Dharura: Nahisi nina dalili zote za Covid naombeni msaada tafadhali

Secret person

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
242
358
Habari za usiku wakuu,

Kabla sijaelezea kwa undani sana Suala la dharura linalonikumba katika afya yangu ambayo kwa dalili zote nahisi nitakuwa nimeunasa ugonjwa wetu ambao inaweza semekana Haipo nchini.

Siku ya Ijumaa Mchana nilianza kujisikia vibaya kuumwa kichwa kwa sana kutapika kukooa mfululizo na kutohisi hamu ya kula kwenda kwenye dispensary nilipima malaria na UTI majibu yalikua BS results ya Malaria Positive na UTI Negative Hivyo Dr alinianzishia dose zifuaatazo

ALU tabs
Amoxiccilin 250 mg 2/7
Paracetamol
Cough syrup

Baada ya kuanza dose kuanzia siku hiyo ya ijumaa nilikuja kumaliza mseto jumapili na huku dawa nyingine zikiendelea lakini hali bado iliendelea kuwa vile vile ambapo nikaamua kwenda kwenye hospital kubwa iliyopo barabara ya kutoka Mikocheni hadi morroco kufika nikapima malaria na FPB.

Majibu yalikuja kuonyesha sina na malaria na wala bloos yangu haina shida yoyote hivyo Dr alinipa Ibuprofen tabs na Cough syrup nyingine zecuf na kuniambia niendelee na Zile antibiotics hiyo ni jana.

Wakuu ninapoongea Hapa nipo macho sina usingizi kichwa kinaendelea kuuma balaa na Huku nikiendelea kukooa kikohozi kikavu kinacholeta sauti kwa mbali na mwili wangu una Joto balaa.

Msaada Wenu wakuu nimeshaanza kujifukiza hapa ndo nimechemsha matangawizi.

Aisee Sijui Huku ndo kufa Huku btw Mbona bado mdogo mimi.

Msaada
 
Mkuu relax, yaani nimeshauguza wagonjwa wengi na walikuwa wamethibitika kuwa na covid na wote wamepona.

Kama huna matatizo mengine makubwa tena, covid na takataka zake zitadunda kwako siku 7 nyingi mbona.. Usijifukize sana chief sio nzuri, fanya kawaida tu maana unahitaji oxygen ya kutosha.

Mwisho acha kuiwazia kiuwoga, ni kama homa tu ya kawaida.
 
Niliumwa kakitu kama c-19 ila kwa ubishi wangu nikawa napiga makali alafu mchanganyiko... Vladimir, k'vant, konyagi, ambiance na kitoko yani nimejikuta napona tu wala sijui kati ya vyote hivyo kipi ni dawa.

Sikushauri utumie hizo vitu ila kikubwa kuwa na imani tu anko you never know which is which.... Pole bro maana sina cha kukusaidia zaidi ya dua njema kwako.
 
Niliumwa kakitu kama c-19 ila kwa ubishi wangu nikawa napiga makali alafu mchanganyiko... Vladimir, k'vant, konyagi, ambiance na kitoko yani nimejikuta napona tu wala sijui kati ya vyote hivyo kipi ni dawa
... Sikushauri utumie hizo vitu ila kikubwa kuwa na imani tu anko you never know which is which.... Pole bro maana sina cha kukusaidia zaidi ya dua njema kwako
Asante sana Imagine Hapa pua kwa mbal zinaziba kikohozi kikavu na kichwa kishawaka moto.

Nipo nje maana ndani naona kama sipati hewa vizuri.

Na Hapa nimeshachoka kwenda mahospitalini
 
Asante sana Imagine Hapa pua kwa mbal zinaziba kikohozi kikavu na kichwa kishawaka moto.

Nipo nje maana ndani naona kama sipati hewa vizuri.

Na Hapa nimeshachoka kwenda mahospitalini
Uko wapi bro? Kama upo mwanza sogea hapa eneo langu nikupe kampani
 
Pole sana kama umetumia dawa za Antibiotic Relax utakaa sawa kikubwa fanya mazoez na uoge kwa sana pia usijichanganye saana na watu na kama upo eneo la wazi i mean kwenye miti mingi jaribu kutulia maeneo hayo ili upate hewa nying na safi isiyo na makemikali
 
Kikohozi | Tangawizi, Iliki, Mdarasini, Asali na Limao
Mafua/Pua | Tangawizi, Limao, Maji Vuguvugu

Tengeneza Tangawizi yenye mchanganyo wa hivyo vitu, tafuta maji ya nazi tumia mara moja kila baada ya masaa 34.

Kuna aina ya mmea/magugu yanaitwa Mabati tafuna kama mirungi, ni matamu ya uchachu kidogo unaweza tumia jojo.

Zingatia mazoezi japo dakika 20 za mazoezi hakika kila siku. Kunywa maji yakutosha.
 
1. Tumia dawa za kupunguza maumivu, mimi nilitumia Flucor Day kunywa viwili halafu utaendelea na kimoja kimoja

2. Kama unakosa appetite ya kula, kula sana nanasi make sure unashiba usikae na njaa

3. Usinywe kabisa kinywaji cha baridi, kunywa maji vugu vugu, kunywa chai yenye tangawizi inayowasha na tumia vidonge vya vitamini C na matunda ya vitamin C

4. chukua maji ya moto kiasi changanya na chumvi na pilipili manga kama unayo kiasi kidogo(a pinch) weka kwny kikombe halafu sukutua yafike kwenye koo pale halafu tema...fanya hivi kila ukiamka, ukitoka kwnye mizunguko na ukimaliza kula halafu unapiga zako chai ya tangawizi

POLE SANA MKUU MIMI NILIFANYA HIVO NIKAENDELEa VIZURI
 
Fanya mazoezi mkuu huku ukinywa maji mengi kwa kila siku walau glass nane lakini iwe unakunywa kidogokidogo iwe kama kilevi chako
 
Mkuu unapona pambana na hofu au uwoga huyo ndo adui ako namba1 kwa sasa

Tangawizi hakikisha kwa siku unatafuna moja mpaka inaisha

Kula matunda hasa mananasi halafu tengeneza juisi ya malimao

epuka kukaa karibu na watu wazima sababu hakuna namna lazima tuwalinde

sisi kazini tuliugua wengi lakini tumepona wote

Covid haina dawa ila wewe pambania immunity yako iwe imara achana na kujifukiza
 
Asante sana Imagine Hapa pua kwa mbal zinaziba kikohozi kikavu na kichwa kishawaka moto...
Saga Tangawizi, binzari, Vitunguu Maji, Vitunguu saumu chemsha, kamulia limao weka asali kunywa Kama chai. Kunywa hii chai mara 3 kwa siku.
 
Niliumwa kakitu kama c-19 ila kwa ubishi wangu nikawa napiga makali alafu mchanganyiko... Vladimir, k'vant, konyagi, ambiance na kitoko yani nimejikuta napona tu wala sijui kati ya vyote hivyo kipi ni dawa
... Sikushauri utumie hizo vitu ila kikubwa kuwa na imani tu anko you never know which is which.... Pole bro maana sina cha kukusaidia zaidi ya dua njema kwako
Hakuna dawa hapo. Una immune system nzuri, una umri mdogo na huna magonjwa nyemelezi (BP, Pumu, diabetes, moyo...)
 
Corona haitibiki " ni kauli ya daktari jana nilipoenda hospitali" jitahidi kula vyakula vinavyoongeza kinga ya mwili hasa vitamini C, tumia na vidonge vya vitamin C. Jifukize , fanya mazoezi na upate muda mwingi wa kupumzika. Pia unaweza ongeza na Bupiji na Cogon zinasaidia kufungua mfumo wa upumuaji. Kama kuna mgonjwa yupo siriaz sana mpe na Ivermectin japo gharama kidogo.
 
Nyungu ukijizoesha inaweza kupelekea Permanent Liver Damage.
Kupona Corona kwa kiasi kikubwa kunachangiwa na Immunity binafsi ya mtu na stage husika, Corona kwenye advanced stage haitolewi na nyungu wala tusidanyanyike-& believe me,wengine wamepiga nyungu na wameenda kijinga kabisa.
 
Ikitokea parapanda limelia ukamsalimie Maalim Seif.. umwambie katuacha ilhali bado tunamuhitaji
 
Habari za usiku wakuu,

Kabla sijaelezea kwa undani sana Suala la dharura linalonikumba katika afya yangu ambayo kwa dalili zote nahisi nitakuwa nimeunasa ugonjwa wetu ambao inaweza semekana Haipo nchini.

Siku ya Ijumaa Mchana nilianza kujisikia vibaya kuumwa kichwa kwa sana kutapika kukooa mfululizo na kutohisi hamu ya kula kwenda kwenye dispensary nilipima malaria na UTI majibu yalikua BS results ya Malaria Positive na UTI Negative Hivyo Dr alinianzishia dose zifuaatazo

ALU tabs
Amoxiccilin 250 mg 2/7
Paracetamol
Cough syrup

Baada ya kuanza dose kuanzia siku hiyo ya ijumaa nilikuja kumaliza mseto jumapili na huku dawa nyingine zikiendelea lakini hali bado iliendelea kuwa vile vile ambapo nikaamua kwenda kwenye hospital kubwa iliyopo barabara ya kutoka Mikocheni hadi morroco kufika nikapima malaria na FPB.

Majibu yalikuja kuonyesha sina na malaria na wala bloos yangu haina shida yoyote hivyo Dr alinipa Ibuprofen tabs na Cough syrup nyingine zecuf na kuniambia niendelee na Zile antibiotics hiyo ni jana.

Wakuu ninapoongea Hapa nipo macho sina usingizi kichwa kinaendelea kuuma balaa na Huku nikiendelea kukooa kikohozi kikavu kinacholeta sauti kwa mbali na mwili wangu una Joto balaa.

Msaada Wenu wakuu nimeshaanza kujifukiza hapa ndo nimechemsha matangawizi.

Aisee Sijui Huku ndo kufa Huku btw Mbona bado mdogo mimi.

Msaada
Nenda Muhimbili,The early the better.
 
Back
Top Bottom