Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Mkuu 'General', umeyasema mengi, baadhi yake nikikubaliana nayo.

Lakini niseme tu kwamba,'It is more complicated than that'!

Tundu Lissu ni jasiri, ndio, lakini watu hata kule kuvaa T-shirts' tu za kumwombea apone, watu waliogopa...

Mkuu,
Viongozi hao wapo, na hata sasa wapo.
Tatizo nionalo mimi, chadema haikuwekeza kwa wagombea majasiri katika jiji la Dar.

Dar ingepata vichwa vigumu kama Lissu, Lemma, Sugu, Heche zamani Chadema wangechukua Nchi.

Kumbuka na Mikoani huwa wanaiga yote yanayotokea Dar, sio kwenye siasa tu hata mambo mengine.

Sasa ukiangalia wabunge wa chadema wa Dar wote ni walaini kidogo mdee anajitahidi...

Nchi kubwa duniani mageuzi yanaanza mji mkubwa
 
Kwakweli mnalalamika mpaka roho inaniuma poleni sana wajameni ndio siasa hiyo jipangeni kwa uchaguzi ujao..

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Hakuna kujipanga, ccm na upinzani sasa Ni nyoka na binadamu. Visasi hadi dunia iishe.
 
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu
Nimeshuhudia wakala wa upinzani akifukuzwa katika chumba cha uchaguzi eti hana barua ya kiapo au barua haikuwa na mhuri wa tume. Je hili si tume imelipanga?
 
Nimeshuhudia wakala wa upinzani akifukuzwa katika chumba cha uchaguzi eti hana barua ya kiapo au barua haikuwa na mhuri wa tume. Je hili si tume imelipanga?
Mkuu 'Mtamamtete'.

Hilo tu la mawakala ilikuwa ni sababu tosha kabisa kwa CHADEMA na ACT kuzuia uchaguzi usifanyike.

Hii ilikuwa ni njia wazi kabisa ya kuharibu uchaguzi, lakini haieleweki kwa nini hawakulipa uzito stahiri jambo hilo.

Wananchi wangeelewa kabisa kwa nini uchaguzi usifanyike.
 
Habari wadau!

Baada ya kushuriki kikamilifu katika mchakato wa kusimamia uchaguzi pale maeneo ya Mwembe Chai nimejifunza mengi sana.

Hizi ndio siri za anguko la upinzani, kutokana na takwimu chache nilizozikusanya.
1. Mawakala wa vyama vya upinzani walitendewa haki ,waliridhishwa na mchakato kutoka zoezi linaanza la kufungua kituo mpaka kuhesabu kura na wakajaza vizuri form #14 na #16 wanazotakiwa kuzijaza kama wameridhika na mchakato au kutoridhika wote walijaza kuridhishwa na mchakato ,mwisho wa zoezi walipewa copy ya matokea toka kwenye form #21A ambayo walisahini matokeo.Hapa hakuna lawama kabisa.

2. Walioenda kupiga kura kwa vituo vingi vya Tanzania walikuwa wengi chini ya 50% hii ni kutokana na ukweli kwamba uchaguzi wa pili wa rais miaka mingi hauwi na wapigaji kura wengi maana wengi wanaamini kama rais yupo madarakani lazima hapite tu (dhana iliyojengeka), hivyo wengi ujiandikisha ili kupata vitambulisho dhana hii inafuta dhana ya kwamba kuna watu walizuiwa kupiga kura.

3. Vijana wamekuwa wanafiki sana hawajajitokeza kabisa kubiga kura ,na wengi wa vijana kama tunavyojua wengi ni washabiki wa upinzani, vituo vingi vilijaa wazee waliojihimu mapema SAA 12 wakapiga kura mpaka kufikia saa 9 vituo vingi hakukuwa na watu kwenye mistari maana wazee walimaliza jambo lao mapema wakaenda kupumzika ,wengi tunajua wazee wengi ni CCM.Inasikitisha vijana wengi walihamkia kwenye virabu vya pombe za kienyeji kama gongo na mbege tarehe 28 kwao ilikuwa kama birthday au sikukuu ya kura vyombo yaani hawakuona kama kuna zoezi la uchaguzi wao walijikita kwenye ulevi wa pombe za kienyeji harafu baadae ndio hao wanakuja kulalamika hapa mtandaoni shame on you guys ,jana mlikesha mkinywa mbege na ma double kick hamkuja kupiga kura Leo mnadai mmeibiwa, au mmeibiwa nyeti zenu?

4. Ukweli utabaki kuwa ukweli kampeni ya CCM ilikuwa ya kipekee iliyibeba ajenda, Sera na dira ya wapi Taifa linatoka na wapi linaelekea, pia chama kiliwekeza sana kwenye kampeni hivyo usitarajie kampeni ya buku ikakupa matokeo chanya ukamshinda mtu aliyewekeza mamilioni kwny kampeni.

5. Mawakala wa upinzani walisalitiwa na viongozi wao wenyewe Mawakala wengi hawakuletewa chai wala chakula cha mchana,kilichokuwa kinafanyika koongozi anakuja kumchungulia wakala na kumuhaidi atamletea msosi wa asubuhi then anapotea ikifika mchana hivyo hivyo anamuhaidi harafu hamletei chakula, ikafika point mpaka msimamizi unaingiwa na imani inabidi uagize msosi mnagonga wote au unambakishia sababu wengi wa hawa Mawakala ni majirani,ndugu na marafiki,class mate wetu hivyo wasimamizi walitambua kuna maisha baada ya uchaguzi.

Mwisho niitimishe kwamba hakuna haja ya wapinzani kupiga kelele wala kutishia kuandamana wafuate taratibu za kisheria kudai madai yao nakala za matokeo si wanazo zilizosainiwa na Mawakala wao.
 
Huyo hayupo nchini hivyo hajui kilichokuwa kinaendelea.

Vituo vingi hapa Dar hata kura hawakuhesabu walichokifanya ni kuwafukuza mawakala kisha wakatoa zile form walizojaza kabla ya uchaguzi na Kuwaita wake wazisaini.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Kumbe ndo ilikuwa hivyo? Au umeambiwa! Wewe umesikia wapi?
 
Mtendaji wetu aliwakubalia,ila siku ya mwisho akawambia watu,kafanye kazi kama kitabu cha tume kilivyoelekeza
 
Wakishinda wapinzani haki imetendeka, ila wakishindwa hakuna haki, tulia sindano iwaingie
Hatuna shida na ushindi wa haki. Naskitika sana na ninatubu kwa kubadilisha tarakimu. Wa kwanza kwa wa pili wa pili akawa wa kwanza. Sikuwa na jinsi. Nina watt na kujiweni ninakopatia tonge ndipo paliponipa hili dili.
Lkn moyoni tunajua ushindi huu umepatikanaje.
 
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu
Aisee usiseme tulioshuhudia haya tunaweza kuandika kitabu. Mawakala wa upinzani kituoni kwangu walitolewa nje kwa nguvu ya polisi na wakarudishwa kusaini. Walipotaka kukataa wakaambiwa hata wasiposaini anisaidie. Hivyo hawakusaini. Tulinyimwa kuwa na simu lkn uonevu kwa mawakala ulikuwepo sana . Mida mwingine hadi wakal a wa CCM usiye aminika unaotolewa nje. Kisha wanafanya yao ndio unaitwa kusaini.
 
Green guards walivalishwa mavazi ya polisi.
JKT walivalishwa mavazi ya polisi.
Na wale walioitwa jeshi la akiba walivalishwa mavazi ya polisi.

Kisha kazi ikaanza kuteka mawakala usiku, kuteka mawakala vituoni na kuingiza maboksi ya kura fake.

Wakati wa kuhesabu kura mawakala walitolewa zikaingizwa form walizojaza za matokeo.

Hata ukiyaangalia matokeo hayareflect uhalisia wenyewe.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
I feel sorry kwa ndugu zetu tuliowapa kazi ya uwakala.

Yaani hata kupepesa macho huwezi, kwenda washroom huwezi, kuinuka kunyoosha miguu huwezi, hata kwenda kununua vocha huwezi hawa mafisiM wamekaa wanakuwinda tu na mabegi yao. Na siku ilipoisha unatolewa nje wanaingiza mabegi.
 
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu
Unajikuta unaelewa sana yani, kana kwamba uelewa wako unaweza bishana na bunduki na ukashinda, mtu akiongea jambo lililomkuta jaribu kufikiri kwa makini kidogo na punguza ujuaji
 
Majuto ni mjukuu. Sasa mmeturudisha kwenye utawala wa Chama Kimoja. Sio peke yenu. Hata mawakala wa vyama vya upinzani wamechangia haya

Magufuli atasema ameshinda ila CCM na TANZANIA kwa ujumla tumepoteza
Hapana kwa mfano huku kwetu Mawakala wa Chadema wameruhusiwa saa 8 kuingia, wengine saa 2 wengine saa 5 n.k
 
Hakuna kitu. Kondoo ni kondoo tu hata wakiongozwa na nini. Hawawezi kuwa simba. Viongozi wapo na uonevu upo. Unahitaji tuuungane ili kuutoa. Sisi Watanzania ni wabinafsi. Hatuwasaidii viongozi wetu.
Mkuu, naamini kuna sababu ambayo (ambazo) bado hatuzijui kwa nini waTanzania wapo hivi.

Mimi naamini hata 'kondoo' wakipata msukumo wanaweza kufanya makubwa sana. Siri ni kujua ni nini kinaweza kuwasha mioyo ya waTanzania na kufanya maajabu.

Lakini ngoja nijaribu kukukumbusha.
Tuliwahi kwenda vitani kama taifa. Ni 'kondoo' hawa hawa ndio waliofanikisha vita ile ipiganwe kwa ufanisi

Hebu jaribu kukuna kichwa kuwatambua hawa 'kondoo'.

Tuachene na kufanya mahitimisho ya rahisi rahisi kulaumu, huku tukiwa hatuna ujuzi na tunayoyalalamikia.
 
Watu wengine mna vichwa vigumu sana. Hiyo ingesaidiaje kupambana na kura kupigwa majumbani na NECCM na kuletwa vituoni kwa mtutu wa bunduki ili zihesabiwe?
'Omusolo', nahisi unahitaji jibu la kina kidogo.

Ngoja nijaribu kwa kifupi tu:

CHADEMA na ACT-Wazalendo walijua kungali mapema sana kwamba hapatakuwepo na uchaguzi huru. Sasa sijui kama hili nawe utalikataa!
Dalili, viashiria, matamko yote toka CCM na hata NEC wenyewe yaliashiria kuwa hapatakuwa na uchaguzi wa Haki na Huru.

Linaloshangaza ni kwa nini hawakufanya maandalizi ya kuuzuia uchaguzi huu mara tu ilipobainika mbinu zinazotumiwa kuunajisi uchaguzi mzima.

Wakati huo ulikuwa ndio fursa nzuri kabisa ya kuuzuia uchaguzi usiendelee, kwa mfano wakala wao walipoanza kuzuiwa wasiingie kushuhudia uchaguzi. Utaruhusu vipi uchaguzi uendelee wakati shuhuda wako wa kuhakiki usahihi wa kura anapozuiwa asishuhudie?

Hili ni moja tu. Kuna mengi ambayo walipaswa kufanya kuzuia uchafuzi huu wa maksudi kabisa uliofanywa na serikali.

Acha nikuachie hapa, kwani nina tani nzima ya lawama juu ya waliyoyafanya CHADEMA na ACT-Wazalendo.

Wamewaangusha sana waTanzania.

Sasa ni kazi bure kuwahimiza waingie kwenye maandamano baada ya kuachia nafasi murwa kabisa!
 
Kam unahitaji msukumo, basi ni PM kesho nakupitia twende barabarani km unakaa Dar. Mnahitaji msukumo gani wakati uchaguzi umeibwa mchana kweupe? Mnataka Maalim, Lissu, Mbowe na Zitto wafanye nini?
It appears you're not serious my compatriot!
It's too late now.
 
kichwa cha habari usiweke wingi.

nimejikuta nimetype kwa chini nika amua kufuta ila punguzeni story maana huwa akili ikizoea hutofanya kazi
 
Msimamizi wa ngazi ya kata aliniuliza VP mbona umeleta matokeo ya hivi nikamwambia ulikuwa unataka yapi? Akaguna,nikamwambia Mimi nilienda kusimamia wapiga kura siyo kuleta kura! Akaniuliza mawakala umewapa nakala,nikamwambia wrote nimewapa,akaniambia umetuangusha maana kituoni kwangu mbunge wa ccm na baba take waliangukia pua.
 
Back
Top Bottom