Tuliowahi kuibiwa tukigombea daladala tukutane hapa

EvilSpirit

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Posts
13,610
Reaction score
21,468
Habari za mchana wakuu.Tunajua dar ni miongoni mwa miji yenye shida sana ya usafiri.

Hili linachangia daladala zigombaniwe sana vituoni kama daladala za mbagala.

Ugombaniaji huu huwa hauna cha mzee,mwanafunzi,mzee,kijana wote mnakuwa kama kuku.

Vibaka ni miongoni mwa wanaojifanya abiria na kutuibia.Mimi ni mmoja wa maboya tuliowahi kuibiwa wakati tunagombania daladala.

Tukio la kuibiwa lilinitokea pale buguruni chama saa moja jioni.Niliibiwa simu niliyoiweka kwenye mfuko wa nyuma wa suruali ya cadet nilifunga kifungo cha mfuko wa suruali lakini niliibiwa niligundua hilo baada ya kuwa nimepanda.

Nilishindwa kuelewa ile simu ilitokaje mfukoni wakati nilifunga kifungo cha mfuko wa suruali.

Nawe tupe madhira yaliyowahi kukutokea ukiwa unagombania daladala
 
Wewe kweli boya.....simu unaweka mfuko wa nyuma!!! Yaani hapo ulimrahisishia sana kazi kaka kibaka.
 
  • Thanks
Reactions: sab
huwezi mtu u
Wewe kweli boya.....simu unaweka mfuko wa nyuma!!! Yaani hapo ulimrahisishia sana kazi kaka kibaka.
huwezi ukawa unajua kila kitu,jambo likikutokea ndio unajifunza kama saivi naificha inakaa na korodani nikishapanda ndio naitoa
 
Mimi niliwahi kuibiwa pesa pekee niliyokuwa nayo na sikuwa na tumaini la kupata nyingine huku nikiwa na mke na watoto [emoji87]. Nilitamani isiwe kweli.
 
Pole.
Kuna chama cha wezi wa kuchomoa noti Mbagara sijui kiko hai.
Yaani walikuwa wanakiita CHADEMA, Hao jamaa wanaingiza vidole viwili taratibu na kutoka na mali mfukoni mwa mtu wakati raia wanagombania bombardier
 
mh we mwana we hivo vidole wanaingiza wapi
 
Jamaaa walikwapua simu kutokea dirishani , ki Nokia changu kikaenda
 
Hii kitu inauma sanakamanda, nimejichanga nikiwa chuo nikanunua kanokia kangu ka kishkaji angalau nipate mawasiliani na wanachuo wenzangu,.Siku ya siku nikakaa chuo mpaka saa tatu kumaliza kazi zote ili siku ya pili niamke fresh, kilichotokea kumbukumbu ambayo inaumiza sana, nikajikongoja posta kupanda bus la mwenge, kumbe nimepanda na mmiliki halali wa simu mana hata alipoichomoa wala sikuisikia zaidi ya kufika home na kuiangalia nikiwa nataka kuomba nondo kwa mshkaji nikagundua kama nimepigwa, niliumia sana ika sikuwa na jinsi ndo ishakuwa tena
 
Hahaha eti mmiliki halali
 
Pole kiongozi,Mwizi pengine alikulia mingo toka unapanda daladala
 
Kuna jamaa mmoja alijaribu kumuibia abiaria mmama kwa kufungua zipu ya pochi tukiwa tumebanana kwenye gari nilipomuona nikamwambia yule mama unaibiwa basi akaigeuza pochi yake upande mwingine yule kaka akashuka ananitukana matusi makubwa makubwa
 
haha ulizuia riziki haramu ya mtu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom