakwenda kwenye branch yangu niliofungulia account ili wanifanyie reconciliation kabla ya kulipa hilo deni. Jumamosi moja nikaenda pale branch nikaonyeshwa full evidence, nilikuwa nataka kukwepa kulipa hivyo nilikuwa naangalia kweli wana ushahidi wa kutosha. Halafu nikawauliza tatizo hili ni kwangu tu au kuna wenzangu, nikajibiwa wapo wenzio mpo kama mia moja hivi. Nikataka kujua ilikuwaje mpaka tatizo likatokea, wakanijibu kuwa kuna tarehe wakaitaja kuanzia saa moja usiku mpaka saa moja na nusu system ya bank kwenye ATM machine ilijichanganya na kufanya kila anaetoa hela kwa muda huo inazidisha mara ishirini ya ile pesa aliotoa na inaweka kwenye account. Nikakumbuka kuwa ni kweli siku hiyo nilitoa kwenye ATM shilingi laki nne. Nikauliza mbona mmekaa zaidi ya miezi miwili ndio mnatutafuta, wakanijibu kuwa hata wao wenyewe walichelewa kugundua hilo tatizo. Nikawajibu hiyo pesa nimeshatumia nitawalipa kidogo kidogo, nikaambiwe niandike kwa mkono wangu kuwa nitalipa hiyo pesa kama ushahidi. Sijalipa mpaka leo ni mwaka wa tatu sasa na ile account nimeichilia mbali, mwanzoni walisumbua sana kwenye simu ila kwa sasa nadhani watakuwa wameshakata tamaa na kuniorodhesha kwenye bad debts.
 
Ni kweli unaweza tumia bila kujua..
Walishaacha kunifuatilia, sababu kosa lilikuwa lao na walichokosea, walikubali ni makosa yao na walitaka nijicomit kwa maandishi, hapo ndo palikuwa pagumu
 
Back
Top Bottom