Tuliopoteza wapendwa wetu, ndugu, jamaa, au marafiki kwa nimonia/changamoto ya upumuaji tukutane hapa tupeane hali halisi

HUNIJUI SIKUJUI

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
1,335
1,509
sio siri ndugu zangu huu ugonjwa unaua sana hasa watu walio na umri mkubwa, nimempoteza shangazi yangu na mpaka sasa tupo kwenye shughuli za mazishi, alilazwa ghafla, tukaambiwa ameshindwa kupumua na sasa hivi nina hofu sana familia yangu isiwe inatoka nje hovyo, niwe natoka mimi tu!

wazazi wangu bado wananipa hofu sana ,kiufupi ndugu zangu naona mda wowote anaweza kufa yoyote nipo nimeshikilia moyo

epukeni misangamano, vaeni barakoa, usipige misere sana kama sio lazima, mutation inatokea kama variant ya kwanza ilikua imetulia, a more deadly variant is coming na sisi tuko vilevile tu tukiamini jamaa ni yuleyule, kumbe kila siku anaumiza kichwa na anajipanga aje kwa staili gani kali zaidi atuchote wengi

captain amekimbia chombo,hata kutoa tahadhari tu ya kwamba chombo kinazama hakuna! jiokoe wewe na nafsi yako kwa njia unazozijua! every man for himself now

na wale mliowahi kuugua huu ugonjwa mkatoka salama mnaweza kushea pamoja na sisi ilikuaje na mlifanya nn mpaka mkafanikiwa!

USIOMBE YAKUKUTE
 
Kaka ni kweli hali hali ni mbaya kwa mujibu wa shuhuda nyingi nilizokutana nazo mitandaoni, lakin nashauri ni vyema tukapeana mbinu jinsi gani tunaweza kujikinga na janga hili. Habari za kuleta ushuhuda ni kuzidi kupeana hofu hali inayoweza kusababisha kushusha kinga za mwili na kuongeza athari zaidi.
 
vaa barakoa, epuka misongamano, familia kutokatoka nje acha, toka ww au mkeo pale inapobidi kabisa, nunua stock ya kutosha weka ndani watoto punguza kucheza nje hovyo
 
NYUMONIA KALI ATTACK LEVELS

Level 1 - Inatibika
Mwili kuchoka
Maumivu ya mwili mzima na viungo
Kichwa kuuma & Kizunguzungu

Level 2 - Inatibika
Kukosa hamu ya kula
Kushindwa kunusa harufu
Homa
Kikohozi
Kukosa pumzi (Kupumua kwa shida)

Level 3 - Hatari na ngumu kutibika
Kifua kubana
Makohozi yenye damu au njano nzito
Kushindwa kupumua/Kukosa hewa
Homa kali
Mapafu kujaa maji (Pneumonia)

Tuchukue tahadhari tafadhali
[/color][/color]
 
daah hatari sana. Maana kutimiza hayo ni kutofanya majukumu ya Kila siku
shida ni kwamba kila kukicha hicho kijamaa kinajipanga upya kuumiza zaidi, kama wave ya kwanza ilikua poa, jinsi kinavyozidi kubadilikika ndo kinaua zaidi
 
vaa barakoa, epuka misongamano, familia kutokatoka nje acha, toka ww au mkeo pale inapobidi kabisa, nunua stock ya kutosha weka ndani watoto punguza kucheza nje hovyo
Wakati huo watoto wanatakiwa kwenda Shule kuhudhuria vipindi.
 
ndiyo tabia ya virus katika DNA replication wao hawana process ya proofreading ya nucleotides pairing sequence, hivyo wana undergo mutation kirahisi
adui anabadili mbinu, alafu sisi tupo vile vile, uko mbeleni inaeza kuja kutokea viriant ambayo ikukupata sio kulazwa tena ni kifo moja kwa moja
 
adui anabadili mbinu, alafu sisi tupo vile vile, uko mbeleni inaeza kuja kutokea viriant ambayo ikukupata sio kulazwa tena ni kifo moja kwa moja
Hapa ni vaccination tu hakuna namna ingawa napo Kuna utata hasa wa huyu kiongozi wa nchii, yeye hana imani na mabeberu kabisa lakini pamoja na kukosa imani nao.binafsi hatuoni akichukua hatua zozote za kisayansi kukabiliana na changamoto hii zaidi ya kupiga nyungu. Ujue Kuna mambo mengine yatupasa kuacha taaluma husika ifanye kazi hii hali yakuleta siasa kwenye kila jambo si zuri kabisa
 
Dah ,huu ugonjwa unaumiza sana ,ndugu yetu katutoka jana tu kwa kubanwa na pumzi leo hii tunamsafilisha kwenda ziwani ziwani nyasa kwa mazishi
poleni sana ndugu zangu, maana hali ni mbaya kutokana na shuhuda mbalimbali zinazotolewa na wadau kwenye mitandao ya kijamii. Tuendelee kuchukua tahadhari na kumuomba Mungu atuepushe na kikombe hiki maana hali hali ishakuwa tete.
 
NYUMONIA KALI ATTACK LEVELS

Level 1 - Inatibika
Mwili kuchoka
Maumivu ya mwili mzima na viungo
Kichwa kuuma & Kizunguzungu

Level 2 - Inatibika
Kukosa hamu ya kula
Kushindwa kunusa harufu
Homa
Kikohozi
Kukosa pumzi (Kupumua kwa shida)

Level 3 - Hatari na ngumu kutibika
Kifua kubana
Makohozi yenye damu au njano nzito
Kushindwa kupumua/Kukosa hewa
Homa kali
Mapafu kujaa maji (Pneumonia)

Tuchukue tahadhari tafadhali
[/color][/color]
🤔🤔🤔 Nafikiri Niko level ya pili
 
poleni sana ndugu zangu, maana hali ni mbaya kutokana na shuhuda mbalimbali zinazotolewa na wadau kwenye mitandao ya kijamii. Tuendelee kuchukua tahadhari na kumuomba Mungu atuepushe na kikombe hiki maana hali hali ishakuwa tete.
Asante ,Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom