Leo jiwe amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya.. hata hivyo huu mwaka ni wauchaguzi ndimbwendimbwe la uchaguzi bado lipo vululuvululu..
Lkn wengi imekuwa kama hawaushughulikii uchaguzi!.. hii yaonyesha uchaguzi wa mara huu umeathirika na kuwepo kwa covid 19,pia mifuko ya watu ni kama vile imekosa uhai maana pesa hakuna!.. pia imejengeka kama saikolojia kuwa rais hutawala miaka 10,hivyo hawaoni nafasi kubwa ya mtu mwengine kuupata urais kwa muda huu mchache wa miaka 5 tu!..
Mwaka 2020 umekuwa ni mwaka wenye matukio yasiyopendeza haswa kutokana na hili janga la covid 19,mdororo wa kiuchumi umeonekana hata ktk nchi kubwakubwa!.. hivyo hivi sasa nchi nyingi zimekuwa zikipigania kufufua uchumi ili maisha yaendelee kama kawaida.
Tanzania ni moja ya nchi iliyoathiriwa na covid 19,haswa ktk sekta ya utalii!.
Japo serikali imekuwa na misimamo yake lkn wapo wachache ambao wamekuwa wakipinga...
Itaendelea...