Tuliowahi kuhisi kuumwa/ Wagonjwa wa Corona tupeane uzoefu

komanyahenry

JF-Expert Member
Sep 15, 2017
903
1,352
Kama wiki kadhaa nyuma kipindi hiko COVID -19 ndio ipo kwenye pick, nilishikwa na homa moja kali na ya ajabu, na before that nilikuwa na ruti sana za kutoka mikoani kuja Dar, ile home iliambata na kuumwa viungo vya mwili pamoja na kikohozi kikavu sana hasa wakati wa usiku nikilala.

Nikazama dispensary ya mtaani nikapima BS, typhoid, UTI na FBP, majibu kutoka vyote sina, nikapewa dozi ya cetrizen kwa ajili ya kikohozi na paracetamol. Nimetumia dozi siku ya pili naona hakuna nafuu nikajiongeza kwa dose ya mseto nikihofia inawezekana maralia ninayo ila haionekani.

Baada ya kumaliza dose ya maleria na cetrizen, bado nikawa nina homa. Hapo ndio nilianza kupata hofu labda nishpata huo ugonjwa wa futa kwenye njia ya hewa, muda huo wife kashaanza kupata wasiwasi na kuwajulisha wazazi wangu kuwa nina corona na sitaki kwenda hospitali uzuri ni kuwa nilikuwa naishi peke yangu maana nipo mkoa mwingine. Ikabidi niingie kupiga nyungo na kupiga chai ya tangawizi, limao na asali na ndio ikawa dose yangu ya asubuhi na usiku.

Ila now nashukuru Mungu nipo vizuri kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza mara ya kwanza kabisa ilikuwa mwishoni mwa mwezi wa 11 nilipata mafua makali sana yakiambatana na homa kari sana kichwa kuuma macho hayaoni yale mafua yanatitirika hayaivi jasho linatoka hatari kwa muda wa week moja.

Kila nikipima maralia hakuna mbaya zaidi wote ndani tuliumwa. Wengine ilikuwa hatari zaidi kila ukienda hospital hakuna ugonjwa unaonekana.
Ilikuwaje bro

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom