Toka nilivyokuwa mdogo mpaka leo, mama yangu ananiambia changu ni chake, na chake ni changu. Ananiitaga baba yake. Hii ilimtokea yeye, but since it was mine too, acha nitoe ushuhuda.
2011, mama alikutana na kaka mmoja aliejifanya anafanya kazi kampuni X ya simu. Akawambia kampuni ilimpa tenda ya matangazo, but alihitaji more money. Kweli Mara ya kwanza mama alimpa 40m akapata na faida juu ya 30m, kwa maama tulirudishiwa 70m in 3 months. Kumbe ilikuwa trailer tu.
Huyu jamaa alikuwa anaendesha marange, land cruiser latest na BMW X5. Anapiga suit tu. Sehemu za kumeet ni golden tulip au White Sands... High class places.
Akaja Mara ya pili, now akasema tenda ya TZ yote, anahitaji 400m. Mama alimuamini sana. Akakopa mkopo bank wa mil 150, akauza magari, viwanja, akampatia 400m. Hapo home maisha yalichange kabisa, mama anatuhakikishia its temporary. Hakujua kuwa its gonna be for a very long time. Jamaa alivyopewa kesho yake akapotea.
Tulikuja kumpata South Africa, tukamuweka ndani, anasema na yeye katapeliwa na kazi alikuwa hafanyi kampuni ya simu X, na magari yalikuwa ya kukodi. Jamaa alikuwa hana kitu kabisa. Katupa Nyumba yake gofu... Matengenezo karibu 50m. Gorofa letu Mara ya mwisho ilifanyiwa valuation ilikuwa 556m. Tukashindwa kurudisha Nyumba imeuzwa. Leo hii tunapokaa. Naandika hapa nalia. Acha nifungue kitabu niendelee kusoma. Nitakujengea tena mama, changu ni chako.
-callmeGhost