Tuliowahi kupigwa kamati tukutane hapa

MBWAMBO NICHOLAUS JR

JF-Expert Member
Oct 27, 2018
424
427
Umofia kwenu wana JF.

Niende kwenye mada moja kwa moja kamati ninayosemea hapa ni ile ya asili kamati ya roho mbaya.

Kwa ufupi kama uliwahi fanyiwa ulozi na wataalamu na kupotea kwenye ramani.

Miaka saba iliyopita aisee nilipata tabu sana kijana mimi mana tangu kuzaliwa mpaka form four sikuwahi kwenda kwa mganga wa kienyeji na kwa nadra sana hospital kutibiwa.

Muda mwingi nipo mzima wa afya kabisa nilianzia shule ya msingi kuuza vitumbua shuleni mama anachoma mimi nauza shuleni wakati wa mapumziko na lazima viishe nilikua nabeba deli la vitumbua 100 kila siku za shule wikiend natembeza barabarani na mitaani.

Shuleni nilipata umaarufu sana kwa sababu nilikua najulikana mana nilikua sikopeshi ila mzigo unaisha una ujanja wangu hadi walimu wananijua.

Nadhani mnajua tabia za wakaka wanaouzaga vitafunwa mashuleni

Likizo nilikua nachoma mihogo nauza mpaka form four nilipomaliza

Sasa kimbembe kilianza hapo baada ya kumaliza shule aisee ROHO YA KUKATALIWA ndio ilianza niingia taratibu vibiashara vyangu vilianza kudorora mara naumwa nikienda kupima ugonjwa sioni fulu kulala basi nilianza kuwa kama zuzu hivi.

Nilifika hadi muhimbili kupima ila hamna ugonjwa ila mwili unauma sana hatari viungo vyote vinauma sio mchezo.

Shangazi yangu mmoja akasema basi twende ukaombewe niliendaga kwa mzee wa ubungo tukasali ilifika mda wa maombi nikaombewa sana basi kila siku za maombi nilikua naenda hapo. Kidogo nilianza kupata nafuu. Miezi mitatu mfululizo ila hivyo hivyo tu.

Kuna bro wangu binamu yeye kasema dogo njoo twende sehemu fulani hivi kwa mtaalamu nikajua specialist kumbe wale wa tawile

Yule mzee aisee akawa anamwambia broo kuwa mdogo wako anatatizo la Roho ya kukataliwa yaani maneno yake direct yanafanana na yule mtumishi wa Mungu basi alinipa maujanja yake huku church baada ya miezi mitatu mbeleni nashukuru Mungu nilipona nimerudi kawaida kabisa....na kuanzia pale aisee nimejifunza maisha haya yana siri kubwa sana jamani sikieni tuu kamati ya ufundi sio mchezo unaweza kuwa mentor.

Share na wewe experience yako
 
Umofia kwenu Wana JF, tuanzie hapa kwanza, kwa Nini unatumia lugha ya kihuni, unatuona sisi humu JF ni wahuni wenzako?
 
unaamka unatoka nje unaota jua unatafta japo buku mbili ukiipata unakula ukishiba unarudi kulala unaamka unatafta tena buku unakula unalala, siku inapinduka, asubuhi unaamka mchoovu, akili inafikiria pesa ya kula tuu na kununua bundle, madem unaopata ni wale toleo la mwisho, wenzako wanatoboa wewe upo tu kama ndondocha, nywele hunyoi hata vuzi unakuja kukumbushwa na beki tatu jaman we mkaka mzuri ila ujipendi, mwili unakuwa hauna nguvu hauna nguvu ya uthubutu ktk jambo lolote lile, yaani unakuwa zombie si zombie dah haya mambo niliyaona hapo uzaramuni watu watundu sana..yaani mtu anakuweka lijiwe mgongoni unalala nalo na unaamka nalo unazurula nalo ye anakuchora tu.
 
unaamka unatoka nje unaota jua unatafta japo buku mbili ukiipata unakula ukishiba unarudi kulala unaamka unatafta tena buku unakula unalala, siku inapinduka, unaamka mchoovu, akili inafikiria pesa ya kula tuu, madem unaopata ni wale toleo la mwisho, wenzako wanatoboa wewe upo tu kama ndondocha, nywele hunyoi hata vuzi unakuja kukumbushwa na beki tatu jaman we mkaka mzuri ila ujipendi, dah haya mambo niliyaona hapo uzaramuni watu watundu sana..yaani mtu anakuweka lijiwe mgongoni unalala nalo na unaamka nalo unazurula nalo ye anakuchora tu.
Sio mchezo mkuu ila wengi hawajawahi ona maisha ya muundo huu
 
Umeifanya biashara yako kwa mazoea muda mrefu,
amekuja mtu kakusoma mapungufu,
Ameanzisha biashara kama yako,
Kayaondoa mapungufu yote aliyoyaona kwako,
Wateja wamehamia kwake,
Unaanza kukimbia huku na kule eti umelogwa!
Mambo mengine yanahitaji uwezo mdogo tu wa kufikiri!
 
Umeifanya biashara yako kwa mazoea muda mrefu,
amekuja mtu kakusoma mapungufu,
Ameanzisha biashara kama yako,
Kayaondoa mapungufu yote aliyoyaona kwako,
Wateja wamehamia kwake,
Unaanza kukimbia huku na kule eti umelogwa!
Mambo mengine yanahitaji uwezo mdogo tu wa kufikiri!
Unayosema yamkini kweli ila kuna mazingira ukiangalia hata akili ya kawaida tuuu watu wanakushika sikio
 
unaamka unatoka nje unaota jua unatafta japo buku mbili ukiipata unakula ukishiba unarudi kulala unaamka unatafta tena buku unakula unalala, siku inapinduka, unaamka mchoovu, akili inafikiria pesa ya kula tuu, madem unaopata ni wale toleo la mwisho, wenzako wanatoboa wewe upo tu kama ndondocha, nywele hunyoi hata vuzi unakuja kukumbushwa na beki tatu jaman we mkaka mzuri ila ujipendi, dah haya mambo niliyaona hapo uzaramuni watu watundu sana..yaani mtu anakuweka lijiwe mgongoni unalala nalo na unaamka nalo unazurula nalo ye anakuchora tu.
Kuna jambo la kujifunza hapa!
 
Okay umeshatuambia haya mambo sana,okay tupe solutions ni nin tufanye ili tuweze kutoka kwenye huo mkwamo?,,,au sio wazee....
 
Back
Top Bottom